Hongera Rais Samia, kitendawili cha uhamisho wa watumishi chateguliwa na Katibu Mkuu Tamisemi, Prof. Riziki Shemdoe

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
Prof. Shemdoe atengua kitendawili cha uhamisho

Nteghenjw Hosseah, OR-TAMISEMI

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Prof. Riziki Shemdoe amesema uhamisho wa watumishi wa Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa utafanyika mara nne kwa mwaka yaani kila robo ya mwaka husika.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Prof. Shemdoe amesema kila tarehe 10 ya mwezi unaofuata baada ya robo mwaka kwisha uhamisho utafanyika na majina yatawekwa kwenye tovuti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI.

“Robo kwanza ya mwaka yaan Julai - Septemba majina ya uhamisho yatakua yanatoka tarehe 10 October , na robo ya Pili Oktoba - Desemba majina ya uhamisho yatatoka Januari 10."

Aliongeza kuwa: " katika robo ya tatu ya Januari- Machi majina ya uhamisho yatatoka April 10 na robo ya mwisho ya Aprili-Juni majina ya uhamisho yatatoka Julai 10."

Aidha Prof.Shemdoe alibainisha kuwa majina ya watumishi wote watakaohamishwa yatawekwa kwenye Tovuti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI ambayo ni www.tamisemi.go.tz.

Pia amewataka Makatibu Tawala wa Mikoa yote nchini kuwasilisha orodha ya watumishi wa kuhama ofisi ya Rais-TAMISEMI kila tarehe 05 ya mwezi unaofuata baada ya robo mwaka.

Aidha, aliwataka Makatibu Tawala wote kutokupitisha maombi ya watumishi wanaotaka kuhamia kwenye majiji, manispaa na miji kwa kuwa maeneo hayo yana idadi kubwa ya watumishi.

Aidha, Profesa Shemdoe aliwataka Makatibu Tawala kuwapa kipaumbele watumishi wenye changamoto mbalimbali zilizothibitishwa.

Pia aliwataka watumishi wote kubaki kwenye vituo vyao na barua za uhamisho zitatumwa kwa waajiri wao na wataona majina yao kwenye Tovuti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Pia aliwataka watumishi kujihadhari na matapeli wanaotaka fedha kwa ajili ya kufanikisha uhamisho wao kwa kuwa Uhamisho ni bure na ni haki ya kila mtumishi.

Alisema kuwa Barua za Uhamisho za kipindi cha nyuma ambazo zilishafika Ofisi ya Rasi TAMISEMI zinashughulikiwa na majina yatatolewa kila mwezi mpaka Juni 30 kabla utaratibu mpya haujaanza kutumika.

NB: Leo yametoka majina 225 ya uhamisho kwa kipindi cha kuanzia April 1-30, 2021
Screenshot_20210506-191845.png


Ili kuona majina hayo, tembelea tovuti ya tamisemi.
 
Hii itaadhiri shule za vijijini
Serikali ianzishe posho ya walimu, walimu wakuu, maafisa elimu kata na Maafisa elimu wanaofisi kwenye mazingira magumu
 
Back
Top Bottom