Hongera Rais Kwa kuhutubia Kwa kiswahili

Hoja ni kwamba,katumia Kiswahili kwa ajili ya uzalendo na kukienzi kiswahili au katumia kwa vile upande wa pili kwake ni giza totoro?
 
Mbona marais wa china, france, korea wanapiga lugha zao? Si ndio maana huwa kuna translators jwenye mikutano mikubwa au wana kazi gan wale?
ningeshauri jpm atumie kiswahili maana mataifa makubwa yote wanatumia lugha zao
 
Hadithi hii inatufundisha nini??
Inatufundisha mambo mengi kama ifuatavyo:
(i) ni lazima tujipende na tuipende nchi yetu
(ii) kwamba wanaopaswa kusikiliza na kuelewa hotuba zetu ni watanzania kwa manufaa yao
(iii) kutambua kuwa ni kichekesho mwenzio anazungumza lugha ya kwao kwa faida ya wananchi wake wewe unahangaika kuzungumza lugha nyingine ambayo wananchi wako hawaielewi kwa ajili tu ya kumfurahisha mtu huyo na
(iv) Kwamba Tanzania haitaendelea kwa sifa tu ya kujua kiingereza.
 
Hao marais wa nchi hizo za Ulaya na Asia wanatumia lugha za nchi zao kwa kuwa walizitumia kama media of instruction wakati wanasoma degree zao. Tujiulize, Dr JPM alisoma degree zake zote tatu kwa kiswahili?
Degree tatu kwa kiingereza bado lugha haipandi una utani wewe teh teh teh teh...
 
Hivi mnatueleza kwamba hiyo thesis ya phd aliandika kwa kiswahili na aka-defend kwa kiswahili?
Mkuu mimi naamini kabisa pasina shaka kuwa yanayomkuta JPM yamewakuta wengi waliosoma michepuo ya sayansi kiingereza cha kujibia maswali huwa kipo na huwa wanashinda mitihani shida inakuja cha kuzungumza wengi huwa ni wazito tena akiwa mbele ya hadhara ndio kabisaaaa.
 
Degree tatu kwa kiingereza bado lugha haipandi una utani wewe teh teh teh teh...
Mtu anaweza kufahamu lugha bila ya kujua kuizungumza. Kuzungumza ni mazoea. Ma Ustadh wote wa Kiislamu Tanzania kwa mfano, wanafahamu Kiarabu, lakini wachache huweza kuzungumza.
 
Ukweli nimemkubali sana Rais wetu kwa kutumia lugha yetu ya Kiswahili maana na rais Wa Vietnam katumia lugha yake .Nimependa sana
ahaaaaaaaaa umemkubali baada ya kutema madongo oh sory kokoto arusha? Ahaaaaaa au na wewe ni kama yeye siku moja alivyosema "am a politicians" ahaaaa ni aibu iliyoje?
 
Seria
Napendekeza serikali iitamke kwamba, kiswahili ndio lugha kuu ya kiserikali kuanzia rais hadi watumishi wa chini, hii itatupa heshima popote na kwamba vijana wetu wanaosomea ukalimani watapata ajira pindi wageni hao wanapokuja nchini na rais anapokwenda nchi za nje.
Sema serikali ifute kiingereza kutumika secondary na vyuo hapo itaeleweka lakini kama itabaki kama ilivyo sasa halafu usikijue na una wadhifa mkubwa hapo hutaachwa kusemwa.
 
Jamani ifike mahali tukubali kuwa hautwezi kupata vyote!

Mkapa alikuwa na kiingereza kizuri, JK hamfikiii Mkapa lakini kidogo afadhali lakin hawa wawili hawakuweza kuvaa viatu vya Mwalimu. Ni Magufuli pekee ameonesha nia na uwezo wa kuvaa viatu hivyo (kwa maoni yangu, so far). Hii inatosha kwa sasa. Hilo la kiingereza atafute walimu wa tuition (aache ubishi tu), wamsaidie kwa miezi sita kutakuwa na improvement kubwa tu.:D:D:D
 
...jana kwenye dhifa na mgeni wake JPM alitumia lugha gani?...ama alisoma hotuba ya kuandikiwa?....ni vema aendelee kutumia kiswahili popote ndani na nje... Hii itamwondolea aibu na kejeli toka ndani na nje....na inaweza kumwongezea confidence pale anapotaka kuongea mambo ya msingi kwa mustakabali wa taifa....kuna wakalimani wengi wako kwa ajili ya kazi hiyo..na wala si aibu kuwatumia....
 
Mwenyekiti wa EAC anaonesha mfano kwa kufanya Kiswahili iwe ndo lugha rasmi Afrika mashariki Hongera Raisi wetu.
 
Kingereza cha kuongea kinataka practice,sasa hawa watu wa sayansi huo inakua ngumu kwao kuliko wana art ambao hudeal na novel nyingi kiasi cha kukuza misamiati na hivyo kuongea inakua rahisi.

Aache kuhutubia kwa kingereza kama kinasumbua kwani akiforce kuna siku atachapia vibaya na itakua noma kweli kama watu watapasuka kwa kicheko
 
Huo mtazamo wako mkuu,coz kiingereza sio lugha rasmi kwetu so raisi kuongea kiswahili haimaanishi hajui kiingereza but ameamua kuienzi lugha yetu,unatakiwa kuwa mzalendo mkui
 
Mkuu mimi naamini kabisa pasina shaka kuwa yanayomkuta JPM yamewakuta wengi waliosoma michepuo ya sayansi kiingereza cha kujibia maswali huwa kipo na huwa wanashinda mitihani shida inakuja cha kuzungumza wengi huwa ni wazito tena akiwa mbele ya hadhara ndio kabisaaaa.
Tupo wengi sana,ukiniondoa kwenye hadhara sina peer kabisa
 
Huo mtazamo wako mkuu,coz kiingereza sio lugha rasmi kwetu so raisi kuongea kiswahili haimaanishi hajui kiingereza but ameamua kuienzi lugha yetu,unatakiwa kuwa mzalendo mkui
Hapo ndiyo mnapokosea eti analienzi acheni upuuzi bana...
Watu kama Vonix namuelewa kabisa...
 
Back
Top Bottom