Hongera Regia, Mbunge kupitia viti maalum CHADEMA

Status
Not open for further replies.

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Wakuu,

Dada yetu na mwanachama mwenzetu (hapa JF) Regia Mtema kapitishwa kama mbunge kupitia fursa za viti maalum kwa tiketi ya chama chake (CHADEMA). Nilisikitika ulivyopigana kupitia siasa za jukwaani na kuonekana kama ulichezewa rafu lakini Mungu kakusimamia na kahakikisha lengo lako haligongi ukuta.

Kwa hili, bila kuangalia itikadi za kisiasa napenda kumpongeza na kumtakia kila la heri huko Bungeni.

Aidha, list itatajwa muda si mrefu kupitia TBC1 kwa wanaoangalia taarifa ya habari ya saa 2 usiku.
 
Hongera Sana Regia Mtema, wewe ni Mpiganaji.

Hata hivyo, kama kuna evidence za kutosha kukata rufaa dhidi ya matokeo katika jimbo lake la Uchaguzi na akashinda, itakuwaje?
 
Duh!

Hongera sana dada yetu, kwakweli ni faraja kubwa sana kwetu kujua hili. Kusema ukweli katika wengi wa CHADEMA ambao matokeo yao yalichakachuliwa, ya Regia yaliniuma zaidi. Mungu wetu ni mwema sana hatimaye amejibu maombi. Kaitumie vizuri miaka yako hii mitano bungeni katika kujiimarisha kisiasa jimboni kwako ili 2015 iwe mteremko kwako.

All the best dada Regia.
 
swafi saana mungu ameona udhalimu uliofanywa na nec na ccm wakadhani dada yetu hatatinga mjengoni, sasa ametinga.
 
Hongera Regia CHADEMA wamekuwa waadilifu kukuteua na bila shaka hili litapoza machungu uliyoyapata kwa kuchezewa mchezo mchafu na CCM
 
Now this is good news...

I believe si kwa jimbo lake tu but to the rest of the nation, Coz what we need is strong leaders with the example of Regia!

Nimefurahishwa mno na nakutakia kila la kheri katika kazi yako.

Ni jukumu kubwa lililopo mbele yako, but you are a very wise and hardworking person.

Mungu akutangulie kwa kila ulitendalo....
 
Safi sana dada,sasa kachape kazi hili 2015 ikifika ukajaribu tena Kilombero, nina uhakika miaka mitano ijayo nguvu za wezi za kura zitapungua zaidi.

Kila la kheri na Mungu akujaalie upate mafanikio kwenye yote unayopanga kufanyia taifa lako.
 
Hongera sana dada...usiwe mwoga kupambana na mafisadi bungeni,tuko nyuma yako!
All the best in ur new role!
 
Looking on the bright side I think this is a great consolation for our dear Regia.

Japo hakushinda jimboni mwake (iwe kihalali au la) katika nafasi yake hii mpya ya ubunge wa kuteuliwa nadhani ata kuwa na fursa ya kumwaga cheche zaidi.

Kwanza kwa sababu atakuwa hana jimbo haimlazimu kupigania maslahi ya watu wa jimbo moja tu bali ana weza aka pigania Watanzania wote bila kuonekana ana wasahau watu wa jimbo fulani.

Pili hii yaweza kuwa hatua moja kuelekea kwenye ubunge wa kuchaguliwa kupitia jimbo. Wabunge wa kuteuliwa kama hawa ndiyo tuna wahitaji. Watu ambao hawakutaka vya kupewa na wakaenda kupambana jukwani siyo wale wanaopiga siasa za chini chini ndani ya chama ili kupata ubunge wa kuteuliwa bila kutolea jasho.

Hongera Gender Sensitive aka dada Regia.
 
nami nakupa hongera sana, ombi moja tu kwako Regia usiende kuwa bubu, ukajenge hoja kama alivyokuwa mbunge wangu mteule IRONI LADY HALIMA MDEE na akina Anne Kilango wa CCM.
 
Namshukuru Mungu sana aliyefuta machozi yako na ya kwetu. Toka mwanzo ulistahili kuwa mjengoni. Changamoto ni kwako mwenyewe kutimiza damira yako kwa nchi yako. MIMI NAJUA UNAWEZA
 
Hongera sana dada. Bila shaka hii itafurahisha waliokupigia kura, ambao walikuwa tayari kuingia mitaani Ifakara kushangilia ushindi ako uliotangaza kwa makosa na ITV. Wawakilishe mjengoni, kwani wabunge walionufaika na wizi wa kura wanaogopa majimboni
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom