Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,304
- 12,965
Asubuhi nilitoa mada yenye kichwa "Tunasubiri kuona busara ya jeshi la polisi wakati wa kurejea kwa Lissu"
Niseme wazi kwa mara ya kwanza jeshi la polisi limetumia busara kubwa kutozuia na kuingilia mapokezi ya Tundu Lissu.
Hiki ndicho wengi tulikuwa tuna kitaka. Polisi wakijiweka kando katika shughuli za kisiasa na kijamii huwa hakuna vurugu wala madhara mpaka pale wao wanapofika na mabomu yao, virungu na bunduki kuanza kutumia nguvu kwenye dhughuli zisizo kuwa na vurugu.
Kwakweli kuna haja ya jeshi kuendelea na utamaduni huu. Waacheni watu wafanye shughuli zao za kulia na kucheka bila kuwaingilia kwa kisingizio cha mikusanyiko.
Kwa muda mrefu polisi na CDM wamekuwa kama wake wenza wanao gombea mume kila siku vitisho na ugomvi Polisi wakiwa ndio chanzo. Polisi kwa leo mmeonesha busara kwa mara ya kwanza.
Namsifu pia mkuu mpya wa mkoa wa Dar es Salaam kwa busara kubwa aliyoionesha kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa. Ingekuwa ni yule bwana masifuri leo ingekuwa ni vilio na kusaga meno. Well done!