SHERRIF ARPAIO
JF-Expert Member
- Aug 25, 2010
- 9,539
- 5,903
Umeongea point nzuri ila kwa utawala huu wa sasa naomba usahau tu hii issue ya political tolerance/agreeing to disagree.Wanabodi,
Kama kawaida yangu, kila nipatapo nafasi huwaletea makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", ambazo pia huchapishwa kwenye magazeti mbalimbali ya ndani nchini Tanzania.
Makala ya leo, ni kumpongeza na kumshukuru Rais Magufuli kwa kufundisha somo la "Managing Diversity" kwa wateule wake, lakini Tanzania tunapoelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na madiwani, bado tunakabiliwa na tatizo kubwa la kutokuwepo kwa "Political Tolerance" linazosababisha "Political Hostilities" kuanzia kwenye mihili ya Mahakama, Bungeni, na Serikalini, kuanzia ngazi ya taifa, mikoani, wilayani, majimboni, kwenye kata hadi mitaani ambapo kuna chama kimoja, CCM kilichosika dola, kinahesabiwa kama chama dola na kustahili haki zote, huku vyama vingine vyote vikibaguliwa na kuhesabika kama maadui visivyo stahili!.
Tatizo hili linaweza kumalizwa kwa somo la "Managing Political Diversity" ambalo rais Magufuli ameisha lianza kwa kuwakaribisha wapinzani kwenye shughuli la kitaifa na kuwaalika baadhi ya viongozi wa baadhi ya vyama vikuu vya upinzani Ikulu, lakini kuelekea kwenye uchaguzi, somo la "Political Tolerance" bado linahitajika sana wakati huu kuliko wakati mwingine wowote, hivyo kunahitajika kuendeshwa kwa somo la "Managing The Political Diversity" ya hali ya juu kwa viongozi wa pande zote, serikali, CCM, na vyama vya upinzania, ili tuweze kuendesha uchaguzi Mkuu ujao, uwe ni uchaguzi huru na wa haki kupitia uwanja ulio sawa, "level playing field!". Hili likifanyika, Rais Magufuli atabarikiwa sana, nchi yetu itabarikiwa sana kwa kupata amani, utulivu, na ustawi, utakaoleta maendeleo makubwa sana ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Kwa faida ya wenzetu wenye uwezo mdogo kusoma nyuzi ndefu, tunaweza kuishia hapa, na kusoma hitimisho
Hili la rais Magufuli na serikali yake kukubali Tanzania ni nchi ya vyama vingi na kuwatendea haki vyama vyote kwenye uchaguzi Mkuu huru, kutapelekea rais Magufuli kubarikiwa, serikali yake kubarikiwa, chama chake CCM kubarikiwa na nchi ya Tanzania kubarikiwa, na hata kama uchaguzi Mkuu ujao utairudisha Tanzania kuwa ni nchi ya chama kimoja, kurudi huko kutakuwa ni kutimiza matakwa ya Watanzania na kutakuwa kumefanyika kupitia uchaguzi Mkuu huru na wa haki na hivyo kuhesabiwa ndio the wishes of the people, hivyo naomba kuusisitiza huu wito wa uchaguzi mkuu kuendeshawa kwa mtindo huu
Ombi Maalum, Uchanguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2020, Uendeshwe Kwa Ceteris Peribus, Sio Kwa Mutatis Mutandis!. Tutabarikiwa!
Mungu Mbariki Rais Wetu Magufuli Aweze kufikisha somo la Managing Political Diversity kwa serikali yake ili tuwe na "Political Tolerance" kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, uwe ni uchaguzi huru na wa haki na kuendeshwa katika uwanja ulio sawa.
Mungu Ibariki Tanzania.
Jumatatu Njema
Paskali
Political tolerance kwa Africa naona iko nchi tatu tu. (S. Africa, Kenya na Malawi)