Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,226
- 26,047
Amani iwe nawe Mama yetu!
Kwa mfululizo nimekuwa nikiandika mada mbalimbali za kukushauri juu ya mustakabali wa uchumi wetu sisi Tanzania kama nchi.
Leo badala ya kukushauri, napenda sana kukupongeza kwa hatua ulizochukua dhidi ya Corona.
Moja ya sifa kuu za kiongozi mzuri ni kuwa anatakiwa awe mtu anayejali uhai wa watu wake na maisha yao kwa ujumla! Anatakiwa kuwa mtu anayetizama kuokoa kwanza uhai wa watu wake huku akizingatia kwa kiwango cha juu.
Kwa wana JF ambao hamjui, kwa sasa, Corona ndo imebeba hoja za uchumi wa dunia. Corona kama ilivyobeba hoja za uchumi wa dunia, kwa sasa ndo imekuwa muelekeo wa dunia kiuchumi. Anayefanya masikhara na Corona uchumi wa dunia unamuacha kweli. Anayecheza na Corona uchumi wa Dunia unamchezea kweli.
Corona pia imetikisa familia nyingi tu hapa Tanzania. Mimi pia ni mmoja ya watu ambao tumetikiswa baada ya ndugu zangu 3 kuugua Corona na ndugu zangu 2 kufariki kwa corona.
Kiuchumi pia Corona imetikisa Tanzania Kwa sababu watu wengi wanepoteza ajira hasa kwenye kampuni za utalii na pia kwenye sekta zilizokuwa zinategemea kufanya biashara na Ulaya na pamoja na America yakiwemo makampuni mbalimbali.
Hatua alizochukua Mama Samia huku zikitangazwa na Media kubwa Duniani kama BBC na CNN zina faida kubwa sana kwa Tanzania kiuchumi na siku si nyingi hali ya ugonjwa huu inapoenda kutulia au kudhibitiwa kwa hatua alizochukua Mama Samia zinaenda kuirudisha kwa kiwango kikubwa sana Tanzania kwenye uchumi wa dunia Yaani utalii na Biashara za kimataifa.
Hatua hizi pia zina faida Kwa kuwaondoa watanzania wengi waliokuwa kwenye hatari ya kuangamizwa na huu ugonjwa hasa wenye magonjwa yasioambukizwa kama kisukari kuwa salama Kwa sababu endapo watapata chanjo watakuwa salama na kuendelea na shughuli za uzalishaji.
Kwa nini nasema haya?
1. Dunia saivi imeanza kujadili jinsi ya watu kuruhusiwa kutembea nje ya nchi zao wakiwa na uthibitisho wa kupokea chanjo. Hili litafanya nchi kuwahimiza raia wao kutembelea maeneo ambayo wanajua hayana threat za corona ikiwemo maeneo ambayo wana chanjo. Hivyo sekta yetu kuu tunayoitegemea katika kutupatia fedha za kigeni haitoweza kurudi kwenye haki yake na nchi kuendelea kufaidika endapo tungeendelea kushupaza shingo na kudai kuwa hatutaki chanjo.
2. Tunakoelekea hata biashara baina ya nchi na nchi zitafanyika kwa kuzingatia protocols ambazo dunia inaenda kuziweka kutokana na Corona. Hivyo tukiwa nyuma, ni kweli tutakuwa nyuma kweli! Dunia itatuacha na Tanzania tutakufa kibudu.
Napenda kukupongeza Mama Samia kwa hatua ulizichukua za kuipa thamani sayansi huku tukimtanguliza Mungu mbele. Napenda kukupongeza pia kwa kufanya maamuzi ya akili na sio tu magumu kwa mustakabali wa usalama na maendeleo ya Tanzania na watanzania kiafya na kiuchumi.