stigajemwa
JF-Expert Member
- Nov 12, 2016
- 449
- 430
Napenda nimpongeze rais kwa kuruhusu sherehe za kumbukumbu za kitaifa ziendelee kufanyika.Nasema hivi kwakuwa mwaka juzi na mwaka jana alizuia baadhi ya sherehe hizi za kumbukumbu muhimu za kihistoria kwa kigezo cha kubana bajeti.
Baadhi ya wananchi tulizilalamikia sherehe hizi kuwa zinaligharimu taifa pesa nyingi za walipa kodi kwa kulipana posho na chakula.Lakini hatukuwa na maana zifutwe kama alivyofanya awali bali baadhi ya gharama na posho zisizo na tija zipunguzwe ktk kuadhimisha sherehe hizi.Hivyo kwa sasa tunaenda nae vizuri
Pia namuomba rais Magufuli aanze safari za nje ya nchi pamoja na Ulaya na Marekani kwa ajili ya kukuza diplomasia ya nchi kimataifa na kushawishi wawekezaji kuja nchini na kushawishi wahisani kuchangia ktk hhduma za jamii .Kwani tulipolalamika kuwa safari za rais zina ligharimu taifa hatukuwa na maana zifutwe bali zipunguzwe kwa idadi yake na msafara ujumuishe watu muhimu wa kazi tu.Hii ni kwa sababu baadhi ya ziara za nje zina tija kwa taifa.