vyuku
JF-Expert Member
- Mar 30, 2012
- 503
- 85
Kwa kipindi kirefu sana wananchi wa jimbo la Arumeru Magharibi hawakuwahi kupata mtu wa kuwasemea bungeni kwa matatizo mengi sana waliyonayo licha ya kuwa wana mbunge(chadema) ambae hajawahi hata mara moja kujitokeza jimboni kwake na hivyo kuwafanya wananchi wa Arumeru Magharibi kutomjua mbunge wao na kuwa wakiwa.
Mh Amina Mollel ni mbunge wa viti maalum Arusha kupitia watu wenye ulemavu,amekuwa mstari wa mbele bungeni kuwasemea wana Arumeru,aliwasemea kuhusu hospitali ya nduruma na kweli wakapatiwa milioni mia tano na sasa imekuwa hospitali bora hasa kwa wakina mama wajawazito,pia aliwasemea kuhusu hospitali nyengine hukohuko Arumeru na wakapatiwa milioni mia nne na kazi inaendelea ,aliwasemea suala la maji yenye floride kila siku bungeni ambayo yanasababisha ulemavu wa kupinda miguu na migongo kwa watumiaji, istoshe leo mbele ya Mh Rais Magufuli amemuomba tena suala la barabara inayosumbua sana kwa ubovu Arumeru, na bila hiyana Mh Rais amekubali ijengwe barabara hiyo na kuipandisha barabara hiyo na kuwa ya mkoa na kutoa amri ianze haraka kutengenezwa.
Leo tunawashuhudia wananchi wa Arumeru wakitarajia kunywa maji safi baada ya kufunguliwa rasmi mradi wa maji safi na Mh Rais.
Hii yote ni kwa juhudi za mbunge wa viti maalum Mh Amina Mollel kuomba mara kwa mara bungeni hatimae amefanikiwa.
Hongera sana jembe la Arusha Amina Mollel kwa uthubutu baada ya wana Arumeru Magharibi kwa miaka mitatu kukosa wa kuwasemea kimaendeleo japo kuwa wana mbunge wao.