Hongera Rais Magufuli kwa kumaliza utata wa malori Rusumo. Sasa tuhamie Mutukula na mipaka ya Kenya, Malawi na Zambia

Mtini

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
1,486
2,332
Napongeza hili kwa sababu kuu tatu:

1. Baadhi ya watanzania wanaodhani wao wanaishi sayari ya Mars, dua zao na maombi yao wanatamani kuona Rwanda inahamia bandari ya Mombasa na Zambia na Congo wanahamia Beira . Walikuwa na uhakika wa asilimia 100 kuwa kwa janga hili jamaa watajikata kumbe they are here to stay.

2. Rwanda walisimika kuwa lazima malori ya Tanzania yapokelewe na Malori ya Rwanda, hii ina maana kuwa biashara ya Malori ingekuwa ngumu kwa kuongeza gharama kwa kuwa mwenye gari angelazimika kuajiri na dereva wa kinyarwanda ambae angepokea gari mpakani kwa kuwa si kitu rahisi kumkabithi gari dereva usiyemjua.

3. Rwanda walisimika kuwa magari yatakayovuka lazima yawe na escort kwa gharama za mwenye gari.

rwanda.jpg
 
Rais Magufuli nahodha bora

Dunia itamwomba radhi
Sasa hapo kilichobadilika ni Nini? before wenye corona walikuwa wanazuiwa boda sasa ukikutwa na corona unabaki Dar hata mpakani hufiki.kwa maneno mengine Ni kwamba anayehudumia ameufyata kwa anatehudumiwa.Hizi njaa za serikali yetu zinatia aibu sana
 
Hivi wewe nongwa kwa Tanzania huwa inakupa midadi ya nini? Unaonekana wewe ni mchawi
Mkuu sasa hapo Kuna nongwa gani.Kwanza serikali yetu imesema itachukua jukumu la kuwapima hapa Dar na kwenye vituo kadhaa vya njiani.Pili mizigo yote itashushwa mpakani na kwa wale wa mafuta and perishables basi wataingia Rwanda chini ya ulinzi mkali maana yake wasije wakajichanganya na wanyarwanda.Yaani hadi sasa RWA 5 TZ 0
 
Hao ni Rwanda wamechukua hatua kiazi wewe. Mnashushia mzigo mpakani nyi mnarudi zenu na macorona mliyobeba. Kwa watu wa malori ya mafuta ni kujiweka isolation. Wewe unaona wapi unafuu hapo? Rais wako simu imezima chaji haipatikani!
wewe jamaa unakaribia kuwehuka kisa chuki.yaani hapo unatamani rais wa rwanda achukue maamuzi yako lakini ni vile haiwezekani.

jamani huyu magu mpokeeni tu,atawaua kwa vihoro kukesha mkisubiri aanguke.vipi bungeni madereva hawajaingia
 
Mkuu sasa hapo Kuna nongwa gani.Kwanza serikali yetu imesema itachukua jukumu la kuwapima hapa Dar na kwenye vituo kadhaa vya njiani.Pili mizigo yote itashushwa mpakani na kwa wale wa mafuta and perishables basi wataingia Rwanda chini ya ulinzi mkali maana yake wasije wakajichanganya na wanyarwanda.Yaani hadi sasa RWA 5 TZ 0
Comments zake against tanzania always, huyo malisa
 
Hao ni Rwanda wamechukua hatua kiazi wewe. Mnashushia mzigo mpakani nyi mnarudi zenu na macorona mliyobeba. Kwa watu wa malori ya mafuta ni kujiweka isolation. Wewe unaona wapi unafuu hapo? Rais wako simu imezima chaji haipatikani!
Makubaliano haya yako vizuri sababu mizigo yao wabebe mpakani maana yake Nini Ni gharama zaidi Kwao na pia ya Kwao inayokuja bandari ya Dar es salaam waishushe mpakani sisi tukaichukue mpakani tuifikishe bandari ya dar es salaam kwa gharama zao sababu Ni ya kwao sio yetu malori yetu yalikuwa yakipeleka mizigo Rwanda yanarudi matupu kwa kukosa mizigo ya kurudi nayo yakishashusha lakini Sasa yatapeleka mizigo ya rwanda mpakani na yatabeba mizigo ya Rwanda kurudi nayo bandari ya dar es salaam Ni uamuzi mzuri hongera kwa serikali

Malori ya mafuta yameruhusiwa watanzania wengi wanamiliki vituo vya mafuta Rwanda uamuzi mzuri pia

Kuhusu perishable goods pia uamuzi mzuri sababu bakhresa anapeleka kuuza vyakula Sana Rwanda Ni mfanyabiadhara mkubwa kule pamoja na akina Azania Millers Ni uamuzi mzuri una faida kwetu Sana

Haya makubaliano nayaunga mkono yako vizuri na maslahi ya Tanzania yamezingatiwa barabara

Wewe li chadema Huna ulijualo zaidi ya lockdown kujifungia Kama mwali

Chadema akili zenu finyu mno
 
Makubaliano haya yako vizuri sababu mizigo yao wabebe mpakani maana yake Nini Ni gharama zaidi Kwao na pia ya Kwao inayokuja bandari ya Dar es salaam waishushe mpakani sisi tukaichukue mpakani tuifikishe bandari ya dar es salaam kwa gharama zao sababu Ni yakwao sio yetu malori yetu yalikuwa yakipeleka mizigo Rwanda yanarudi matupu kwa kukosa mizigo ya kurudi nayoyakishashusha lakini Sasa yatapeleka mizigo ya rwanda mpakani na yatabeba mizigo ya Rwanda kurudi nayo bandari ya dar es salaam Ni uamuzi mzuri hongera kwa serikali

Malori ya mafuta yameruhusiwa watanzania wengi wanamiliki vituo vya mafuta Rwanda uamuzi mzuri pia

Kuhusu perishable goods pia uamuzi mzuri sababu bakhresa anapeleka kuuza vyakula Sana Rwanda Ni mfanyabiadhara mkubwa kule pamoja na akina Azania Millers Ni uamuzi mzuri una faida kwetu Sana

Haya makubaliano nayaunga mkono yako vizuri na maslahi ya Tanzania yamezingatiwa barabara

Wewe like chadema Huna ukijualo zaidi ya lockdown kujifungia Kama mwali
Hivi hiyo barua pia imezungumzia mizigo ya Rwanda kuja Dar au hayo ni mawazo yako? Je kipindi kile Cha sitofahamu Kati ya JK na PK mizigo ya Rwanda ilikuwa inapita wapi?
 
Hivi hiyo barua pia imezungumzia mizigo ya Rwanda kuja Dar au hayo ni mawazo yako? Je kipindi kile Cha sitofahamu Kati ya JK na PK mizigo ya Rwanda ilikuwa inapita wapi?
Ilikwama Rusumo madereva wa Tanzania walizuia mamia ya malori ya Rwanda Rusumo yasije Tanzania Baada ya wao kuzuiwa Kuingia Rwanda .Ya Tanzania yakawa hayaendi Rwanda na ya Rwanda hayaji Dar es salaam hata taarifa za habari huangalii? Wewe mtu ajabu mbona mna hata nyuzi humu.kibao za lockdown ya malori ya Rwanda Rusumo uko so outdated ulikuwa lockdown ya chadema Nini? Hata taarifa za habari ulikuwa husikilizi?

Kipindi Cha sintofahanu ya JK Kagame mwenyewe alikuja kumpigia magoti JK kuomba mizigo.iendelee kupita Dar es salaam Baada ya wafayabiashara kumgomra kupitisha Mombasa sababu ya umbali na gharama
 
Nimeona barua inazungumzia mizingo inayoelekea Rwanda na si transit good from Rwanda via Tanzania
 
Back
Top Bottom