Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,319
- 72,747
Watu wamekusifu kuwa kule Bukoba umesema bila kuremba na kile unachokiamini. Hii ni style yako kila mahali, hukwepeshi kabisa. Hutajenga nyumba za waathirika hata kwa wale wasio na uwezo kabisa kwani sio kazi ya serikali (kwani sio Building contractor). Hupeleki chakula mahali penye njaa kama mvua ilinyesha na hawakulima, kwani serikali haina shamba.
Sio Bukoba tuu, bali kila mahali ulipo pata nafasi ya kuzungumza umeyazungumza hayo na kuwa kila mtu afanye kazi ili kujiletea maendeleo na kuwa msema kweli mpenzi wa Mungu. Safi sana.
Natumaini kuwa Chama chako kitakupendekeza (hata kama hakitakutaka) kugombea 2020 nafasi hiyo tena, tunakuomba wakati wa kampeni uwe hivyohivyo msema kweli mpenzi wa Mungu. Waambie hutatoa chakula kwenye njaa, au tetemeko,kimbunga na mafuriko yakitokea watajijua kwani hayo hayaletwi na CCM.
Usiseme tena kama kule Tabora kuwa wanafunzi wakipata sifa ya kuingia chuo wakikosa mikopo Bodi nzima haina kazi, bali uwaeleze wazazi kuwa kama mwanao hajafaulu daraja 1&2 tena sayansi utamlipia mwenyewe kama huwezi "wafwa". Ndio ni mtindo wa kusema Ukweli ili kuwa mpenzi wa Mungu.
Wananchi wameonyesha kukupenda sana kama tulivyo ona kule Bukoba jana, kwanini lakini? Ni kwa sababu unasimamia ukweli, na msema kweli mpenzi wa Mungu.
2015 Lubuva alikupa 52% ya ushindi kama sikosei, lakini baada ya kujua ukweli ulivyo na kwa vile Utawaambia ukweli Watanzania wakati wa kampeni 2020 basi nahakika hata bila "Lubava" lazima utazoa zaidi ya 95%