MTANZANIA620
Member
- Jun 20, 2023
- 63
- 76
Nguvu ya maridhiano ya kisiasa katika uongozi wa nchi ni kubwa na inaleta mabadiliko chanya. Ina jukumu muhimu katika kukuza umoja wa kitaifa, kuleta utulivu wa kiutawala, kiusalama, kuwezesha na kutoa nafasi ya Nchi kufanya shughuli za maendeleo hata kufikia maendeleo endelevu.
Hii ndio sababu ya msingi iliyomsukuma Jemedari wetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kuja na falsafa ya 4R ambayo ndani yake kuna Maridhiano ya Kisiasa.
Faida za maridhiano ya kisiasa ni nyingi baadhi yake ni:-
1. Kukuza Umoja wa Kitaifa
Maridhiano ya kisiasa yanayaleta pamoja makundi yaliyokua yamegawanyika kisiasa, kikabila, kidini, kiuchumi nk
Hali ambayo inakuza maono ya pamoja kama taifa, kuimarisha umoja wa kitaifa na kuchagiza maendeleo ya pamoja.
2. Kuzuia na Kutatua Migogoro
Maridhiano ya kisiasa husaidia kushughulikia malalamiko na dhuluma za kihistoria ambazo mara nyingi husababisha machafuko.
Kwa njia ya mazungumzo na maelewano, maridhiano ya kisiasa yanasuluhisha mizozo bila kutumia vurugu, kuhakikisha amani na usalama vinaendelea kudumishwa.
3. Kuimarisha Taasisi za Kidemokrasia
Maridhiano ya kisiasa hutanguliza ushirikishwaji na maelewano hivyo kuimarisha taasisi za kidemokrasia na kufanya utawala/uongozi wa Nchi kuwa shirikishi na wenye uwakilishi zaidi.
Maridhiano haya yanahakikisha sauti zote, ikiwa ni pamoja na makundi yaliyotengwa, yanasikika na kuheshimiwa.
4. Kuimarisha Uimara wa Kiuchumi
Maridhiano ya kisiasa hupunguza hali ya taharuki na kukosekana kwa utulivu wa kisiasa katika Nchi hali ambayo hupelekea wawekezaji na wafanyabiashara kukimbiza mitaji yao na kuogopa kuwekeza au kuendelea na biashara katika hali ya mizozo na migogoro hivyo kudhoofisha uchumi wa Nchi.
Maridhiano yanawezesha serikali kuwa na utulivu wa kisiasa, kuzingatia utungaji sera na kufanya maendeleo badala ya kutumia muda mwingi kudhibiti mizozo na migogoro.
5. Kujenga Imani Miongoni mwa Wananchi
Maridhiano ya kisiasa yanajenga na kukuza uaminifu kati ya wananchi na serikali/viongozi wao, na hivyo kuimarisha imani na kujenga uhalali wa kisiasa katika haki na uendeshaji wa serikali.
6. Kuwezesha Haki ya Mpito
Katika mazingira ya baada ya migogoro na mizozo ya kisiasa, mara nyingi maridhiano ya kisiasa huambatana na taratibu kama vile kuundwa kwa kamati toka pande zote, fidia, na mageuzi ya kitaasisi ili kuponya majeraha ya jamii.
Matokeo ya mchakato huo huwezesha jamii kusonga mbele bila vikwazo, hisia mbaya itokanayo na dhuluma za zamani.
Tumeshuhudia wafungwa wa kisiasa wakiachiwa huru, vyama kuanza kupokea ruzuku, mikutano ya kisiasa ikirejeshwa na maandamano yakiruhusiwa.
7. Heshima na ushirikiano kimataifa
Maridhiano ya kisiasa huipa Nchi/serikali/viongozi heshima kimataifa hivyo kuungwa mkono na jumuiya ya kimataifa kwa kuendelea kunufaika na misaada ya kifedha, ushirikiano na mahusiano imara kidiplomasia.
Changamoto ya Mchakato wa Maridhiano ya kisiasa
Maridhiano ya kisiasa yanaweza kuwa ni mchakato mrefu na mgumu, unaohitaji ujasiri, utulivu wa kiuongozi, ustahimilivu, ukomavu kiuongozi na kujitolea kwa dhati kutoka kwa washikadau wote.
Yanaweza kukwamishwa na kutoaminiana kwa kina, masilahi yasiyobadilika na ukosefu wa nia njema kisiasa. Hata hivyo changamoto hizi hayafungi milango ya kufufua na kuendeleza mchakato huu mwema kwa ustawi wa Nchi na wananchi wake.
Hitimisho
Maridhiano ya kisiasa si tu ni kitendo cha kiungwana na maelewano bali ni nyenzo ya kimkakati ya kujenga amani, utulivu na maendeleo ya kudumu. Viongozi imara na wenye ufanisi mithili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan utumia nguvu ya maridhiano kubadilisha mataifa yao, wakionesha nguvu inayotokana na umoja na kuheshimiana miongoni mwao.