Hongera Profesa Ted Mlyamkono na Profesa Hugh Mason kwa kitabu cha Game Changer -" Magufulis first term in office"

dndagula

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
1,457
1,442
Nimefurahishwa na wazo la Profesa Ted Malyamkono na mwenzake kwa kuandika kitabu kinachoelezea mchango wa Rais JP Magufuli na mabadiliko aliyoyaleta ya kijamii,kisiasa na kiuchumi nchini. Mwelekeo Mpya

Kitabu hiki angalau kimejaribu kuonyesha sera na maono ya Rais Magufuli kimaandishi na kitaaluma katika kuiongoza nchi. Uongozi ni kipaji lakini pia ni taaluma.

Kila awamu tumeona mabadiliko, lakini kasi ya mabadiliko ya sasa ni kubwa mno na yanaonekana wazi. Falsafa ya Awamu hii ya hapa kazi tu inalenga kwenye matokeo yanayopimika( result oriented philosophy)pamoja na maadili nidhamu na uwajbikaji ambavyo ndiyo msingi na nguzo ya mafanikio.

Hapo awali awamu zilizopita Hapakuwa na misistizo kisiasa wa falsafa bayana yenye kuzingatia matokeo ingawa ilizungumzwa kwenye sheria kadhaa.

Aidha, uwepo wa mifumo yenye msisitizo wa ukusanyaji Kodi,Ulinzi wa raslimali, Udhibiti wa ufisadi nchini, uwajibikaji na mahusiano/mashirikiano ya kimataifa,miundombinu mipya ya kiuchumi na kijamii, mifumo mipya kwenye madini nk.

Haya ni mabadiliko makubwa ambayo kwa kweli ni "change maker" kwa kipindi hiki cha socio economic transition.Hogera prof Mlyamkono kwa kitabu hiki kizuri. Ninakubaliana na Waziri Mkuu kuhusu kuchapisha kitabu hiki kwa kiswahili kwa vile ni Urithi wa Vizazi Vijavyo.Mungu Ibariki Tanzania.
 
Suppression of democracy wakati mnatoa maoni kwenye jamii forum bila bughudha!
Ni kwa sababu fulani tu but otherwise haya maoni usingeyaona, unadhani zile kesi za Max zilikuwa zina nini ndani?

So unapoandika jambo rudi nyuma utafakari why jf still openly kwa wachangiaji wake!!
 
Mbona tunajua kuna Wabunge walihongwa mamilioni kusaliti upinzani ili kwenda "kuunga mkono juhudi"---- vipi hao maprof, hawajahongwa "kuunga mkono juhudi"???

Awamu hii ina mambo.
 
Kiongozi bora ni yule anayefuata katiba na sheria za nchi...Mfano mkuu kwa bara la Africa ni Ghana.

Hao ni maprof wachumia tumbo.
 
Kuna siku wewe utajitambua au ndio pambio baada ya jingine? Kwa nini kila mwaka Mexence Melo yuko mahakamani? Pathetic! Utakua lini wewe?
Kuna mijitu ina roho mbaya na za kishetani. Yaani mahangaiko yote wandugu Maxence Melo, Mike Mushi na JF Team wayapatayo yeye haoni wala kuonyesha " appreciations"!!
Yaani roho mbaya iliyopitiliza ya kichawi ndiyo hii.
 
Yeye anaona hayo ni afya njema kwa tasnia ya habari! Jana nimemsikiliza msemaji wa jeshi la Uganda. Kiswahili kizuri sio cha kipande ya huko. Nafikiri ni mtanzania aliajiriwa kujibu maswali ya uchafuzi bbc. Shallow and devoid of logic blah blah, very characteristic of wabongo! Sikilizia matokeo huko. 'Wakurugenzi' wanatangaza wabunge wa upinzani wakibwaga mawaziri wateuliwa wa Museveni. Yeye yuko busy anaiba kura za BW. Hakuna cha Nileteeni Gwajima. Hakuna anayempelekea!
 
Nimefurahishwa na wazo la Profesa Ted Malyamkono na mwenzake kwa kuandika kitabu kinachoelezea mchango wa Rais JP Magufuli na mabadiliko aliyoyaleta ya kijamii,kisiasa na kiuchumi nchini. Mwelekeo Mpya

Kitabu hiki angalau kimejaribu kuonyesha sera na maono ya Rais Magufuli kimaandishi na kitaaluma katika kuiongoza nchi. Uongozi ni kipaji lakini pia ni taaluma.

Kila awamu tumeona mabadiliko, lakini kasi ya mabadiliko ya sasa ni kubwa mno na yanaonekana wazi. Falsafa ya Awamu hii ya hapa kazi tu inalenga kwenye matokeo yanayopimika( result oriented philosophy)pamoja na maadili nidhamu na uwajbikaji ambavyo ndiyo msingi na nguzo ya mafanikio.

Hapo awali awamu zilizopita Hapakuwa na misistizo kisiasa wa falsafa bayana yenye kuzingatia matokeo ingawa ilizungumzwa kwenye sheria kadhaa.

Aidha, uwepo wa mifumo yenye msisitizo wa ukusanyaji Kodi,Ulinzi wa raslimali, Udhibiti wa ufisadi nchini, uwajibikaji na mahusiano/mashirikiano ya kimataifa,miundombinu mipya ya kiuchumi na kijamii, mifumo mipya kwenye madini nk.

Haya ni mabadiliko makubwa ambayo kwa kweli ni "change maker" kwa kipindi hiki cha socio economic transition.Hogera prof Mlyamkono kwa kitabu hiki kizuri. Ninakubaliana na Waziri Mkuu kuhusu kuchapisha kitabu hiki kwa kiswahili kwa vile ni Urithi wa Vizazi Vijavyo.Mungu Ibariki Tanzania.
Tutakapo pata maudhui halisi ya kitabu tutauona ugame changer--Naona wengi wamefocus kwenye kujenga lakini wamesahau upya na ubunifu kwenye sector kuu kama kilimo na uvuvi,biashara,elimu,sayansi na technolojia
 
Back
Top Bottom