Hongera Prof Ndalichako lakini

Ngwananzengo

JF-Expert Member
Jul 28, 2012
1,911
1,314
Prof Ndalichako ametoa maamuzi ya kufuta utoaji wa matokeo kwa mfumo wa GPS. Watu wamemuunga mkono na kushangilia. Wengi wanasema ni hatua nzuri ya kuitoa elimu yetu "ICU". Mimi pia nampongeza. Mosi kwa kuonyesha tafsiri hasa ya maana ya uongozi kwa kutoa uongozi. Pili kwa kufanya maamuzi yasiyoongozwa na hisia.

Pamoja na hayo ni vizuri tukatambua kuwa "ELIMU" ni Mali ya jamii/Taifa na si serikali. Si jambo jema kuigeuza elimu kama "patching bag" kwa kila mtendaji kufanya anachotaka pindi anapopewa dhamana ya kuongoza. Asasi za kiraia, taasisi za dini na Serikali, taasisi za elimu, wazazi, wanafunzi na wataalam walikatae jambo hili. Wadau niliowataja watambue haki yao waliyonayo ya kushiriki na kutoa maana juu ya mabaliko yoyote katika sekta ya elimu. Prof Ndalichako aandae mfumo utakaozuia elimu kuchezewa kama "patching bag".
 
Umeongea vizuri, lakini unasahau kuwa Rais ana unlimited and unquestionable powers, like wise Waziri. Hivyo basi tupate katiba itakayotoa maelekezo elimu iweje na si kumpa Rais na Waziri mamlaka ya kufanya mabadiriko anaposhauriwa na mke wake
 
Nakubaliana na wewe. Kama katiba ndio suluhu basi natuitafute. Lakini ni vizuri tukajiuliza katiba ipi ile iliofanya wabunge wakasakata "mayenu" au ile ya wananchi.
 
'patching bag'----'punching bag'
GPS (Global Positioning System)------GPA (Graded Average Points)
 
GPS ni global positioning system na pia kunaweza kuwa na maana nyingne ile mojawapo ni hiyo. Sasa unasema dr ndalichako amefuta huo mfumo kwanza tuelezee ulikuwa unatumikaje kwenye elimu yetu? Ulianza kutumika lini?

Back
Top Bottom