Hongera Regia, Mbunge kupitia viti maalum CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Mdogo wangu tumekuombea sana. Sasa prove kuwa unaweza. Tembelea jimboni ulipokuwa unagombea, toa shukrani kwa kukuchagua ingawa 'orijino komedi' ameiba kura zako. Fanya uliyoyaahidi kwa kadri unavyojaliwa. Mimi nitakuchangia shilingi 20,000. Tuwasiliane kupitia 0754 275305.

Nakupenda sana mdogo wangu. Mungu amewaumbua wezi wa kura zako.
 
katika hali halisi ya maisha mtu anayekukosoa hukusaidia kujijenga na kujua wapi urekebishe nafikiri kiranga alipokuwa anamkosoa regia kulingana na muono wake alikuwa anamsaidia vile vile kujua wapi anatakiwa arekebishe kulingana na maoni ya kiranga. Bado naamini rafiki wa kkweli ni yule ambaye yuko tayari kukosoa udhaifu wako hivyo sio busara kuingiza kiranga na regia kwenye mada hii itakuwa ni kuwavunjia heshima wote wawili. Huwa ninapenda sana jinsi Kiranga anavyochangia kwani kama ni upanga atauita upanga na wala sio mundu

Hopngera GS nakutakia maisha mema bungeni na mungu akujaze busara zitakazowezesha kujenga hoja na kuwezesha kuwatete watanzania na nimatumaini yangu kuwa umeyachukua maoni ya kiranga ukayafanyia kazi kwani yanaweza kukusaidia na kujua unakiwa uweje

Hongera sana sana saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
wakuu,

dada yetu na mwanachama mwenzetu regia mtema kapitishwa kama mbunge kupitia fursa za viti maalum kwa tiketi ya chama chake (chadema). Nilisikitika ulivyopigana kupitia siasa za jukwaani na kuonekana kama ulichezewa rafu lakini mungu kakusimamia na kahakikisha lengo lako haligongi ukuta.

Kwa hili, bila kuangalia itikadi za kisiasa napenda kumpongeza na kumtakia kila la heri huko bungeni.

Aidha, list itatajwa muda si mrefu kupitia tbc1 kwa wanaoangalia taarifa ya habari ya saa 2 usiku.
hongera sana,regia. M
 
MSISITIZO:safari yetu ya Dodoma kumpongeza Bi Regia ipo pale pale
 
Ingawaje umepita kwa viti maalum kwenye hoja zako bungeni uwe una-target matatizo ya Jimbo la Kilombero ili iwe rahisi kwako kulishinda kwa urahisi mwaka 2015 maana wananchi watakuhesabu wewe kama ni mtetezi wao Bungeni!

Hongera sana da'Regina
 
Hongera Sana Regia Mtema, wewe ni Mpiganaji.

Hata hivyo, kama kuna evidence za kutosha kukata rufaa dhidi ya matokeo katika jimbo lake la Uchaguzi na akashinda, itakuwaje?

Uchaguzi utaitishwa na CHADEMA watamsimamisha mgombea mwingine, ni mawazo tu
 
Nami nichukue fursa hii kukupongeza Mh Regia na kila la kheri katika kazi zako, ukiwa na tatizo tuone tutashirikiana nawe !
 
Bibie Regia hongera sana na nakutakia kila la kheri isipokuwa nakuomba kazi moja tu ya ziada, Pamoja na wenzako - WAVUTE KINA DADA WENGINE WENGI CHADEMA, CCM inawapiga bao hapo..

Ushauri mzuri, kwa nyongeza zaidi wavute wale makini tu, wenye uchungu na nchi. Uwanja wa kuipigania nchi upo CHADEMA. Uwanja wa kupigania chama na ubinafsi tu upo CCM.
 
Hongera sana Regia! Mnapaswa kuweka bidii ya kufanya kazi ili miaka mitano ijayo msiwe wahanga wa kukataliwa na wapiga kura kama vile ccm ilivyokataliwa karibu nchi nzima. Nawatakia heri katika ujenzi wa Taifa la Tanzania! Tanzania tajiri hapo hapo MASIKINI SANA!
 
Kuna swali la kimsingi hapa..................na jibu lake ni kuwa............akishinda rufani yake basi yeye ataelekea kwenye chaguzi ndogo maana mahakama haina mamlaka ya kumtangaza mshndi ila kuyatengua matokeo endapo itaridhika taratibu zilikiukwa.................baada ya hapo ni kampeni na akishinda jimboni basi kiti maalumu Chadema itabidi iangalie kwenye ile orodha yake nani anafuata.................

Na ikitengua ni lazima wagombea wawe walewale? Mi nadhani ikiwa hivyo unaweza kumuachia mtu mwingine agombee kwa chama chako ukitaka, au...
 
Good stuff!

Hongera Regia na CHADEMA...
Nilikuwa nimepotea kidogo 7bu nilikuwa mbali sana na mtandao ila nimerudi na ninampongeza sana Dada Regina na Chadema kwa ujumla wake na pia na namuomba akawachakachue mafisadi.
 
Hongera dada Regia, sasa panga unalo litumie vizuri kupambana na akina Mteketa, ili wanakilombero watambue kuwa wewe ni zaidi ya Mteketa.
 
I love you sister Regia!
Natamani nipate no yako ya simu nikupigie ili niisikie sauti yako!
Kweli una watu wengi sana nyuma yako wanaokupenda, the evidence is here!
Mimi ninachokuombea ni kwamba UWEZE KU'DELIVER kule bingeni, kama ambavyo chama na wanachama walivyokuamini, na si tofauti na hivyo!
Mungu akubariki sana mpenzi!
 
Wakuu,

Dada yetu na mwanachama mwenzetu Regia Mtema kapitishwa kama mbunge kupitia fursa za viti maalum kwa tiketi ya chama chake (CHADEMA). Nilisikitika ulivyopigana kupitia siasa za jukwaani na kuonekana kama ulichezewa rafu lakini Mungu kakusimamia na kahakikisha lengo lako haligongi ukuta.

Kwa hili, bila kuangalia itikadi za kisiasa napenda kumpongeza na kumtakia kila la heri huko Bungeni.

Aidha, list itatajwa muda si mrefu kupitia TBC1 kwa wanaoangalia taarifa ya habari ya saa 2 usiku.

Congrats!!!!!!!! dada Regia, katumie vyema miaka mitano kutuonesha sisi tunaokuamini hatujakosea.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom