Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,489
- 40,999
Leo vyombo mbalimbali vya kimataifa vimetoa uzito wa hali ya juu kutekwa kwa Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA, na kukamatwa na wasaidizi wake.
DW - Chadema yawaamuru wafuasi wake kumsaka Mbowe
Aljazeera - Tanzania’s Chadema party says leader Freeman Mbowe arrested
BBC - Chadema kwenda mahakamani kesho iwapo Freeman Mbowe hataachiliwa
VoA - Tanzania's Main Opposition Leader Freeman Mbowe Arrested
Africannews - Tanzanian opposition party says leader Freeman Mbowe, 10 others arrested | Africanews
AFP - Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Freeman Mbowe akamatwa
Si mara ya kwanza kwa viongozi wa upinzani, na hasa CHADEMA kutendewa unyama na Serikali ya CCM. Lakini matukio hayo mengi hayakupewa coverage kubwa kama hili tukio, ukiondoa lile la Tundu Lisu kushambuliwa kwa risasi 38, na 16 zikiingia mwilini mwake.
Wengi wanajiuliza, ni kwa nini?
Vyombo hivi vimetoa uzito wa hali ya juu, hasa kwa nia ya kuonesha undumilakuwili wa Rais Samia. Maana ni hivi karibuni, yeye mwenyewe kwa kauli yake, aliihakikishia jamii ya kimataifa kuwa ataheshimu misingi ya demokradia, utawala unaoheshima sheria na haki za raia. Hata kabla ya mwezi kupita, tunashuhudia matukio ya kidikteta yasiyoheshimu katiba, sheria na mikataba ya kimataifa ya kuheshimu haki za watu.
Mashaka yale ambayo Jumuia ya Kimataifa ilikuwa nayo juu ya utawala wa Serikali ya CCM, chini ya Rais Samia, sasa yanapata majawabu yasiyo na shaka.
Mtangulizi wake alikuwa na bahati. Aliingia madarakani wakati Jumuiya ya kimataifa ikiamini Tanzania inafuata misingi ya kidemokrasia kwa kiasi fulani. Taratibu, watawala wakaanza kuipa mashaka jamii ya kimataifa, na baadaye Jamii ya kimataifa ikatambua kuwa Tanzania inaongozwa kwa misingi ya kidikteta, na walichukua hatua kadhaa ikiwemo kutoa kauli kali dhidi ya utawala uliokuwepo, kupunguza na kufuta misaada mingi ambayo Tanzania ilikuwa ikiipokea.
Rais Samia, amechukua uongozi, nchi ikiwa katika udikteta, na jamii ya kimataifa ikimwangalia kwa ukaribu kama ana dhamira ya kubadilisha utawala wa nchi kutoka kwenye udikteta na kuifanya nchi iongozwe kwa ustaarabu wa Dunia. Naye akachombeza kuwa amedhamiria kufuata misingi ya haki na demokrasia. Kabla ya due diligence kukamilika, matukio ya kuthibitisha kuwa anachotamka na anachotenda ni tofauti, yanaendelea kutokea.
Gharama za kubadilika na kuwathibitishia wanadamu wastaarabu, hata wamwakini, zitakuwa kubwa zaidi sasa kuliko hapoalipoingia. CHADEMA walichofanya ni kuithibitishia Dunia kuwa Rais Samia, anaihadaa.
Kuongoza nchi kunahitaji upeo mkubwa na mpana, lakini pia inastahili kuzungukwa na wasaidizi wanaoweza kuiona kesho kabla ya kufika kesho, sio ambao uwezo wao wa kuona mambo unaishia mita moja.