Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,491
- 51,073
Kama kuna kitu pengine utakiita ni Legacy katika utumishi wako kwenye wizara ya Mazingira, basi hii sheria ya Mifuko ya Plastiki ni Achievement kubwa sana kwako.
Nchi iligeuka dampo la manailoni, mito iligeuka mhanga kwa watu kutupa mifuko hiyo, Watu walivuta hewa chafu zenye uwezo wa kuathiri afya baada ya mifuko hiyo kuchomwa.
Akina Mama ntilie walipika Wali mtaani kwa kufunikia manailoni!, Hatari ilioje. Leo utafiti unaonyesha Wilaya ya Kinondoni ina tatizo la watu kuwa na upungufu wa nguvu za kiume, sababu mojawapo bila shaka ni hii ya kula chakula kinachopikwa kwa kufunikiwa manailoni ( utafiti unaonyesha kuna uhusiano wa electyle dysfunction na matumizi ya vyakula vilivyomo kwenye mifuko ya plastiki hususan baada ya kupitishwa kwenye joto kali).
Nakuomba bwana Makamba kwa kushirikiana na mamlaka nyingine zinazohusiana na vyakula upige marufuku upishi wa kufunikia nailoni, hii ni hatari kwa afya za walaji
Serikali isikubali kurudi nyuma, hakuna faida zozote za kiuchumi zinazoshinda thamani ya Mazingira!
Katika hili jambo serikali imefanya uamuzi makini na sahihi, na iangalie pia chupa, Kama Bia zinaweza kuuzwa kwenye chupa za glass basi turudi katika utamaduni wa zamani wa soda kuuzwa kwenye chupa za glass pia.