Hongera sana Dr Slaa ;Ujasiri wako unatisha

Status
Not open for further replies.
Mzee wa gongo...
Vipi kampeni ya TOKOMEZA UJANGIRI?Wale watu hawakupata ile kitu kweli?Maana hata wakoloni wetu wawili Mjeruman na Mwingereza hawakuwahi kutenda dhambi kubwa yakutisha hivyo.Hamja laaniwa kweli nyinyi?Nafkiri laana ya Mwangosi inawatafuna
 
watu wanaangalia gongo tu bila kujua Dr Slaa alikuwa ana maanisha nini; hebu angalia mambo yafuatayo ili kujua kiongozi mwenye mawazo mbadala wa kuokoa afya za watu na kutengeneza kipato halali kwa wananchi wake;
1)Watu wengi ni maskini wanakunywa gongo kwa kuwa ni bei rahisi kuimudu,
2) fedha za gongo zinachukuliwa na mapolisi kwa njia ya rushwa
3)Gongo inatengenezwa katika mazingira machafu hivyo kuhatarisha afya za wanywaji
4) CDM ikiingia madarakani itawaagiza SIDO watengeneze mitambo ya kutengeneza gongo kwa njia ya usafi

Mkuu ulisha wahi kuonja gongo? Au unapiga debe wengine wanywe?????
 
Ujasiri wa kuhalalisha gongo?

Hivi unajisikiaje kupost ujinga kila saa ndani ya mkusanyiko wa watu makini? Mbona unaonyesha una muda mwingi usio na faida?
Au wewe ni mwehu tukusamehe tuu? Najua waweza kuwa mwehu usijijue,pse kama unajirani muulize hali yako ya kiakili anaionaje? Akisita kidogo ujue ndio jibu then TAFAKARI au kuwa wazi tukusaidie.
 
Ujasiri wa kuhalalisha gongo?

Tanzania tumechelewa mambo mengi. Nchi zingine wameruhusu biashara mpaka za ngono na kodi yake tunapewa msaada sisi tusiopenda na kukemea ngono! Naunga mkono hoja na ikiwezekana aruhusu na bangi. Hakika kwa ruhusa ustaarabu utakuwapo kuliko sasa. Gongo na bia si sawa tu?
 
Dr. hata ndani ya makambi ya jeshi anakubalika sana. Kutana nao utasikia wakimkubali na ndo maana uchaguzi 2010 alipata kura nyingi maeneo yote wanayoishi wanajeshi, hasa Kibaha yote mpaka Mlandizi, Lugalo na Makongo Gongolamboto. By the way watu wamejengewa hofu hasa kwa kazi za ajira kwa watu wasiokuwa na professional kama hao wa Lumumba wenye elimu ya chuo cha kivukoni

Mkuu umenena,hata jeshini wanamkubali ile mbaya,sema sheria za jeshi haziruhusu siasa. Wanasema sisis wananchi ndo tunawaangusha
 
Naona ufipa buku 2, mpo kazini, kujitekenya na kujichopeka dole halafu mnacheka wenyewe eeenh! Mmebakiza tu kusema slaa we handsome!!
 
Ujasiri wa kuhalalisha gongo?
hoja zenu za kitoto ndizo zinazoimaliza ccm akusaidii kitu kutoa hoja ya kitoto mbele za watu makini yaani ni sawasawa unamwambia mtu mzima kichwa kama train alafu unategemea watu wataona eti umeongea kitu cha msingi, chadema inapendwa kutokana na viongozi wake kuongea mambo yenye maana,sasa nyie kalieni kusema upuuzi wenu faida yake mtaiona
 
Nimeona nitumie JF kumpongeza Dr Slaa kwa kufanya ziara yenye mafanikio makubwa.Wako watu ambao kwa hisia zao walionekana ni wana ccm,walikutisha usifanye ziara hiyo hasa Kigoma na wakasema unaweza hata kupoteza maisha.
Ripoti tulikuwa tukizipata humu kwenyeJF,wakisema vijana wameandaliwa kukumaliza hali ambayo kwa mtu mwoga angeweza kukimbia.Kuna kipindi tulipokuwa tunafuatilia kupitia humuJF walisema Vijana wanapewa 5000 waandamane kukupinga na kweli walitokea na mabango lakini hukutishika.Kijana mmoja alipo hojiwa alionekana nimtoto wa katibu mwenezi wa ccm huko Kigoma hali iliyo toa taswira kama ccm walikuwa nyuma ya upinzani huo.
Ni mambo ambayo ametuhumiwa hata Zito kuwa anafanya uasi kuhujumu cdm.Lingine ambalo linanishawishi nikwamba,kwa chama kama cdm ndiyo kwanza kinajijenga,isingekuwa rahisi kumuonea kijana kama Zito aliye kuwa hodari na jasiri katika chama.Katika vita kamanda hodari sindiyo anafaa kwanini umfukuze?Siamini kama cdm ni wajinga hivyo kupoteza nguvu kazi kubwa namna hiyo.Huenda kwa sasa wamepima faida na hasara za kijana huyo na wakaona afadhali kukaa mbali nae.Haya ni maoni yangu wakuu kama mfuatiliaji wa humu kwenye JF.

Kwakuliona hilo nakulisema hilo nawewe unastahili pongezi umefanya hivyo kwa nafasi yako katika kujenga na kuleta maendeleo yakweli.hongera sana mkuu.
 
Na bado mtakataana sana mwaka huo mpya.
Siku zote walivyokuwa wakijaa kwenye mikutano yenu hapo nyuma hamkuwaita majina msiyoyapenda ila leo hii mnawaita ni wanaccm.
Nyie kukataana hamjaanza leo.
Halafu mie huwa nawashangaa sana,ivi nyie chadema mnadhani wananchi mmewakatia hati miliki?eti mkutano wa slaa waje na mkutano wa wengine wasiende.
 
Binafsi namkubali Dr. Slaa, kwa wale wanaojua profile yake watakubaliana nami, Nakumbuka aliwahi kumwadabisha askofu kwa kupotoka.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom