Hongera Rais Samia Suluhu kukutana na Tundu Lissu. Watanzania hatutaki uadui unaosababishwa na wanasiasa wabinafsi wachache

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,951
12,535
Nimefurahishwa na taarifa rasmi iliyotolewa na serikali kupitia Afisa habari wa kurugenzi ya mawasiliano Ikulu Bi. Zuhura Yunus, kwamba Mh. Rais wa JMT, Bi. Samia Suluhu Hassan akiwa ktk ziara ya kiserikali nchini Ubelgiji amekutana na Mwanasheria, mwanaharakati, mwanasiasa machachari na makamu M/kiti Tanzania bara wa chama kikuu cha upinzani, CHADEMA ndugu Tundu Antipas Mughway Lissu.

Tundu Lissu yuko Ubelgiji nchi ya kigeni si kwa sababu ya kupenda bali kama mkimbizi wa kisiasa. Alikimbilia huko baada ya kutishiwa kuuwawa kwa mara ya pili na serikali ya Hayati Rais John P. Magufuli mara baada ya uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani Oktoba, 2020.

Katika uchaguzi mkuu huo, yeye alikuwa mgombea wa Urais kwa tiketi cha CHADEMA akichuana vikali na aliyekuwa mgombea wa CCM Hayati John P. Magufuli na mshindi wa uchaguzi huo na Tundu Lissu akishika nafasi ya pili.

Tundu Lissu ni mwanasiasa machachari kwa maana ya u - machachari kwelikweli. Ni mkosoaji mkubwa wa sera za serikali ya CCM tangu enzi za utawala wa awamu ya tatu chini ya Hayati Benjamin Mkapa, baadaye Jakaya Kikwete na kilele cha ukosoaji wake ikawa wakati wa utawala wa Hayati John P. Magufuli.

Wanasiasa wengi waliufyata wakati wa utawala wa awamu ya tano chini ya Hayati Rais John P. Magufuli ambaye ni kiongozi aliyesadifu tabia zote za kiongozi dikteta.

Tundu Lissu hakuwahi kumwogopa. Hakujali tabia ya udikteta wake. Alimkosoa waziwazi yeye binafsi na pia alikosoa sera, mipango na maamuzi mengi ya serikali aliyokuwa anaiongoza chini ya CCM.

Hayati Rais John P. Magufuli basically hakuwa kiongozi mvumilivu, hakupenda kukosolewa katika lolote analoamua. Kwa sababu za kisiasa, Tundu Lissu akawa adui namba moja wa Rais Magufuli na serikali yake na CCM.

Tundu Lissu akawa kero kwa Rais Magufuli, kero kwa serikali yake. Kwa sababu hizi wakatafuta kosa la kisheria kumfunga Tundu Lissu gerezani, wakakosa.

Wakajaribu kujibu hoja zake za ukosoaji dhidi ya Rais Magufuli na serikali yake zilizokuwa zinaibuliwa na huyu mtu, nako wakashindwa kuzipatia majibu sahihi ili kubalance shutuma zake ili umma umwone Tundu Lissu kama mtu mwongo na mzushi asiye mzalendo.

Bahati mbaya sana wakaja na mkakati mbaya, wa hovyo na wa kijinga wa kumuua tena kwa risasi za AK47 na SMG zaidi ya 35 huku 16 zikizama mwilini mchana kweupe katikati ya Jiji la Dodoma, Septemba 2017.

Kwa neema na rehema za Mungu mwenye enzi akazuia mauti ya kupangwa na wanadamu kumchukua mtu huyu. Tundu Lissu akaokokea ktk tundu la sindano kimiujiza na dunia nzima kushangaa.

Bahati mbaya sana, mtesi wake mkuu Rais John P. Magufuli mauti ikatangulia kumtwaa mwezi March, 2021 akamwacha aliyemdhania ni adui yake akiwa hai.

Makamu wake Bi. Samia Suluhu Hassan akatwaa kiti chake. Ndiye Rais wa JMT sasa.

Leo kafanya tukio kubwa sana na kukumbukwa. Kukutana na kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na aliyedhaniwa ni adui wa taifa hili huku ukweli ukiwa kinyume chake.

Hongera sana Rais Samia S. Hassan. You are great leader in deed kwa kuvuka mstari wa laana kwa nchi yetu.

Hopefully, mazungumzo yenu yatazaa Tanzania mpya kijamii na kimahusiano kuanzia kesho. Aidha tunawataka hao ndugu zetu wanaoishi uhamishoni ktk nchi za kigeni kwa sababu za kisiasa na kwa kutopenda warudi nyumbani tujenge nchi yetu pamoja.

Sisi wananchi kwa kweli hatutaki kugombanishwa na wanasiasa waroho wa madaraka wachache. Tunataka kuishi kwa AMANI na UPENDO bila kujali tofauti zetu za itikadi za kisiasa na kidini.

Asanteni usiku mwema wote.
 
Bandiko moja zuri sana ahsante mleta mada kwa uandishi mzuri ni mara chache sana kukutana na waandishi weledi kama wewe hapa jf, labda pascal mayalla lkn naye siku hizi nyuzi zake zinachosha heading peke yake unakuwa ulishajua kuwa huyu ni P
 
Haki Uhuru na demokrasia ni vitu muhimu kwa Tanzania kama havipo hivi Chadema itaendelea kuonekana wachochezi
 
... Glory be to our God; oh Lord thy name be glorified! None like you oh our creator; you are alfa and omega oh the God of Abraham, oh the God of Isaac, oh the God of Jacob.

Without you, oh Lord, where would we be today? We praise you, we worship you oh the God of gods. Amen.
 
Alishasema amewasamehe wote siku ile pale kanisani ikungi, hivyo lisu mtu wa Mungu na watu simtarajii afukue makaburi kama wengi wenu mnavyotamani (simlaumu mtu maana nature ya binadam ktk udhaifu wake mojawapo ni kutaka kulipa kisasi au kushuhudia kisasi kwa mbaya wake), lile tabasamu la brother lisu ni wazi mama amemwahidi 'supu' nzito ya kukandia maumivu na majeraha yake yote, ni suala la mda tu tutashuhudia ikiwekwa mezani, hii zama ni kama iliyotabiriwa na manabii wa kale juu ya nyakati za masiha kwamba "mito itatiririsha utamu, vilima vitatoa haki, nchi zitafunuka na kumzaa mkombozi, nyoka na chui watakula pamoja na mwanambuzi, mtoto atacheza panapo pango la nyoka Wala hatadhurika"
 
Back
Top Bottom