Hongera sana Dr. John Pombe Magufuli, Rais wetu Ajaye wa Awamu ya Tano

Musoma

Senior Member
Oct 12, 2010
137
221
Nakumbuka mwanzoni mwa mwaka 2005 tukiwa tunajiandaa kufanya UE (University Exams) pale Mlimani ,kulitokea kama kamgomo baridi fulani hivi ka Daladala zilizokuwa zikitokea Mwenge kwenda Ubungo kupitia Chuo.

Basi siku hiyo mimi na rafiki zangu wawili tulikuwa tumesimama pale Utawala tukisubiri gari lolote litakalopita hapo tuombe lift litusogeze Ubungo ama Mabibo Hostel yalipokuwa maskani yetu!

Baada ya kusimama pale kwa muda kidogo mara nikaliona Mercedez Benz jeusi linakuja nikalipiga mkono,likapunguza mwendo na kupaki pembeni .Dereva wa gari lile akafungua mlango na kutoka kutufuata ,alikuwa amevaa suruali ya jeans ya blue,raba nyeupe, fulana yenye mistari mithili ya pundamilia na kichwani alikuwa amevaa kofia la pama kama lile la Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayadit.

Baada ya kutusogelea kwa karibu tukamtambua ,mimi na rafiki zangu wale tukamsalimia na yeye akatuuliza kuna shida gani pale Chuo siku ile, kwani ameona hali si ya kawaida na wanachuo wako katika makundi makundi! Tukampa picha ya pale kisha naye akatumbia alikuwa katika zoezi la kukagua barabara iliyojengwa kutoka Survey hadi Gate Maji.

Baada ya maelezo yale akatoa “offer” ya kutupa lift hadi Mabibo Hostel.Wakati anafungua mlango kuingia kwenye gari lake wale rafiki zangu wakaniambia kwa utani, wewe kaa mbele na Waziri mwenzako sisi tutakaa siti ya nyuma! Yule Dereva akaniuliza kumbe na wewe ni Waziri hapa Mlimani ?,nikamjibu ndio mimi ni Waziri wa Fedha hapa.

Katika mazungumzo yetu huku akiendesha gari lake taratibu na kwa kuwa alikuwa “simple” siku hiyo nikapata ujasiri nikamuuliza ;vipi Mheshimiwa kuhusu afya yako maana tulisikia juzi kati hapa kuwa umekula sumu Dodoma na ukakimbizwa Ujerumani kwa matibabu ya haraka?,akanijibu ! kisha nikamuuliza tena ,vipi mwaka huu “unaingia ulingoni ?” akanijibu ,hapana muda wangu bado ,bado navuta pumzi. Huyo Dereva hakuwa mwingine bali ni Dr.John Pombe Magufuli.

Usiku ule nilipomwona Dr.John Pombe Magufuli akiingia ukumbi mpya wa Mikutano wa CCM huku wajumbe wa mkutano mkuu wakimshangilia kwa vifijo na nderemo nilibaki nimeduwaa! Nikajisemea moyoni kumbe Ndugu huyu anajua kuzichanga karata zake vizuri namna hii!

Sikuamini kama kweli Dr.John Pombe Magufuli alikuwa anaelekea kutimiza ndoto yake ya siku nyingi kirahisi namna ile! Hata kwa mtu ambaye kwa mara ya kwanza alikuwa ameingia Tanzania kutoka sayari nyingine na akaibukia kwenye Mkutano Mkuu wa CCM pale Dodoma angeona dhahiri ushindi wa Dr.Magufuli usiku ule.
Yeye binafsi alifurahi kupitiliza na wengi mliona hata hotuba yake ya kuomba kura ilitaka kukosa format nzuri kwa kuwa alikuwa “overwhelm”!

Anayesema Dr.John Pombe Magufuli kaokota “Urais” hamjui vizuri Dr.Magufuli ! Ni mtu aliyejua anachotaka na katika mchakato wa kumtafuta mgombea Urais ndani ya CCM alicheza kete zake kama vile Eddie Murphy ( Hakeem) mtoto wa Mfalme wa Bemunda kwenye ile movie y a “COMING TO AMERICA” alivyom-win Lisa binti ya yule Tajiri mwenye Hotel.

Hata magazeti ya hapa nyumbani ambayo mengi ni ya kishabiki na kufuata mkumbo tu hayakumpa “attention”isipokuwa gazeti moja tu la Raia Mwema ndilo lilionekana kunusu “harufu “ ya Dr.John Pombe Magufuli.Nalipongeza gazeti la Raia Mwema na nakiri waandishi wake ni watu mahiri sana,na pia nahisi wako karibu na watu wa “KITENGO”.

Kuibuka kwa Dr.John Pombe Magufuli kama mshindi wa kinyang’anyiro cha mgombea Urais ndani ya CCM kumenifanya niendelee kuiamini CCM kama taasisi makini na yenye watu makini sana na kwa hili JAKAYA ni “fundi”.

Dr.Magufuli alitafuta wadhamini ndani ya Chama kama mtu mwenye maelekezo fulani! Sasa utasemaje kuhusu kauli kama ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Mzee Philip Mangula aliyoitoa siku chache kabla ya vikao kuanza Dodoma kuwa,” Mgombea wa CCM hajinadi,atanadiwa na Chama”.

Kwa hili Hongera sana Jakaya,Hongera sana CCM! Mmethibitishia Ulimwengu kuwa CCM ni taasisi imara na makini na hakuna mtu mmoja mkubwa kuliko CCM! Heshima ilioje!!!!!!!?

Nilichojifunza zaidi ni kuwa Dr.John Pombe Magufuli ni mwanasiasa mjanja sana ambaye anajua kutafuta anachotaka! Na katika hili nimempa “A” plus kama nilivyompa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya!

Kumbuka mwaka 2007 Uhuru Kenyatta aliulizwa kwa nini hagombei Urais yeye akajibu kuwa hawezi kugombea kwa kuwa hana uhakika wa kushinda na akaamua kumuunga mkono Rais Mwai Kibaki.

Sote tunakumbuka alichomfanyia Raila Amolo Odinga mwaka 2013! na sasa masikini Raila Amolo Odinga upepo unaonyesha nafasi yake ya kuikanyaga Ikulu ya Nairobi kama Rais wa Nchi hiyo imekuwa “reduced to ashes”!

Kwa kifupi Dr.John Pombe Magufuli amefuzu mafunzo yote ya mwanamapinduzi wa China Sun Tzu katika kitabu chake cha “The Art of War”. “He knows how to choose his battles wisely”. Na kuna wisdom ambayo amewashinda wapinzani wake nayo ina state kwamba,”Even if you are interested in something,don’t show to others that you are dying for it”. WATAKUKWAMISHA TUUU!

Hongera sana Dr.John Pombe Magufuli ,Rais wetu ajaye wa Awamu ya Tano.
 
Pole sana. Porojo zako hazina msaada wowote kwa CCM na Magufuli. Mwaka huu ni kilio tu kwa CCM na Magufuli.
Acheni kumpa faraja za kinafiki Magufuli wakati hali ni mbaya sana kisiasa. Mwambieni ukweli Magufuli ili ajipange na sio kumpa matumani hewa hapa.
 
Musoma

Hongera sana kwa uchambuzi makini.Ulichosema ndio ukweli wote kuhusu JPM.big up
 
Last edited by a moderator:
Baada ya kutafakari kwa kina, Na kwa muda mrefu sana.... Nimeamua Kumpigia kura edwardlowassa kuwa Rais wangu wa awamu ya tano wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania bila kujali kashfa zake. Kama kweli alikuwa ana hatia, hao wanaohubiri kashfa hizi ndio waliotakiwa kumfikisha mahakamani.

Nimeamua kwa Moyo mweupe, Akili Timamu, Bila kushawishiwa na kwa uthabiti kumpigia Lowassa kura kwasababu zifuatazo; - Hatia yake ingethibitishwa na Mahakama pekee.
-Wanaomtuhumu leo (CCM) na serikali walitakiwa kumfikisha mahakamani.
.
-Chini ya CCM wanafunzi wanakaa chini

-Chini ya CCM huduma ya Maji ni shida

-Chini ya CCM rushwa na ufisadi umekita mizizi.

-Chini ya CCM shilingi imeporomoka na kufariki.

-Chini ya CCM huduma ya Afya ni shida

-Chini ya CCM Wajawazito wanajifungulia chini mahosptalini

-Chini ya CCM gharama za maisha zimepanda kukithiri.

-Chini ya CCM ajira hakuna kwa wasomi.

-Chini ya CCM viwanda vimekufa

-Chini ya CCM mashirika ya Umma yamekufa.

-Chini ya CCM Rasilimali zinatumika hovyo.

-Chini ya CCM Twiga wamepanda ndege bila kuonekana na rada.
Hawa twiga sijui walikuwa na Passport!

-Chini ya CCM waandishi wa habari wameuawa.

-Chini ya CCM maelfu ya wanavyuo hawana mikopo

-Chini ya CCM Elimu ya kuanzia shule ya Msingi hadi Chuo kikuu imeshuka kiwango cha ubora.

#3N
-NIMEJIANDIKISHA
-NIMEJIAPANGA
-NITATUMIA KIKATIO CHANGU VIZURI
 
Last edited by a moderator:
Ndio maana chuo kikuu cha daslam miaka hii ya kikwete kimeshuka thamani na madaraja afrika kumbe vilaza kama wewe ndio wanapewa uwaziri pale chuoni.

Kama chuo kinaweza kua na vilaza kama wewe mawaziri unategemea kitapanda hadhi kweli, nilikua najiuliza kwa nini chuo kikuu miaka hii kimekua hivi kumbe ni chaka la vilaza.
 
  • Thanks
Reactions: rr3
Huu ni ukweli mchungu kwa mafisadi michadema ikiongozwa na fisadi papa Lowasa lakini mwaka huu wataumbuka na mipesa yao ya ufisadi.
 
Baada ya kutafakari kwa kina, Na kwa muda mrefu sana.... Nimeamua Kumpigia kura edwardlowassa kuwa Rais wangu wa awamu ya tano wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania bila kujali kashfa zake. Kama kweli alikuwa ana hatia, hao wanaohubiri kashfa hizi ndio waliotakiwa kumfikisha mahakamani.

Nimeamua kwa Moyo mweupe, Akili Timamu, Bila kushawishiwa na kwa uthabiti kumpigia Lowassa kura kwasababu zifuatazo; - Hatia yake ingethibitishwa na Mahakama pekee.
-Wanaomtuhumu leo (CCM) na serikali walitakiwa kumfikisha mahakamani.
.
-Chini ya CCM wanafunzi wanakaa chini

-Chini ya CCM huduma ya Maji ni shida

-Chini ya CCM rushwa na ufisadi umekita mizizi.

-Chini ya CCM shilingi imeporomoka na kufariki.

-Chini ya CCM huduma ya Afya ni shida

-Chini ya CCM Wajawazito wanajifungulia chini mahosptalini

-Chini ya CCM gharama za maisha zimepanda kukithiri.

-Chini ya CCM ajira hakuna kwa wasomi.

-Chini ya CCM viwanda vimekufa

-Chini ya CCM mashirika ya Umma yamekufa.

-Chini ya CCM Rasilimali zinatumika hovyo.

-Chini ya CCM Twiga wamepanda ndege bila kuonekana na rada.
Hawa twiga sijui walikuwa na Passport!

-Chini ya CCM waandishi wa habari wameuawa.

-Chini ya CCM maelfu ya wanavyuo hawana mikopo

-Chini ya CCM Elimu ya kuanzia shule ya Msingi hadi Chuo kikuu imeshuka kiwango cha ubora.

#3N
-NIMEJIANDIKISHA
-NIMEJIAPANGA
-NITATUMIA KIKATIO CHANGU VIZURI
Kama unaishi kwa fadhira za mafisadi kama wewe lazima usifie mafisadi halina ubishi lakini wewe na baba zako mafisadi mkiongozwa na fisadi Lowasa mtakura za migongo mpaka basi.
 
Ndio maana chuo kikuu cha daslam miaka hii ya kikwete kimeshuka thamani na madaraja afrika kumbe vilaza kama wewe ndio wanapewa uwaziri pale chuoni.

Kama chuo kinaweza kua na vilaza kama wewe mawaziri unategemea kitapanda hadhi kweli, nilikua najiuliza kwa nini chuo kikuu miaka hii kimekua hivi kumbe ni chaka la vilaza.
Mafisadi mnakazi kweli kujitetea mwaka huu hivi kwasasa huyu fisadi mwenzenu anawapa kiasi gani kwa siku najua huwezi kuishi bila usaidizi wa mafisadi.
 
Bila shaka unatafuta kiki ili kama akibahatisha kwa wizi wa kura na wananchi wakaamua kumsamehe basi akukumbuke!!Tafakari,chukua hatua!!
 
Pole sana. Porojo zako hazina msaada wowote kwa CCM na Magufuli. Mwaka huu ni kilio tu kwa CCM na Magufuli.
Acheni kumpa faraja za kinafiki Magufuli wakati hali ni mbaya sana kisiasa. Mwambieni ukweli Magufuli ili ajipange na sio kumpa matumani hewa hapa.

Magufuli yuko busy kariakoo anachagua laptops za waalimu..Bure kabisa hili jamaa mi nilidhani ana kichwa kikubwa ana akili kumbe kimejaa nzi tupu..we wanafunzi hawana madawati unaanza kusema mambo ya laptop si wendawazimu huo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom