Hongera Rais Magufuli kwa hili la mchanga wa dhahabu

ALWATAN KIZIGO

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
539
642
Rais, John Magufuli wiki iliyopita alifanya ziara katika Bandari ya Dar Es Salaam ambapo alibaini uwepo wa makontena yaliyokua yamesheheni mchanga wenye madini ya dhahabu,yaliyokuwa yamekwishafungwa tayari kusafirishwa kwenda nje ya nch,licha ya awali kuwapo kwa agizo lake la kutaka usafirishaji huo usitishwe.

Hatua ya Rais Magufuli kuzuia kusafirishwa kwa kinachoitwa mchanga wa dhahabu kupelekwa nje ya nchi kwa lengo la kulinda rasilimali za taifa, hakika ni ya kishujaa na yenye kustahili pongezi za dhati kwa sababu kwa miaka mingi, nchi iligeuzwa mithili ya shamba la bibi.

Mara kadhaa tumekuwa tukisikia malalamiko ya kuibiwa rasilimali za nchi kupitia njia hizi zinazoitwa mchanga wa dhahabu. Lakini cha kufurahisha ni kwamba, Rais ameonesha uzalendo kwa kusisitizia zuio, yote ni kwa faida ya nchi yetu.

Magufuli si wa kwanza kutaka kuona nchi inanufaika na rasilimali za nchi hii. Rais wa Awamu ya Kwanza, Mwalimu Julius Nyerere pia alikuwa mstari wa mbele katika hili la kukodisha machimbo ya dhahabu kwa wawekezaji bila ya kufanya tathimini ya kutosha. Alitaka madini yazuiwe kuchimbwa hadi nchi itakapokuwa na uwezo wa kufanya hivyo.
Vivyo hivyo, kama itaonekana ujanja ujanja ni mwingi katika hili la mchanga wa dhahabu, serikali inaweza kurudi kule kule kwa Mwalimu, yaani kutokuwa na papara ya kusafirisha mchanga hadi hapo nchi itakapokuwa na uwezo wa kuuyeyusha na kuuchenjua mchanga huo.
Ndiyo maana nasisitiza, pengine Rais Magufuli asiishie kwenye `mchanga wa dhahabu’, bali rasilimali zote zinazopigiwa kelele kwamba zinanufaisha zaidi wawekezaji kuliko nchi.

Aidha, natarajia ushauri mzuri kutoka kwa watunga sheria wa nchi hii ambao tunaamini kwa uzalendo wao, watafanya kazi nzuri kupitia kamati itakayoundwa na Spika Ndugai.
 
Ni vyema tukajuzwa kuhusu mikataba yake ili isiwepo sintofahamu baadae
 
Halafu mkishazuia mchanga usipelekwe nje ya nchi, mnaufanyia nini?
 
Tunauza rasilimali za nchi kwa glass ya wine.

Hongera Rais Magufuli
 
Natamani na mimi niungane na watanzania wenzangu kupongeza move ya Mtukufu Rais, ILA! nachelea kusema Sheria na Mikataba ilisainiwa na wanaccm wenyewe na yeye akiwemo! Muhimu hapa nashauri warudi Bungeni watunge sharia za kulinda maliasili ikiwemo madini yetu kwanza! Mikataba ivunjwe thru proper channels ....isije ikatokea tena eti kodi zetu zinalipa fidia kwa ACASIA et al ....
 
Ndugu zangu kwa mara ya kwanza nimekuwa nafatilia sakata la mchanga wa dhahabu naungana na Rais Magufuli kama kweli makontena yalikuwa na madini yenye thamani ya trillion 1.2 na kila mwezi yanaondoka kama aya tena zaidi ya miaka 17 hapa sisi kama nchi lazima tuungane kwa pamoja bila kuweka uchama mbele tusilaumiane kwa yaliyopita ila tuanze pamoja na kumuunga magufuli kwa hatua haliyochuchukua ingawa ina madhara makubwa ila akuna njia nyingine zaidi ya hiyo tuliyochukua kama taifa
 
Ndugu zangu kwa mara ya kwanza nimekuwa nafatilia sakata la mchanga wa dhahabu naungana na Rais Magufuli kama kweli makontena yalikuwa na madini yenye thamani ya trillion 1.2 na kila mwezi yanaondoka kama aya tena zaidi ya miaka 17 hapa sisi kama nchi lazima tuungane kwa pamoja bila kuweka uchama mbele tusilaumiane kwa yaliyopita ila tuanze pamoja na kumuunga magufuli kwa hatua haliyochuchukua ingawa ina madhara makubwa ila akuna njia nyingine zaidi ya hiyo tuliyochukua kama taifa
Una habari na zile ndege zinazotua na kuruka na dhahabu safi si chini ya tani kwa mwezi mara mbili au tatu?
 
Dhamira au nia ya JPJM ni safi sana, hata mimi namuunga mkono. Jinsi anavyo lishughulikia ina walakini sana. Amelifanya suala la kiutendaji kuwa la kisiasa na la kumpatia kiki.

Imekula kwetu chaliangu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom