Engineer Mohamed
JF-Expert Member
- Jul 27, 2007
- 451
- 9
Hongera Jaji Munuo
kwa niaba ya wana JF wenzangu tunakupa hongera sana kushika wadhifa huo mkubwa.
source http://www.majira.co.tzJAJI Eusabia Munuo wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania ameteuliwa kuwa makamu Rais wa Chama cha Majaji Wanawake Ulimwenguni (IAWJ).
Uteuzi huo uliotangazwa jana kupitia taarifa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu wa Chama Cha majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) Jaji E. A Kileo na kueleza kuwa uteuzi huo unaanza mwaka 2008 hadi 2010.
Taarifa hiyo ilisema kuwa uteuzi wa Jaji Munuo umetokana na juhudi zake kiutendaji katika na kusimama kidete katika kutetea haki na usawa kwa watu wote ndani ya jamii.
Tunachukua nafasi hii kumpongeza Jaji Munua kwa heshima kubwa aliyotunukiwa ambayo inazidi kung'arisha sifa kubwa ya Tanzania mbele ya mataifa mengine duniani.
Watanzania wana kila sababu kujivunia uteuzi wa Jaji huyu ambayo unazidi kuandika historia kwa wanawake wa Tanzania kuzidi kuaminika na kupewa majukumu makubwa kimataifa.
Jaji Munuo ni miongoni mwa wanawake wa Tanzania waliokabidhiwa dhamana kubwa kimataifa hivyo rai yetu ni kumtaka aendelee na moyo wake wa uchapaji kazi na ikibidi sasa aongeze mara mbili zaidi ili kuzidi kuwajengea sifa wanawake watanzania na Taifa kwa ujumla.
Miongoni mwa wanawake walioshika dhamana kimataifa kwa uchache ni pamoja na na Katibu Mkuu Msaidizi wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha Rose Migiro, Rais wa Bunge la Afrika, Dkt. Getrude Mongela na Mkurugenzi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo ya Makazi la Umoja wa Mataifa, Profesa Anna Tibaijuka.
Tunazidi kumtakia mafanikio makubwa Jaji Munuo katika kutekeleza jukumu hilo na kila analofanya akumbe kwamba amebeba heshima na ni kilelezo cha mamilioni ya Watanzania.
kwa niaba ya wana JF wenzangu tunakupa hongera sana kushika wadhifa huo mkubwa.