Hongera Rais Trump wa US na Rouhan wa Iran, Rais Magufuli anaweza kuiga mwenendo uliopita kwa hili

battawi

JF-Expert Member
Mar 29, 2014
2,030
2,000
Baada ya miaka kadhaa tangu Rais Trump wa Marekai kuingia madrakani,na kufuta mkataba wa maelewano wa US na Iran ulio sainiwa na Obama, sasa amekubali kuwa panaweza kuwepo mazungumzo na Iran na kuruhusu diplomasia ichukue mkondo wake.

Hii ni dalili nzuri sana ya kuondosha kiwingu cha vita vilivyo kwisha onesha dalili za kuibuka wakati wowote pale Ghuba ya Uajemi. Hii ndio busara na ndio akili inayoona mbali ,kuliko ile ya kusogeza manuwari na kukusanya silaha ,na kuvimbishiana misuli1566979189310.png


Hongera hizi pia nazituma kwa Raisi wa iran kwa kuonesha kwake utayari wa nchi yake juu ya mazungumzo ya kuondosha mivutano ambayo sehemu kubwa huziathiri familia za watu wa kawaida zaidi kuliko viongozi wa nchi wenyewe.Pia natowa kongolei kwa raisi wa Ufaransa Bw. Mcroni kwa ku 'mediate' suala hili kwa kutumia ushawishi wa EU kwa marekani,walipokutana kwenye mkutana wa G7 uliofanyika hivi karibuni ambapo walitumia fursa hiyo kumshawishi Raisi wa marekani

Sasa narudi hapa nyumbani Tanzania,ambapo Kuna chama Tawla na Kambi ya Upinzani Inayoonesha kuvunjwa nguvu kabisa na Raisi Aliyepo madarakani.Magufuli hajawahi hata mara moja kuwachukulia wapinzani kuwa ni wenzake katika siasa na angalau kuwaita ikulu kushauriana katika mambo ya msingi ya kitaifa, kama walivyofanya watangulizi wake.

Raisi Magufuli amepiga marufuku kabisa harakati za vyama vyote vya upinzani ,kiasi cha kwamba hata wakifanya mikutano yao ya ndani ,basi huvamiwa na polisi na kuzuiwa.Anataka dunia ijuwe kuwa Tanzania upinzani umekufa wakati anatumia Rungu la dola kuukandamiza usionekane.

Hakuna mikutano ya hadhara,hakuna ,Maandamano,hakuna kukutanisha vyama vya siasa na kuzungumza navyo yeye akiwa kama Raisi wa nchi na kutafuta Mustakbali wa siasa nchini,ni UADUI MBELE KWA MBELE.

Sasa nahisi ni wakati muwafaka kwa Raisi kuondosha vikwazo na KUKUTANA NA VYAMA VYA UPINZANI na kuwauliza ni namna ipi bora wangelipenda kuendesha siasa ,huku wakishauriana na kurudisha mahusiano mema na kukuza KUAMINIANA na UZALENDO .Tuondoe mivutano isiyokuwa ya lazima kama alivyo fanya TRUMP na ROUHANI au jirani zetu Keyata na Odinga kule Kenya.

Taifa hili ni letu sote,hakuna haja ya kuvutana kwa kitu ambacho ni urithi wetu kwa pamoja.
MUNGU IBARIKI TANZANIA,WABARIKI VIONGOZI WAKE,RJRSHA AMANI NA UMOJA MUNGU


1566979385606.png
 

mgaga1

New Member
Aug 16, 2019
3
20
Rais was Iran amesema hatokutana na Trump mpaka aondoe vikwazi dhidi ya nchi yake ya Iran
 

Perth

JF-Expert Member
Feb 10, 2014
3,063
2,000
Maandamano we ya nini au unataka ukauze maji ya kandoro na sigara kwa wingi?,watapewa ruhusa uchaguzi ukiwadia sio kila muda wawe na uhuru walizoea vibaya, kila kitu kina kanuni na taratibu zake omba kibali pewa fanya yalio ndani ya kibali chako ukikiuka unatiwa ndani,.
 

kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
25,954
2,000
Hakuna mikutano ya hadhara,hakuna ,Maandamano,hakuna kukutanisha vyama vya siasa na kuzungumza navyo yeye akiwa kama Raisi wa nchi na kutafuta Mustakbali wa siasa nchini,ni UADUI MBELE KWA MBELE.
1.Mikutano ya hadhara ipo,mbowe,msigwa,lema wanafanya tangazo la mwisho nimeona juzi kubenea nae anafanya wake manzese
2.Maandamano ya nini?hatuwezi kuwa nchi ya maandamano kila wakati
3.Rais wetu hawezi kuzungumza na watu wanaomwita dikteta
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom