Hongera Rais Samia, Kwenda US, Kuhutubia UN, Safari ya Kuzindua Filamu Yako ya Royal Tour, Tunaomba Tukusindikize, Dreamliner Yetu Itue New York

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,178
Wanabodi,

Rais Wetu, Ndege Zetu.png

Kila nipatapo fursa, huwaletea mfufululizo wa makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" Makala ya leo ni bandiko la pongezi na ombi. Pongezi ni kwa Rais Samia, kusafiri kwa kukwea pipa la watu, kwenda nchini Marekani, na kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA. Ombi ni kwa Safari ijayo ya Rais Samia kwenda Marekani ni mwanzoni mwa mwaka ujao, kwenda kuzindua ile filamu yako, ya Royal Tour, tunakuomba safari hiyo, usipande ndege za watu, panda ndege yetu ya Dreamliner, tena tunaomba safari hiyo itangazwe kikamilifu kabla, ili Watanzania wenye uwezo, wakiwemo wasanii, wanamichezo, wafanyabiashara wakubwa na na sisi waandishi wa habari, tukusindikize kuitangaza Tanzania, na tangazo la Dreamliner yetu kutua pale JFK, jijini New York, Marekani ni tangazo tosha la utalii, kuvutia Wamarekani kutembelea Tanzania, kwa Tanzania kuonyeshea tuna direct flighs za US. Hongera sana, Mama Samia kwenda Marekani na kuhutubia UN.

Declaration of Interest
Humu jf kuna kikundi fulani kidogo, cha watu fulani wako kama wajingajinga fulani, kwenye issues serious za kujadili issues na idears wao wanaleta umbea wa kujadili watu, wako kama wetu wenye wivu wa kike, (Mama zangu,,dada zangu, wake zangu, binti zangu na wapenzi wangu, mnisamehe sana kwa neno wivu wa kike), ni kawaida kwa wanawake kuwa na wivu, ila kitu cha ajabu humu JF, hao wajinga wenye wivu wa kike humu JF, sio wanawake!, ukiandika chochote kizuri kuhusu serikali yetu, kama kuipongeza serikali au kiongozi yoyote wa serikali, wao wivu huwaka moto ndani yao , hivyo hununa, kuanza kubeza, au hata kutukana na badala ya kujadili mada iliyopp mezani, huleta viroja vya kumjadili mtoa mada kuwa ana njaa, na pongezi hizo, sio pongezi za kweli bali ni pongezi za kujikombakomba na kujipendekeza kusaka uteuzi!. Hawa ni wajinga. Naomba kama na wewe ni mmoja wa kundi hili, nakushauri bora uishie hapa, bandiko hili hatutaki umbea wa kumjadili mtu, wala wivu wa kike, kuumia mtu mwingine anapofanikiwa, anaposifiwa au kuongeza. Naomba ku declare interest openly, mimi Pasco Mayalla, huwa naandika kusifia vitu vya kweli tupu na vinavyostahili sifa, na pongezi, tena napongeza kwa dhati kwa maslahi ya taifa na sio kwa lengo la kusaka fursa za uteuzi wowote na kama kuna makosa, huwa nakosoa. Msifiaji msaka fursa au mtafuta uteuzi, kazi yake itakuwa ni kusifu tuu, kamwe hawezi kukosoa!. Mimi kwenye sifa nasifu na kwenye makosa nakosoa.

Kwa Vile JPM Hakuvuka Bahari, Kitendo Cha Rais Samia Kuvuka Bahari, Kuhutubia UN, Kinastahili Pongezi za Dhati.
Kwa vile kipindi chote cha JPM, hakuwahi kuvuka bahari, na rais wa Tanzania hakuwahi kuhutubia UN kwa miaka yote mitano ya JPM, kitendo cha Samia kuvuka bahari, kwenda nchini Marekani na kuhutubia UNGA, kinastahili pongezi za dhati. Hongera sana Rais Samia.

Rais Akisafiri Media Huwa Inaonyesha Akikwea na Akitua, Hii Safari ya UN Vipi?.
Kwa kawaida rais akisafiri, huwa tunaonyeshwa picha na video za eapoti, siku akiondoka huku akionekana akipanda ndege, na siku akirudi pia tunaonyeshwa akishuka kwenye ndege, na kuandaliwa press briefing ya rais pale eapoti kutujuza kilichojiri huko. Lakini safari hii ya Mama Samia kwenda UN, hatukuonyeshwa akipanda ndege, wala akishuka kupokelewa bali tumeelezwa tuu kuwa rais atakwenda Marekani, hatukuonyeshwa akiondoka, wala akipokelewa, tukaja kuonyeshwa tayari ameishafika Marekani akijichanganya na Watanzania, akiwemo Mtanzania mwenzetu maarufu sana aishie Marekani Da Mange ndio tukajua kumbe rais keshafika.

Hakuna chombo cha habari kinachojiuliza kwanini rais asafiri kimya kimya, apokelewe kimya kimya na kuibuka tuu tayari yupo Marekani. Kuna sababu gani ya rais wetu kusafiri bila kutumia ndege zetu, na badala yake rais wetu kasafiri kwa ndege za mashirika ya nje hivyo sio busara kumpiga picha rais wetu akikwea pipa la watu, wenyewe hawapendi na usumbufu kwa abiria wengine.

Kama Tanzania Tuna Ndege Zenye Uwezo wa Kufanya Direct Flights to US, Kwanini Rais Wetu Apande Commercial Flights?.
Enzi za Mkapa na JK, mimi nikiwa mwandishi wa habari wa kujitegemea, wakati wa safari za mbali za rais wetu, vyombo vya habari tulialikwa kumsindikiza rais wetu, na alikuwa anaandamana na kundi kubwa la wafanyabiashara. Enzi hizo pia rais wetu alipanda ndege za mashirika mengine kwasababu wakati huo, Tanzania tulikuwa hatuna ndege zenye uwezo huo.

Lakini kipindi cha JPM, Tanzania imejenga uwezo, sasa Tanzania tuna ndege kubwa za abiria za masafa marefu, kwanini rais wetu aendelee kusafiri na ndege za mashirika mengine, wakati sisi tunalo shirika letu, ATC, tunazo ndege za masafa marefu, Boeng na Airbus “The Dreamliner”?. Why?!. Hii ni aibu!. Ile siku sisi waandishi tulipopata fursa ya kumuuliza maswali JPM, pale Ikulu, nilipopata nafasi, kabla ya kuuliza swali, nilitoa hoja ya waandishi tushirikishwe kwenye mambo ya kuitangaza vizuri nchi yetu, na mimi nikasema waandishi tutajitegemea, kwa usafir chakula na malazi. Nimesafiri sana na Mkapa na JK, hivyo hii sasa ni zamu ya Samia, akisafiri safari za kimataifa, itolewe fursa kwa vyombo binafsi na wafanyabiashara kuandamana na rais.

Bila hata kusubiri majibu ya serikali au ya ATC, sababu pekee iliyomfanya rais Samia kusafiri kwenda Marekani kwa ndege za abiria za mashirika mengine, ni kwasababu kwanza ATC haina route ya Marekani, pili kupeleka mdege mkubwa, kama Dreamliner Marekani ni gharama, mafuta na landing charges ambazo zinalipwa kwa saa, hivyo huo mdege umpeleke rais Marekani, umsubiri kwa siku atakazokazokaa huko, na kumrudisha, ukilinganisha na kama akipanda ndege ya abiria kama wasafiri wengine, usafiri wa ndege za abiria ni nafuu kuliko kuipeleka Dreamliner Marekani.

Kutangaza Utalii Kimataifa ni Ghali, Hakuna Kitu Kinaongoza Kutangaza Utalii Kama Usafiri wa Ndege
Kama ilivyo katika kutangaza utalii, kuandaa filamu ya utalii na kuitangaza katika vyombo vya kimataifa, ni ghali, lakini kama tunataka kukuza utalii, hatuwezi kuepuka gharama, ndio maana tumekubali rais wetu kurekodi filamu ya Royal Tour kuutangaza utalii wetu. Hakuna kitu kinachoongoza kuvutia utalii, kama usafiri wa direct flights. Hakuna kitu kingeitangaza Tanzania nchini Marekani, kama ndege ya ATC kutua uwanja wa ndege wa New York, nchini Marekani huku imembeba rais wa Tanzania.

Rais wa Tanzani kwenda nchini yoyote ikiwemo Marekani kwa ndege ya watu wengine, wakati ATC inazo hizo ndege ni aibu, ni kosa, kosa sio kufanya kosa, kosa ni kurudia kosa, muda wowote mwakani, kuanzia miezi ya mwanzoni, rais Samia atakuwa na ziara rasmi ya kutembelea Marekani, ambapo katika ziara hiyo pia rais Samia ndio ataizindua rasmi ile filamu yake ya Royal Tour, naomba sana, tusifanye tena kosa la rais wetu kusafiri kwa ndege za watu, tusirudie kosa kwa rais wetu kutua Marekani kwa ndege za watu wakati sisi wenyewe tunazo hizo ndege na uwezo wa kulirusha li Dreamliner letu likiwa full board kwenda Marekani, tunao.

Kitu cha kufanyika ni kabla rais hajafanya ziara nchi yoyote, zille taasisi zote zinazohusika na shughuli mbalimbali ziarifiwe rasmi, ili ziandae trips. Mfano baada tuu ya kujua filamu ya Royal Tour inayo muonyesha movie Star wa Tanzania, Chief Hangai, itazinduliwa lini, nchini Marekani. Na tunajua Dreamliner inabeba abiria 300, ukiondoa rais na ujumbe wake wa kiserikali, say ni watu 30, kwanza serikali inatangaza fursa kwa taasisi zote za umma, wenye issues zozote za kufanya Marekani, wapange hizo issues zao zifanyike kipindi hicho. Waserikali hao, wafanye booking ATC. Then ATC inatangaza excursion trip ya Marekani kwa nafasi zote zilizobakia, hivyo trip ina correspond na siku za ziara ya rais kwenye nchi hiyo, lets say ni ziara inakayodumu siku 7. Inauza hizo nafasi zilizobakia kwa wafanyabiashara wa sekta binafsi, au Watanzania wengine wowote wenye uwezo, tukiwemo sisi waandishi wa habari.

Dreamliner Yetu ikitua JFK, Utaungaza Vizuri Utalii Wetu Kuliko Tangazo Jingine Lolote!.
Hivyo Taarifa tuu kuwa rais wa Tanzania, ametua Marekani na dege la Dreamliner la Tanzania, akiandamana na ujumbe wa watu 300!. Hili ni tangazo tosha la utalii kimataifa, kwasababu hakuna ndege yoyote ya direct kutoka Marekani hadi Tanzania, hivyo ATC pia itapata fursa ya kuanzisha route ya Marekani na nawahikishia ndege itajaa!.

Paskali
 
Mama Samia kaamua kufanya suprise, video ya kwanza ni selfie ya Dada Mange kule USA. Mama hakutaka publicity iambatane na safari yake tena ndefu.

Kuongoza hizi nchi za afrika ni kazi ngumu sana. Mama sasa anachimbwa ili watu wajiridhishe kama kaenda kaenda US na kundi la wafanyabiashara au la. Nongwa ni nyingi mno.

Kwenda US ni kelele kutokwenda kama JPM na kwenyewe ni kelele nyingi tu.
 
Mama Samia kaamua kufanya suprise, video ya kwanza ni selfie ya Dada Mange kule USA. Mama hakutaka publicity iambatane na safari yake tena ndefu.
Kuongoza hizi nchi za afrika ni kazi ngumu sana. Mama sasa anachimbwa ili watu wajiridhishe kama kaenda kaenda US na kundi la wafanyabiashara au la. Nongwa ni nyingi mno. Kwenda US ni kelele kutokwenda kama JPM na kwenyewe ni kelele nyingi tu.
Hakuna chochote hapo ni sawa na 0
 
Ukitaka unaweza kupeleka ndege zote za ATCL zikapark JF Kennedy airport, na usipate ongezeko lolote la watalii wala wawekezaji.

Rekebisha sheria za uwekezaji, punguza tozo za utalii, heshimu demokrasia, haki, utawala wa sheria, utapata watalii na wawekezaji wa kutosha, tena bila ya haja ya kupeleka ATCL. Lakini kwa hizi sera za kuwabambikia akina Mbowe, fungia vyombo vya habari, kupora uchaguzi, na utawala holela usiofuata sheria wa kusema Rais yupo juu ya sheria, hata tumvalishe manyanga Rais aweanacheza ngoma pale New York, ni kazi bure. Sana sana akina Paskali watapata threads za kuandika kuwa leo Rais wetu amecheza vizuri sana mdundiko pale New York.
 
Ukitaka unaweza kupeleka ndege zote za ATCL zikapark JF Kennedy airport, na usipate ongezeko lolote la watalii wala wawekezaji.

Rekebisha sheria za uwekezaji, punguza tozo za utalii, heshimu demokrasia, haki, utawala wa sheria, utapata watalii na wawekezaji wa kutosha, tena bila ya haja ya kupeleka ATCL. Lakini kwa hizi sera za kuwabambikia akina Mbowe, fungia vyombo vya habari, kupora uchaguzi, na utawala holela usiofuata sheria wa kusema Rais yupo juu ya sheria, hata tumvalishe manyanga Rais aweanacheza ngoma pale New York, ni kazi bure. Sana sana akina Paskali watapata threads za kuandika kuwa leo Rais wetu amecheza vizuri sana mdundiko pale New York.
Well said!👏🏽
 
Kwa taarifa yako Dreamliner lipo Marekani likimsubiri Chief H.

Kama Chief H. angepanda ndege ya abiria CCM wangesambaza hizo picha dunia nzima kumsifu kuwa mzalendo.

Wenzio wameondoka kimya kimya kuogopa maneno ya wadanganyika kuwa tozo zinatumika vibaya.
Hata mimi ndivyo nilivyomuelewa Pascal Mayalla . Hii ni hoja chokonozi ili apate taarifa maana kuna usiri mkubwa sana wa namna alivyosafiri. Sidhani kama anajipendekeza kama wengi wanavyofikiri.
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom