mzalendoalltz
JF-Expert Member
- Mar 25, 2015
- 828
- 709
Pole na Shughuli wana JF
Kwanza napenda nijitambulishe kuwa mimi siegemei kwenye siasa bali uzalendo zaidi
Napenda tena kutoka moyoni kumpongeza Rais wangu kwa mambo mengi mazuri anayoyafanya, hataka kama kuna machache anakosea lakini kwa mwelekeo wa Rais Wangu, ana kauzalendo ndani yake, wanaomwita hafai yawezekana wameguswa na jinsi anavyo taka mambo ya wtz yawe. Nionavyo mimi huyu Rais wangu ana vision ambayo sisi wengine hatuioni, ijapokuwa tutaiona tu baadaye.
Nipende pia kumwambia Rais wangu kuna mambo mengi amekuwa akitaka tufanye sis watanzania ili taifa liendeleee na lililo kubwa ni mapato ya nchi ambayo yanakusanywa kwa njia nyingi sana,
mfano:
1.Wageni kuingia nchini kwa kulipa ada maalumu
2.Kodi/ushuru
3.Mapata kwenye vyanzo vya Asili
4.Adhabu mbalimbali tunazozifanya wale ambao hatufuati sheria n.k
leo nitaongelea hili la wageni kufanya kazi bila kibali na wanakwepa kulipa pato, na hayo mengine tutaendelea kuyaongelea siku zijazo.
Naomba niseme kwa masikitiko makubwa haya yafuatayo ambayo kwa kweli watu hawa Rais wangu akiwakamata awape adhabu kali sana na kama hakuna sheria basi atunge sheria kali sana hata ya kwafilisi wahujumu uchumi.
Na idara ya Uhamiaji
Sielewi ni kwa nini au hawajitambui, tunapoteza mapato mengi sana kupitia idara hii, kwa mfano kuna miradi mbalimbali inayoendelea hapa nchini, kuna biashara nyingi zinaendelea hapa chini n.k miradii hii inakuwa inaendeshwa na wageni na mara nyingi wageni hawa wanawaajiri wageni wenzao kutoka nje ya nchi, sijui sheria inasemaje ila ninahisi ni kuwa harusiwi kuajiriwa mgeni ambaye hana utaalam fulani katika eneo fulani la utaalamu huo. lakini cha kusikitisha miradi mingi hasa ya wachina wanaofanya kazi hawana utaalamu wowote, ni walinzi, wapishi, n.k wanaziba pengo la watanzania.
Lakini ninalotaka kusema ni kuwa wapo wachina na wengine wengi hatukatai kuwepo hapa nchini lakini wanatakiwa wapewe work-permit (kibali maalum cha kufanya kazi) na kinalipiwa kiasi fulani cha fedha kwa ajili ya kulijenga taifa letu, lakini utashangaa wanakuja kama watalii halafu wanafanya kazi zaidi ya miaka mitatu bila kulipa pato lolote kwa taifa, Rais wetu anajitahidi kuonge kila siku lakini watendaji ambao ni watanzania na ambao kila siku wanakuwa wakilalama kuwa mishahara ni midogo, wakati wanapoteza pato kubwa sana, mnafikiri Rais atapata wapi fedha kama nyinyi hamumsaidii?????? kazi mmekaa ofisini mnasuburi rais akafanye hizo kazi?????
ninavyoongea sasahivi kuna wageni wanaishi na kufanya kazi, biashara bila vibali aidha ni kwa uhamiaji kutokujua au wanatoa hongo.
tunaomba mtoke offisini tembeeni kwenye sehemu mbalimbali, tembeleeni miradi inyofanywa na wageni, mjue kama wanastahili na kama wanastahili je wanalipa pato kwa taifa?
na kama sio waondoweni haraka, nafasi hizo zifanywe na watanzania.
Wageni wengine mafano wachina, wahindi, wanakuja hapa halafu wanachukua wenzao kutoka china halafu wanawaficha kwenye majumba, wakimaliza kazi, ndani na kwa jinsi Uhamiaji wetu hawataki kutembelea miradi mbalimbali basi wageni hawa haramu wanazima ndoto za watanzania kupata kazi.
Ombi kwa Uhamiaji popote pale
Tunaomba Uhamijiaji Muanze kutembelea Miradi yote inayofanywa na Wachina kama sehemu ya kuanzia, fuatilieni mjue wanaishije hapa nchini? Je ni halili au sio halali na Je hata kama wana kibali je sheria inawaruhusu, tumuunge mkono Rais wetu ipo siku tutafurahia
Ombi kwa Rais wangu
Kwenye hizi ofisi za uhamiaji hakuaminiki, tunaomba uunde timu yako ifanye uchambuzi kwa kutembelea miradi inayofanywa na wachina ujue kama wanafanya kazi kihalali na kulingana na sheria. nionavyo mimi kuna wafanyakazi wanahujumu juhudi zako. Ni lazima tufanye kazi wote kwa lengo la kuinua nchi yetu.
Aksanteni najua nimewaboa lakini inauma sana..........