nderingosha
JF-Expert Member
- Mar 20, 2011
- 4,281
- 3,243
Nimefurahishwa na kitendo cha Prof.Muhongo...waziri wa nishati na madini kupiga marufuku matumizi ya wataalam wa nje kwenye shughuli ambazo zinaweza kufanywa na wataalam wetu wazalendo.....hili ni jambo jema kwani litaondoa ugonjwa wa utegemezi uliojaa TZ kwa serikali kutokupenda kuwatumia wataalam wake wazalendo...jambo ambalo limepelekea nchi kuingizwa mikenge bila kujua....mara nyingine hao wanaoitwa wataalam(experts)wamekua mzigo mzito kwa serikali kiasi cha kusababisha kudhoofisha morale wa wataalam wa kizalendo.....jambo ambalo linadhoofisha utendaji kwa kiasi kikubwa kwani wao experts hulipwa pesa nyingi sana ukilinganisha na wataalam wazalendo....
My take:
My take:
- Ni lini serikali itaanza kuwavuta nyumbani wataalam wazalendo wa kitanzania waliopo nje ya nchi ili waje kusaidia kuendesha nchi hii??...Namaanisha wataalam katika fani zote.....
- Ni lini TZ wataanzisha ..a "think tank institution" au "professional incubator"....itakayokuwa na wajibu wa ku accomodate wataalam wetu wataokuwa wanamaliza nchini na nchi za nje au wastaafu ....ili wawepo nchini muda wote watakapohitajika na nchi kwenye taaluma zao??....jambo ambalo litaondoa utegemezi wa wataalam wa nje......
- Ni lini JK ataacha tabia ya kuwalisha vyakula kwa bei mbaya watanzania walioko nchi za nje(haswa USA)..tena kwa kodi za mtanzania anaepigika TZ....na badala yake ajenge utaratibu wa wa kuongea na professionals wa kitanzania walioko pande zote za dunia hii(si marekani peke yake)....Najiuliza ni kwanini JK anapokuwa marekani ana tabia ya kuongea na wabongo..lakini aendapo nchi nyingine hafanyi hivyo...why?....what is so special with Tanzanians living in USA???......wana mchango gani special kwa TZ hawa????.....Hivi JK anajua kuna watanzania wangapi wako India....China... Russia...Poland...Scandinavia ..na hata nchi nyingine za africa kama RSA...Namibia..Botswana etc?????...tena real professionals??????wanaoweza kuwa na mchango mkubwa TZ kuliko hata hao wanaoishi USA?.....Rais anapoonyesha ubaguzi wa wazi wazi kwa raia wake walioko nje ya nchi lazima kuwe na maswali mengi ya kujiuliza......
- Ni lini serikali ya TZ itafanya sensa ya professionals wake walioko nje ya nchi ili kujua potential iliyopo na hatimae kuwa na taarifa zao ili hatimae kuwatumia mara watakapohitajika???.....nasema hivi maana kuna watanzania wengi mahiri wako nje ya nchi ambao wangeweza kutumika kusukuma gurudumu la maendeleo na hata kupunguza mzigo wa serikali kulipa bei mbaya kwa foreign experts....ambao mara nyingine ni mafeki..au wababaishaji.......Kinachotakiwa ni kuwakaribisha nyumbani tu na ikiwezekana kuwapa vitengo hawa wataalam wa kitanzania...ili waweze kutoa mchango wao ipasavyo......jambo ambalo halifanyiki.....kwani mara nyingi tunaona wanabezwa mara warudipo nyumbani.....na hata kuwa frustrated mara nyingine......Huu ugonjwa wa kubabaikia wageni TZ utaisha lini?????......Thanks to Prof.Muhongo kwa kuliona hili.........maana yeye nae amaeishi nje....ameliona hili.......wish we had people of his thinking in TZ.....tusingekuwa tulipo.....kina Kagame wa Rwanda hili ameliona na sasa ana value mchango wa warwanda walioko nje....