Hongera RPC wa Mbeya kwa harakati za kudhibiti dawa za kulevya

getrusa

JF-Expert Member
Aug 16, 2013
2,150
1,821
Wakuu napenda kutoa mrejesho na shukrani kwa jeshi la polisi mkoani Mbeya, kwa operation waliyofanya ya kukamata watengenezaji wa gongo na wauzaji wa madawa ya kulevya.!! HONGERA RPC Mbeya na timu yako.

Najua huenda eneo la mama John hakitakuwa kituo cha madawa tena!

Binafsi nashukuru pia JamiiForums kweli mnatimiza wajibu wenu.
 
Huyo Mama John mwenyewe kakamatwa?
Maana nimesikia yule jamaa mwenye famasi anaitwa Maranatha kakamatwa!!
 
Nasikia hali ilikwisha kuwa mbaya nchini hadi hayo madawa ya kulevya yakawa yanauzwa pharmacy
 
Kuna eneo linaitwa mams John, ilikuwa ni shida kila mtu alikuwa akijua kuwa ni center ya drug.! Na gongo hope haitakuwa Nguvu ya soda.
 
Aisee jamaa alianza kufanya mambo makubwa sana .alijenga ghorofa mwanjelwa pale kwa haraka sana .kumbe jamaa alikuwa frug dealer?.
 
Aisee jamaa alianza kufanya mambo makubwa sana .alijenga ghorofa mwanjelwa pale kwa haraka sana .kumbe jamaa alikuwa frug dealer?.
Ukimuona jamaa mwenyewe kama mlokole lakini bonge la brazamen,na ana mama batoto wa nguvu sana,ila jamaa mwenyewe ni mpole sana huwezi zania yaani yeye na mkewe ni watu wakimya na wapole sana ila siwezi kuwahukumu kwa makosa hayo hadi wafunguliwe kesi na hukumu itolewe.
 
RPC hapo stand kuu ya mabasi yaendayo mikoani patazame kwa macho makali tuma vijana wako
 
Acheni wivu nyie watu wa mby ..sio destur yetu iyo mambo waachieni watu wa pwani..mtu maendeleo kidogo utasikia madawa ya kulevya au freemason..
Chapeni kazi..
No research no right to say..ndio maana jana Mshimiwa Waziri Mkuu ame onya..sio kutumia fimbo ya madawa kuchafuana
 
RPC hapo stand kuu ya mabasi yaendayo mikoani patazame kwa macho makali tuma vijana wako
Yaani nawapongeza polisi wetu. Baada ya rais kutamka tu nimeshangaa mara bangi, gongo, madawa n.k fasta fasta tu. Hivi ni kweli wamegundua au?
 
Wakuu napenda kutoa mrejesho na shukrani kwa jeshi la polisi mkoani Mbeya, kwa operation waliyofanya ya kukamata watengenezaji wa gongo na wauzaji wa madawa ya kulevya.!! HONGERA RPC Mbeya na timu yako.

Najua huenda eneo la mama John hakitakuwa kituo cha madawa tena!

Binafsi nashukuru pia JamiiForums kweli mnatimiza wajibu wenu.
Mkoa wa mbeya naamini wanafanya kazi kwa kuzingati taaluma zao,naona mkuu wa mkoa ,mbunge,RPC wanashirikiana kwa kiasi ndio maana naona kama kumetulia ingawa kuna upinzani kwa sehemu kubwa nadhan kuna elekea kuwa kama moshi sasa kama shetani asipo tia mikono yake huko.
 
Back
Top Bottom