Hongera Rais mstaafu Benjamin Mkapa

mmbangaya

JF-Expert Member
Jan 16, 2015
997
1,763
Habari Jf!

Binadamu anayefanikiwa kwenye maisha ni yule ambaye haogopi kufanya jambo lolote bila kujali kama anaweza kupata hasara. Wachumi wanawaita risk takers.

Kipindi kampeni za urais zilipokuwa zinaendelea mzee mkapa alikuwa anatumia lugha kali mpaka nikawa nikimsikiliza naogopa. Alikuwa anatumia lugha kali bila kujali nani atakuwa rais ajae wa JMT.

Ila sasa nimepata somo kwamba huyu mzee mkapa alikuwa risk taker and now biashara imemlipa.

Hongera sana kwa kufanikiwa katika hili.
 
Una haki ya kumpongeza Na hapa duniani atasifiwa sana ila Mbinguni hakika Mungu huukata mkono Wa mwovu Maisha ni duniani Na Mbinguni
 
Mzee alijitoa sana jamani. Hongera nyingi ziende kwake. Anastahili pongezi tele.
 
Katika siasa za Tanzania. Mkapa ni wa uzani ya juu - heavyweight. Ni mtu asiyetaka ujinga. Ni raha sana kuwa na mtu wa aina hii katika nchi yetu. Si kwamba wengine hawafai, bali kila mmoja ana faida zake kwa wakati wake. Katika uchaguzi uliopita kuanzia chamani hadi taifa Mkapa kafanya kazi nzuri. Namwomba Mkapa aandike kitabu kuhusu siasa ndani ya chama, vyama vya upinzani na taifa kwa ujumla. Hongera Mkapa, najivunia uwepo wako. MUNGU akujalie afya njema na maisha marefu.
 
Alikuwa anatetea mali alizopora pamoja na mkewe

Tunasubiri kuona hatua atakazochukua Magufuli.
 
Habari Jf!

...

Ila sasa nimepata somo kwamba huyu mzee mkapa alikuwa risk taker and now biashara imemlipa.

Hongera sana kwa kufanikiwa katika hili.

Nakubaliana nawe. Alianzisha ANBEN akiwa ikulu na 'akajiuzia' KIWIRA akiwa rais. Bahati mbaya hazikulipa sana. Ila ndo upambanaji huo!!
 
Katika siasa za Tanzania. Mkapa ni wa uzani ya juu - heavyweight. Ni mtu asiyetaka ujinga. Ni raha sana kuwa na mtu wa aina hii katika nchi yetu. Si kwamba wengine hawafai, bali kila mmoja ana faida zake kwa wakati wake. Katika uchaguzi uliopita kuanzia chamani hadi taifa Mkapa kafanya kazi nzuri. Namwomba Mkapa aandike kitabu kuhusu siasa ndani ya chama, vyama vya upinzani na taifa kwa ujumla. Hongera Mkapa, najivunia uwepo wako. MUNGU akujalie afya njema na maisha marefu.

NILIMPENDA SANA hadi niliposikia pahala kawapa wasouth lease ya miaka mia ya kiwira....
 
Back
Top Bottom