Hongera RC Makalla, hakika vibanda vya Machinga ulikuwa ni uchafu

Amos Makalla anaupiga mwingi haswa.......

Kitu kimoja wengi wasichokijua ni kuwa mh.Mkuu wa mkoa ana hulka ya "USIKIVU SANA"...KUJISHUSHA SANA....na UTEKELEZAJI MKUBWA na si "pang'ang'a"

Kongole kwake

Siempre JMT
"Pang'ang'a", hiki ni kimatumbi chetu au.....hapa umeniacha njani Jumbe.
 
Mabanda yameshaanza kurudi, leo nineshuhudia watu wanapigilia mabanda yao upya, kuna mengine bado yapo na uchafu au matakataka bado yapo tele tu, daah kweli uchafu ulijaa
 
Nawapongeza sana Mhe Rais Samia, hakika ameonyesha kujali maslahi ya Taifa kuliko mbwembwe za kisiasa. hapa nampa marks 100%.
pia Hongera sana Makalla kwa uongozi wako
Hii nchi iliharibiwa sana aisee kwa siasa za kitoto
 
Iringa ipi safi?
Kama usafi ndio huu,basi nahitaji akili mpya kujua uchafu ni nini!
Bodo mkoa flani unajiita mji kasoro bahari.!

Mji mchafu sijawahi kuona, hivi hawa wakuu wa miji huwa hawatembelei mikoa mingine mfano mkoa wa Iringa.
Mkoa wa Iringa ni msafi nahisi utakua umeupiga gep Moshi kwa sasa.
 
Lakini tukumbuke ktk shida ya ajira hao machinga ambao Leo mnafurahia kuwa wamefukuzwa mjini ni vijana graduates ambao wamekosa ajira hawajapenda kupanga vitu barabarani ila ni maisha ....mpango mzima wa hili swala sijaona ukizungumza ni jinsi watawasaidia Hawa machinga warudi ktk hali yao ya kawaida.....Sasa wanaugulia maumivu makali ya kiuchumi na tukumbuke wengine wanafamilia.....na hapo hapo wanasiasa wanazungumza watu wajiajiri .....nyinyi ambao mnafurahia mji kuwa msafi pengine mna ajira zenu maofisini lakn hamuangalii maumivu wanayopitia wenzenu ...jadirini ni kivipi serikari itapunguza tatizo la ajira...kwani magufuri alikuwa ajui kuwa mji ni mchafu alikuwa anajiuliza wanaenda wapi...mnafurahia lakn hamjui impact yake inaweza kuongeza ualifu.....

Haiwezekani ivunjwe sheria ya mji na jiji kue pachafu sababu ya ajira, ajira ni ajira itafutwe solution lakini haiwezekani ipindishwe sheriq sababu ya ajira
 
Naomba picha nione muonekano wa Rangitatu baada ya mavhinga kuondoka maana ilikuwa Ni burumai tupu (kama kweli wamachinga wamehama)
 
13 November 2021
Dar es Salaam, Tanzania

MUONEKANO MPYA MOROGORO ROAD TOKA UBUNGO MPAKA KIMARA

Ni baada ya jiji letu kufanikiwa kujinasua toka mtego wa Machinga kutopangwa, sasa kila raia wa jiji hili pamoja na machinga wanafaidi mpangilio wa maisha. Machinga wanakopeshwa mikopo, vifaa n.k wakiwa ktk maeneo rasmi yanayotambuliwa na pia raia wote kwa ujumla pamoja na machinga sasa wanafaidi kuendelea na shughuli zao bila bughudha.



Source : Godove Mgongolwa
 

12 November 2021​

DAR ES SALAAM RAPID TRANSIT (UDA-RT)-MWENDOKASI- MAGOMENI bus stop to UBUNGO bus Station


source : Godove Mgongolwa

Jiji letu la Dar es Salaam lazidi kupangika ili shughuli za kijamii na kiuchumi ziendelee vyema kwa ufanisi mkubwa bila kusahau usalama kwa mali za raia wote waishio ndani ya jiji hili kubwa Afrika Mashariki.
 
Mwendazake alikuwa nyoko sana kwenye baadhi ya mambo! Kwenye hili alitukosea heshima sana! Miji yote sasa hivi inapendeza sana, njoo ujionee Mwanza kulivyonoga! Mwanza Machinga tumewapanga vizuri, watuvumilie tu! Ujinga wa wanasiasa kutaka kura za bure watawaachia tena 2025 warudi kwenye maeneo yao, kazi kweli kweli!
 
18 November 2021

Mitaa ya Posta sehemu za Maktaba Street, Sokoine Drive jijini Dar es Salaam

Walking Downtown Dar es Salaam, Tanzania | East Africa (unedited content)



Source : James Chusi
 
Back
Top Bottom