Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Binafsi nimefurahishwa na kasi ya Rais Dkt. Magufuli. Naamini wapo pia wengi wanaoungana nami katika furaha hii. Rais Magufuli ameanza kwa kasi ambayo kama ataimaintain, Tanzania haimalizi miaka mitano itakuwa tayari ni nchi yenye kipato cha kati.

Hata hivyo wapo baadhi yetu ambao wanakejeli kasi hiyo. Hao kwangu ni watu waliozoea ubwete na bora liende!. Wanamwona Magufuli kuwa ni mtu atakayekuwa kauzibe kwao!

Wapigaji wote, wavivu wote na wazee wa madili wote watamchukia Rais Magufuli ila mi niseme na niwaombe tu kwamba tumpe support huyu jamaa kiukweli atatufikisha mahali fulani!

Tuwafichue wote wanaopanga kumhujumu (najua wanajulikana), tuwakatae kwani hawana nia njema na taifa letu.

Habari zaidi, soma => Mafanikio ya Rais Magufuli 2015 - 2020

=>Toka kwa Wananchi: Kero na Vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa...
 
Kweli huyu ndiye rais niliyemsubiri kwa miaka mingi sana. Sikuhizi yule jamaa yangu aliyekuwa anafanya kazi pale halmashauri ya manispaa ya kinondoni simuoni tena.

Yaani yeye alikuwa anatembepea maeneo mawili tu. Kwenye ATM na BAR. Anajifanya eti yuko serikalini ndo maana hafanyi kazi. Na kama wiki hivi sijamwona alafu nikimpigia simu anasema yuko busy. Ngoja aje amkute hayuko apigwe chini ntacheka alafu hata hana nyumba.

Magufuli hebu mtembelee na huyu umfinye kidogo ajifunze kuishi kwa kuchubuka kama sisi
 
Tumechoka dharau kutoka kwa vijinchi vidogovidigo mh. Raisi turudishe kwenye chati ya Afrika turudishe heshima we are big nation.

Ni kweli kabisa. Tuko nyuma kwa sababu ya kuleana. Hatuna nidhamu ya kazi wala nidhamu ya maisha. Tunaishi kwa kubabaisha tu. Tumekuwa wachuuzi wa bidhaa za nje ikiwemo mitumba. Hatufanyi uzalishaji wa bidhaa.

Polisi barabarani wanakula rushwa kama sala yao. Nenda pale kibaha maili moja uone namna polisi wenye vitambi wanavyokimbilia mabasi ya abiria kutoka mikoani yanavyoingia stendi. Konda wanaweka rushwa kwenye ratiba za mabasi na polisi wanachukua 'posho' hizo haramu. Watu hawafanyi kazi ofisini ......eti wanakweda kunywa chai........... cai Ukiigia .....gia nyi gB
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli , leo mchana amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kukutana na hali ya kumsikitisha.

Rais amesikitishwa na kuhuzunishwa na hali ya huduma kwa wagonjwa hususan wanaolala chini. Pia amekasirishwa na hali ya kutokujali wala kushughulikia vifaa vya kufanyia kazi ambapo amekuta mashine muhimu za uchunguzi wa magonjwa kama vile MRI na CT-SCAN zikiwa hazifanyi kazi kwa muda wa miezi miwili sasa, ilihali mashine kama hizo katika Hospitali za binafsi zinafanya kazi na wagonjwa wanaelekezwa kwenda kutafuta huduma huko?. Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema na kutoa maelekezo yafuatayo :

Rais amevunja Bodi ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambayo ilishamaliza muda wake na amemteua Prof. Lawrence Mseru , kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Muhimbili kuanzia kesho tarehe 10 Novemba, 2015.

Dkt. Hussein L. Kidanto ambaye ndiye anayekaimu hivi sasa, amehamishiwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambako atapangiwa kazi nyingine.

Balozi Sefue pia amesema, Rais ametoa wiki moja na kwa vyovyote si zaidi ya wiki mbili kwa uongozi mpya wa Muhimbili kuhakikisha kuwa mashine zote za uchunguzi wa magonjwa ambazo hazifanyi kazi zinafanya kazi na kuhudumia wananchi kama ipasavyo.

Tayari Wizara ya Fedha imetoa shilingi bilioni 3 kwa ajili ya kazi hiyo na kulipa madeni ya ukarabati wa mashine za uchunguzi wa magonjwa nchini.

Hata hivyo Katibu Mkuu Kiongozi amesema kuanzia sasa hospitali zote nchini zinatakiwa kutenga fedha kutoka kwenye mapato yao wenyewe na kuhakikisha mashine na vifaa vyote vya kazi vinafanya kazi wakati wote (Regular Maintenance).

Balozi Sefue pia metumia nafasi hii kuwaagiza watendaji na viongozi wote katika sehemu za kazi kuhakikisha wananchi wanahudumiwa ipasavyo na kazi za umma zinatekelezwa ipasavyo.

Hakutakuwa na huruma kwa watumishi wa Umma wasiojali wananchi na mahitaji yao. Amesisitiza Balozi Sefue.

Mwisho

Imetolewa na;

Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu ? Dar es Salaam.
9 Novemba, 2015
 
Ziara za magufuli na maagizo makali havikuwa vitu vipya kwangu kwani ata Mjomba alikuwa hivyohivyo.

namuona Raisi wangu anafanya maamuzi. Bila kujari yuko sahihi kiasi gani kwani ni bora kufanya maamuzi ukakosolewa na wachache kuliko kuogopa kufanya uamuzi. Ameanza kuikata kiu ya maamuzi magumu niliyoitamani kutoka kwa Lowassa.

Nashauri baada ya kuunda balaza la mawaziri Raisi wangu awapangie majukumu mazito mawaziri wake na awasisitize wawe wepesi kufanya maamuzi juu ya wizara zao na kuweka utaratibu utakaowezesha kujua na kusimamia hadi ngazi za chini kabisa ya idara zao.

Mfano waziri wa fedha aweze kuwajibishwa kwa kushindwa kuchukua hatua kwa ubadhilifu kwenye halimashauri

Au waziri wa elimu aweze kuwajubishwa kwa utoro na uzembe unaofanywa na walimu shuleni

Au Waziri wa afya awajibishwe kwa miji kujaa taka kila kona .

Hii inamaana kubwa sana hawezekani raisi agundue uozo mkubwa kwenye idara chini ya wizara unayoongozwa na waziri fulani na kuchukua hatua alafu waziri abaki salama. Waziri anasimamia wizara moja tu wakati raisi anaangalia wizara zaidi ya kumi na tano.

Hivyo hivyo waziri akigundua uozo kwenye idara iliyo chini yake sana mfano waziri wa elimu agundue shule fulani walimu hawahudhurii shuleni kabisa anatakiwa amwajibishe mkurugenzi na afisa elimu kwa tukio hilo kwani haiwezekani waziri agundue uozo chini alafu mkurugenz abaki salama wakati waziri anaangalia Tanzania nzima na mkurugenzi anaangalia halimashauri moja tu.

Pia mkurugenzi adili na wakuu wa shule.

Hivyo basi Rais wa ngu ukikuta uozo dili na mawaziri tu mawaziri ndio watajipanga, Na waziri wa kwanza kumfukuza hiyo wizara yake uisimamie wewe kwa muda ili mawaziri waone mfano.
 
Naogopa wasije wakamdedisha

Rais wetu apewe ulinzi mkubwa. Wazalendo wa kweli wa nchi hii wanataka maendeleo ya kweli. Wanataka uozo uliopo katika jamii yetu utokomezwe kwa kasi. Viongozi wamekuwa kama miungu watu. Wezi ndio wanapewa nafasi katika taasisi zetu. Waadilifu katika nchi hii ni kama hawatakiwi.

Wahuni tu wanapewa madaraka makubwa kwa kujipendekeza kwa viongozi. CCM kumeoza kwa sababu ya kubebana. Serikali nako kumeoza kwa kuwa CCM kumeoza. Taasisi za CCM zimeoza hazina viongozi wa maana wamejaa wababaishaji. Taasisi za serikali nazo zimeoza kwakuwa wanawekwa watu wasio na uwezo.

Asilimia 90 ya wakuu wa wilaya hawana uwezo. Uozo uko pia kwenye halmashauri. Halmashauri zimekuwa kitovu cha ulaji. Nchi hii ni lazima ikombolewe kutoka kwa viongozi mafisadi. CCM ijisafishe na serikali nayo isafishwe.
 
Wakati tuki furahia haya ya nagufuli , tuna muomba amalize ya zanzibar maalim aapishwe amsaidie naye aondoe uoza huko znz..seif hataki mzaha na kazi ...mpe haki yake Tanzania kwa ujumla ibadikike
 
Back
Top Bottom