Hongera Rais Samia uendelee hadi 2030

Mars 12

JF-Expert Member
Feb 25, 2021
221
349
Madam President kwa muda mfupi umetuonyesha kile ambacho mtangulizi wako Hayati Magufuli kilimshinda. Umekuwa unatumia busara, haki na ukweli.

Hata pale wananchi wanapolalamika hukurupuki,unapenda kusikiliza pande zote mbili.Huo ndio uadilifu wa uongozi. Tunaishi kwa wema na utulivu tofauti na mwanzo enzi za Magufuli. Kila mwananchi anafanya shughuli zake kwa kujiamini bila ya woga uliokuwepo.

Umesema ukweli kuhusu covid 19 na tunaanza kuona wananchi wakianza kuuchukulia kwa tahadhari zote zinazotolewa. Umeacha utaratibu wa kuwatumbua viongozi hadharani kwani nao ni binadamu wana familia,jamaa ila unachukua hatua kistaarabu na kuwachukulia hatua za kinidhamu.YAANI UMETURUDISHIA UTU NA HESHIMA ULIOPOTEZWA NA HAYATI JPM.

Unajua unachokifanya. Naamini binadamu hawana shukurani,ila Endelea na utaratibu wako kwani kuna methali isemayo tenda wema uende zako.

WEWE NI RAIS WA TANZANIA HADI 2030. MWENYEZI MUNGU AKUPE AFYA NJEMA NA AKUJAALIE MAISHA MAREFU.

AMEEN.
 
Rais ni mzuri ila CCM Ni mbaya Sana, inamfanya aonekane hajui alifanyalo, inamtukanisha. Mafuta yaendayo Zambia, yanapita kwenye bandari yetu, na yanapita kwenye ardhi yetu, tunawakamua Kodi..
Kama ni hivyo tafsiri yake ni dhaifu ndio maana wanamfanyia hivyo pia wala hana huo uzuri, hizi kodi yeye pia kakubaliana nazo na uliona jana kule morogoro akizitetea.

Unaingia mtego wa hao chawa.
 
Kama ni hivyo tafsiri yake ni dhaifu ndio maana wanamfanyia hivyo pia wala hana huo uzuri, hizi kodi yeye pia kakubaliana nazo na uliona jana kule morogoro akizitetea
unaingia mtego wa hao chawa.
Alikuwa hamtetei Samia, alikuwa akiitetea CCM. Mwema hatetetwi, ila mwovu hutafuta watetezi. CCM Chanzo Cha Matatizo
 
Alikuwa hamtetei Samia, alikuwa akiitetea CCM. Mwema hatetetwi, ila mwovu hutafuta watetezi. CCM Chanzo Cha Matatizo
Yeye sasa hivi ndio mwenyekiti, na CCM wote hufuata utashi na kauli ya mwenyekiti wao.

Umeona alivyokuja na issue ya corona, wote wakafata anachotaka na hio ndio CCM.

Hivyo hizo Kodi na tozo yeye ndio kaja nazo. Usishangae siki akitoka madarakani hawahawa mawaziri watashangaa ilikuaje walizipitisha
 
daa!!
We jamaaa andika tuu vizuri kwani unakimbilia waapi mzee!!?
 
Ili awe mzuri zaidi aanzishe mchakato wa katiba mpya ya nchi ataacha legacy nzuri ya kukumbukwa daima, aachane na uhafidhina wa chama chake.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom