Hongera Rais Kikwete kwa Uongozi Shupavu!

MAFILILI

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
2,377
1,190
Ni faraja kwa Watanzania kuona uongozi bora wa Rais Jakaya Kikwete umefanikisha maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru yakiambatana na matukio yaliyojaza furaha lukuki wa wananchi wa rika zote, makabila yote, dini zote na vyama vyote nchini mwetu.

Uongozi ulio adirifu kutoka na Amiri Jeshi Mkuu, umetuletea Watanzania siku ya jana iende vizuri huku tukijipongeza kwa sherehe husika.

JK twakutakia afya njema ili uweze kumalizia miradi mikubwa iliyoanza kwa kipindi chako cha uongozi kwa vile:-
1. Chuo Kikuu cha Afya na Tiba eneo la Msoga
2. Ujenzi wa Barabara za Juu kwa Juu jijini DSM
3. Ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara - DSM
4. Ujenzi wa Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa - Mwl Nyerere, Jijini DSM
5. Uanzishwaji wa Usafiri wa Treni jijini DSM
6. Ujenzi wa daraja la Kigamboni
7. Upanuzi wa Chuo Kikuu cha Muhimbili - eneo la Luguruni
8. Ujenzi wa bandari Bagamoyo
9. Uboreshaji wa makazi na mafunzo kwa Polisi
10. Uanzishwaji wa Katiba Mpya

Watanzania tunapenda uongozi wako; wasemehe wanaobeza uongozi wako hasa CHADEMA; wenye macho tunayaona mabadiliko yenye tija yaliyopatikana wakati wa uongozi wako
 
Ukiondoa uanzishwaji wa katiba mpya yote uliyoorodhesha siyo kazi ya rais

Tunamtaka rais wetu:

  1. Asimamie ukuzaji wa uchumi;
  2. Alinde amani na kudumisha utawala wa sheria;
  3. Alinde rasilimali zetu; na
  4. Apambane na rushwa na mafisadi.

Hizi ndizo kazi za rais na si kushughulikia kazi za mawaziri!
 
Hapo ndipo tunazidi kusisitiza mabadiliko yanayotakiwa kuenda na katiba sio vyema kunyamaza
 
Mimi sidhani kama CHADEMA wanabeza yale mema yaliyofanywa na JK kilio chao ni kwamba hayo aliyofanya ni machache sana kulinganisha na rasilimali mali za Nchi zinavyopotea kizembe, mfano kutoroshwa wanyama, wizi ndani ya taasisi za serikali na kushindwa kuwajibishana, ufanisi mbovu wa baadhi ya mawaziri na watumishi wa serikali ukwepaji kodi na uingizwaji wa bidhaa feki, yapo mengi yakisimamiwa vizuri hiyo miradi unayosema ingekuwa mara 4 ya hapo.

Yapo mengi yanayofanya uongozi wa Mh JK uonekane si imara, maisha magumu kwa WATZ, shilingi kushuka thamani kila uchwao, chukulia matukio ya Polisi kuua raia, katika kipindi kifupi tumeshuhudia matukio mengi ya namna hiyo lakini hembu tuambizane ni nani mpaka sasa amechukuliwa hatua au kuwajibishwa? hakuna, sasa haya sio chadema tu wanayolilia hata raia wasio na vyama wanapenda kuona Rais wao akichukua hatua, wanapenda kuona rais wao akitoa amri wauza unga, watoa rushwa na wapokea rushwa wakamatwe, mwenyewe si amesema anawajua, mbona kimya.

Binafsi namuombea afya njema na maisha marefu na Mungu ampe uwezo zaidi wa kutekeleza yale yaliyo mema kwa WATANZANIA,aitete katiba na kuilinda kwa dhati bila kumuonea haya yeyote, awatumikiea waliomchagua na itikadi za vyama ikae pembeni, yeye ni Rais wa WATANZANIA wote.......MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
MAFILILI

Umesahau kusema pi akajenga Mlimani City...pambaaf kabisa.Vingi ya vitu alivyosem ani upanuzi wa taasisi husika chini ya mamlaka zake.Gesi hawakuwa na option zaidi ya mwekezaji kuona ndio nji ashaihi ya kuipeleka dar, NSSF wanatafuta pa kuwekeza ili hela zionezeke, muhimbili bado wan ammalaka inayoweza jua wanahitaji nini na hivyo kuweka katk mipango yake kam ilivyo kwa UDSM walivyoamua jenga mlimani City na hivyo kutafuta funder.

Mengine umeandika hata kuanza bado.
 
Last edited by a moderator:
heshima mbele,,
tuendeleze list za pongezi,,

11.kubariki utoroshwaji wa tembo wetu

12.kuipa meno takukuru kwa kupigana na rushwa kubwa kubwa & rushwa ndogo ndogo

13.kuwakamata vinara wa dawa za kulevya aliotamba kuwafaham

14.kuzidisha ugumu wa maisha kwa walalahoi

15.kufanikiwa kuwavua magamba mafisadi wote

16.kuimaliza dunia kwa ziara za kutembeza bakuli na kukuza uchumi wa nchi

17.kuipa nchi 2015 rasmi kwa upinzani in a peaceful way

haya kimbia haraka sana nenda lumumba pale kachukua posho ya lunch kwa nape kabla hajaondoka
 
Naona Upo Kiribu nae mwambie wanafunzi tunasubiri zile computer alizotuahidi ama ulikuwa upepo tu?
 
Pongezi zaidi:
kutoa elimu bora kwa watoto wa wao wa kwetu mmh
kuongeza idadi ya wanafamilia kwenye SiSieM na serikali
 
Umesahau kusema pi akajenga Mlimani City...pambaaf kabisa.Vingi ya vitu alivyosem ani upanuzi wa taasisi husika chini ya mamlaka zake.Gesi hawakuwa na option zaidi ya mwekezaji kuona ndio nji ashaihi ya kuipeleka dar, NSSF wanatafuta pa kuwekeza ili hela zionezeke, muhimbili bado wan ammalaka inayoweza jua wanahitaji nini na hivyo kuweka katk mipango yake kam ilivyo kwa UDSM walivyoamua jenga mlimani City na hivyo kutafuta funder.mengine umeandika hata kuanza bado.
Kwa vile huoni mema yaliyofanyika wewe elezea mafanikio ya CHADEMA na M4C,
-kuua mu Morogoro
-kuua mwandishi Iringa
-maandamano yasiyoisha
-wabunge wenu waliochaguliwa wote maneno matupu yasiyovunja mfupa wala kuleta maendeleo
-mlisema hamumtambui rais
-mlisema na nchi haitatawalika
-mlichukua msaada wa Kameruni

Katika yooote hayo ofisi yenu bado iko uchochoroni, maneno meeeengi!
 
Asante sana Jh Kaya kwa kuwapelekea wakina mama maji hadi mlangoni mwao.
ImageUploadedByJamiiForums1355143792.060610.jpg
 
Tutaendelea kumkumbusha kuhusu
*Ajira kwa vijana
*Maisha bora kwa kila mtanzania
*Kuigeuza Kigoma kuwa Dubai!
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom