Hongera Rais Samia kwa kuishi maneno yako

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,592
29,721
Nampongeza kwa dhati Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuamua kuiweka Tanzania upya kwenye ramani ya nchi zinazosimamia na kulinda Utu.

Tangu ameingia madarakani siku 109 zilizopita amekuwa akikemea kwa wazi matendo ya aibu yanayofanywa na mamlaka za nchi hususani polisi na ofisi ya DPP bila kuwasahau TRA na TAKUKURU kwa kuwaasa kuacha kubambikiza watu kesi na kuondoa mahakamani kesi zote zilizoundwa kwa kigezo cha kisiasa na kiuonevu.

Masheikh wa Uamsho ambao walisota ndani tangu enzi za Kikwete wamefutiwa kesi kwani inaonekana walishtakiwa kama kutolewa kafara kwa matukio ya kipuuzi yaliyotokea Zanzibar.

Mtaani kwetu kuna wananchi wawili ambao walikuwa mahabusu dhidi ya kesi za uhujumu uchumi nao wametoka na kufutiwa kesi zao za kubumba.

Leo tunaona Mahakama ikimfutia mashtaka Mdude Nyagali kesi ya kubambika ya madawa ya kulevya na utakatishaji.

Naamini mengi mazuri yanakuja na Watanzania tuungane kujenga nchi yetu.

Pia nikiwa kama MwanaCCM ndakindaki ninawaomba radhi wote niliowahi kuwakwaza humu kupitia hoja na misimamo yangu kisiasa.

Nimegundua kwamba, chama changu cha CCM kiliamua kuunda propaganda za kutusadikisha waumini wake kwamba kipo mstari sahihi.

Naunga mkono mashtaka dhidi ya yule DC wa Hai na ikiwezekana kwa wengine iwe funzo kwa viongozi wengine kuheshimu dhamana walizopewa.

Tuungane kumpongeza mama Samia Suluhu Hassan
 
Mafanikio ya Samia ni habari mbaya sana kwa Lisu maana 2025 hana chake tena.

Ccm itaendelea kupeta.

Bavicha wote wanashangilia ccm sasa hivi
 
Yote hayo hayasaidii chochote kama hatujapata Katiba mpya itakayolinda haki zetu. Leo yupo Mama Samia kaliona hilo, jee Kesho akitotokea mwengine kama mendazake sio tutarudi kule kule au nazaidi?
 
Bado mbona hujakubali kuwa tulikua na dikteta umeongelea propaganda tu?
Ni mtoto mdogo pekee ukimtajia mkate lazima uhakiki alphabeti zake.

Kama hukuliona hilo basi haujakomaa kisiasa
 
I love the commitment, dedication and humility of our president. She walks her talks.

She has managed to heal the nation that was horribly shattered by her predecessor in just 100 days. Bravo madam SSH!!!!

We expect many more good things from her e.g new constitution
Hataki kuwa mnafiki
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom