Hongera Prof.Muhongo kwa kupiga marafuku kuwatumia wataalam wa nje...Serikali ya TZ je??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera Prof.Muhongo kwa kupiga marafuku kuwatumia wataalam wa nje...Serikali ya TZ je???

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nderingosha, May 21, 2012.

 1. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2012
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,545
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Nimefurahishwa na kitendo cha Prof.Muhongo...waziri wa nishati na madini kupiga marufuku matumizi ya wataalam wa nje kwenye shughuli ambazo zinaweza kufanywa na wataalam wetu wazalendo.....hili ni jambo jema kwani litaondoa ugonjwa wa utegemezi uliojaa TZ kwa serikali kutokupenda kuwatumia wataalam wake wazalendo...jambo ambalo limepelekea nchi kuingizwa mikenge bila kujua....mara nyingine hao wanaoitwa wataalam(experts)wamekua mzigo mzito kwa serikali kiasi cha kusababisha kudhoofisha morale wa wataalam wa kizalendo.....jambo ambalo linadhoofisha utendaji kwa kiasi kikubwa kwani wao experts hulipwa pesa nyingi sana ukilinganisha na wataalam wazalendo....

  My take:
  • Ni lini serikali itaanza kuwavuta nyumbani wataalam wazalendo wa kitanzania waliopo nje ya nchi ili waje kusaidia kuendesha nchi hii??...Namaanisha wataalam katika fani zote.....
  • Ni lini TZ wataanzisha ..a "think tank institution" au "professional incubator"....itakayokuwa na wajibu wa ku accomodate wataalam wetu wataokuwa wanamaliza nchini na nchi za nje au wastaafu ....ili wawepo nchini muda wote watakapohitajika na nchi kwenye taaluma zao??....jambo ambalo litaondoa utegemezi wa wataalam wa nje......
  • Ni lini JK ataacha tabia ya kuwalisha vyakula kwa bei mbaya watanzania walioko nchi za nje(haswa USA)..tena kwa kodi za mtanzania anaepigika TZ....na badala yake ajenge utaratibu wa wa kuongea na professionals wa kitanzania walioko pande zote za dunia hii(si marekani peke yake)....Najiuliza ni kwanini JK anapokuwa marekani ana tabia ya kuongea na wabongo..lakini aendapo nchi nyingine hafanyi hivyo...why?....what is so special with Tanzanians living in USA???......wana mchango gani special kwa TZ hawa????.....Hivi JK anajua kuna watanzania wangapi wako India....China... Russia...Poland...Scandinavia ..na hata nchi nyingine za africa kama RSA...Namibia..Botswana etc?????...tena real professionals??????wanaoweza kuwa na mchango mkubwa TZ kuliko hata hao wanaoishi USA?.....Rais anapoonyesha ubaguzi wa wazi wazi kwa raia wake walioko nje ya nchi lazima kuwe na maswali mengi ya kujiuliza......
  • Ni lini serikali ya TZ itafanya sensa ya professionals wake walioko nje ya nchi ili kujua potential iliyopo na hatimae kuwa na taarifa zao ili hatimae kuwatumia mara watakapohitajika???.....nasema hivi maana kuna watanzania wengi mahiri wako nje ya nchi ambao wangeweza kutumika kusukuma gurudumu la maendeleo na hata kupunguza mzigo wa serikali kulipa bei mbaya kwa foreign experts....ambao mara nyingine ni mafeki..au wababaishaji.......Kinachotakiwa ni kuwakaribisha nyumbani tu na ikiwezekana kuwapa vitengo hawa wataalam wa kitanzania...ili waweze kutoa mchango wao ipasavyo......jambo ambalo halifanyiki.....kwani mara nyingi tunaona wanabezwa mara warudipo nyumbani.....na hata kuwa frustrated mara nyingine......Huu ugonjwa wa kubabaikia wageni TZ utaisha lini?????......Thanks to Prof.Muhongo kwa kuliona hili.........maana yeye nae amaeishi nje....ameliona hili.......wish we had people of his thinking in TZ.....tusingekuwa tulipo.....kina Kagame wa Rwanda hili ameliona na sasa ana value mchango wa warwanda walioko nje....
   
 2. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Tupo wataalamu wengi sana tunaoishi nje ya nchi ambao tungeweza kuchangia maendeleo ya hapo nyumbani. Tatizo moja liliopo ni kuwa hakuna utaratibu maalum uliowekwa na serikli wa kuonyesha ni sehemu zipi zinahitaji wataalam na wa sifa zipi, na pia kama kuna nia ya kuwapokea wataalam hao.
   
 3. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  wakati mwingine ni bora kumuweka mtaalam wa nje...hivi umeshaona jinsi watanzania tunavyofanya kazi???
   
 4. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2012
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,545
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  wazi kabisa.....hakika kama kuna kitu serikali ya TZ inapoteza ni kutowatumia wataalam wake ambao wengi husomeshwa kwa pesa nyingi lakini wanaishia kukimbilia nje kutafta green pastures...bila kuweka mazingira ya kuvuta nyumbani watanzania hawa TZ itakuwa inamwaga maji kwenye gunia....kwani watasomesha watu kwa pesa nyingi na matokeo hawatayapata...kwanini hili watawala hawalioni???..msingi wa TZ kusomesha wataalam wake ni ili waisaidie TZ na si nchi za nje....tena wataalam wa kitanzania nje tayari wana exposure na experience ya kutosha kuisaidia TZ katika karne hii ya 21....ndio maana wamekubalika nje ya nchi.....we really need people like Prof.Muhongo to make the government realize this painful fact.....
   
 5. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #5
  May 21, 2012
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,545
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  ndio sababu nasema wataalam wa kitanzania walioko nje watakua mmbadala poa...kwani tayari wana exposure na jinsi wenzet wanavyofanya mambo....i mean ile hali ya kujali muda...kujituma na kufanya kazi ili kupata majibu....hili linakosekana sana TZ....ndo sababu tunashobokea wageni....mbona watanzania hawa hawa ukiwapeleka nje wanawajibika???
   
 6. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #6
  May 21, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Nimefanya kazi huku nje kwa miaka 20 sasa kwa bidii kama wafanyakazi wengine na katika mazingira ya huku. Kuhusu ufanyaji kazi wa Tanzania ni kuweka mazingira ya kufanya kazi kwa nidhamu na kujenga utamaduni kuwa kazi yako ndio msingi wa maisha yako, familia na jamii kwa ujumla. Tukijua hilo patakuwa na uwajibikaji katika kazi, mfanyakazi atawajibika, na mwajiri vilevile atawajibika kwa mfanyakazi. Vitu vyote hivyo lazima viende sambamba.
   
 7. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #7
  May 21, 2012
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Namhurumia Prof... maana atakutana na mkono wa PPRA.... ahahaha mifumo ya kuiba imewekwa Prof.
   
 8. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #8
  May 21, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  TENDER..... & TENDERING......teh teh teh
   
 9. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #9
  May 21, 2012
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,545
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  hiyo mifumo ya kuiba iliyowekwa ndo ya kupambana nayo.....hapo ndipo watanzania wanaopewa dhamana wanaposhindwaga......na ndio maana hata kina Nundu walishindwa...maana walikuwa waoga wa kuchukua hatua....ukiangalia watu kama kina Nundu wana CV nzuri tu...maana walifanikiwa hata kufanya kazi nje poa....tatizo walipopewa madaraka wakaingia mkenge huo huo wa mifumo feki...matokeo ni kukwama na kubaki kulalama....Umeona Prof.Muhongo kaingia tanesco tayari kasimamisha utekelezaji wa sera mpya ya umeme/nishati..maana ni feki...vile haikushirikisha wadau...kwa maana ilikuwa inaandaliwa na wachache(kina ngeleja et al) kwa ajili ya kutafuna nchi...Tatizo la watanzania ni kupenda short cuts.....hata kusoma vitu ni wagumu....hili ni janga......kwa prof.kusoma documents kubwa na kuzielewa si shida hata kidogo....Ukiona msomi ameingia kwenye kashfa za ufisadi ujue ni kwa ajili ya tamaa binafsi........
   
 10. Fisherscom

  Fisherscom JF-Expert Member

  #10
  May 21, 2012
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,442
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Mwanzo mzuri,tusikate tamaa mapema kiasi hicho. Muda upo na kinaweza fanyika kitu cha maana. Tumpe muda kwanza.
   
 11. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #11
  May 21, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Dingswayo alikuwa mfalme wa wapi vile? Wewe cheza na mitandao ya Tanzania. Wataalam wangapi wamerudi na wakakumbana na vigingi; idadi ni kubwa mno. Mkuu kuna tatizo la mfumo. Watu wengi wakitoka kwenye private sector (Yaani ambao hawako kwenye serikali ya Tanzania) wakifika na kuja na mifumo yao mipya ya kiutendaji wanakumbana na mifumo na magenge yaliyojijenga na kujiimarisha ndani ya taasisi husika; basi hao wataalam toka nje huishia kuonekana hawafai. Ukweli ni kwamba huwa wamekuja bila kujua kwamba kuna watu wamechomeka mirija mahala fulani na wao hujaribu kuikata hiyo mirija; vumbi lake kaka utatamani urudi ulikotoka.

  Huyu prof. ana maono kwa kweli wataalam wa nje wanatuhujumu lakini muda si mrefu utasikia kwamba anataka kwenda kinyume na sheria ya manunuzi ya mwaka 2004 (2011). Tusubiri tu tuone. Inabidi prof. awe na ngozi ngumu manake huko yeye ataonekana kama Osu (Things fall apart).
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #12
  May 21, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kasheshe hapo ndipo kwenye shida. Mkuu nimefuatilia hii the Public Procurement Act iliyoanzisha PPRA nikagundua kwamba ilitengennezwa na World Bank. Hiii sheria yetu inafanana na sheria ya Uganda na ile ya Kenya. Wazungu kwa makusudi walijiwekea vipengele vya kujipendelea ndani ya kichaka cha utandawazi! Sheria yao halafu uje kuwaengua kirahisi! Naona panakaribia kuchimbika. Huenda kwa hilo tamko tu tayari wameishakutana na kutaka kulithibitisha hilo tamko isije ikawa ni vyombo vya habari.

  Hawa mabepari/development partners wamejipanga ile kinoma.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #13
  May 21, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kimbunga

  Dingswayo alimfuatia Chaka Zulu, mfalme wa waZulu.

  Kama nilivyoeleza kwenye post yangu nilisema kuwa ni lazima mazingira yawekwe ili mtu aweze kufanya kazi kwa ufanisi, kinyume cha hapo haitawezekana na tutashindwa kufanya kazi. Niliondoka nchini kuja ughaibuni kusoma PhD. Nilijua wazi kabla ya kuondoka kuwa sitarudi kazini hapo kwa sababu wakubwa wa kazi walikuwa wanafanya juu chini kuwavunja moyo wale wote waliokuwa na elimu juu yao, labda kwa kuogopa kupoteza vyeo vyao. Huo ndio mfumo niliouacha na nadhani bado unaendelea sasa pamoja na madudu mengine mengi.
   
 14. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #14
  May 21, 2012
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  nilipompendea prof ni pale aliposema yeye si mwanasiasa na ni msomi....ninapoogopa ni pale aliposema load shedding ikitokea management itafutwa kazi ( katika hotuba yake ya juzi ).....sijui tuwashe kuni kuzalisha umeme:A S embarassed::A S embarassed::A S embarassed:

  nakupongeza sana prof na kama utasimamia maneno yako ni wazi shirika litabadilika sana hongera sana ni timu ya uhakika tunategemea mengi kutoka kwenu pamoja na uwajibishwaji kwa wale wabadhirifu na wazembe,
   
 15. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #15
  May 21, 2012
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hakuna lisilowezekana, tatizo ni sisi wenyewe either tumesha-changanyikiwa au tumeshajenga vichwani mwetu kuwa hiyo mirija haikatiki kamwe. Kwa mfano angalia mtu kama Magufuli akibomoa majumba na magereji yaliyojengwa kwenye road reserve tunamlaumu sana hata hapa JF. Wakati huohuo bado tunamlaumu Prof. Tibaijuka (ambaye nae ni mtaalam aliyekuwa nje ya nchi!!!) eti kwanini anaogopa kubomoa nyumba zilizojengwa kwenye mkondo wa bahari/kwenye viwanja wazi/recreational etc. etc....:hat:
   
 16. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #16
  May 21, 2012
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  We Engineer unataka kusema hauna jenereta la serikali pale nyumbani kwako?:lol:
   
 17. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #17
  May 21, 2012
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,545
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  dada Nsiande naona we ni kati ya wafanyakazi walio chini ya wizara ya huyu Prof.na ni vizuri kuona unamuunga mkono.....i hope mtatoa support ya kutosha ili jamaa aibadilishe wizara maana ni kupitia wizara hii taifa la TZ litaweza kunufaika na raslimali tele za madini...gas...coal...uranium....na probably mafuta....yaani hii wizara inahitaji uzalendo wa hali juu....jambo ambalo wale majambazi kina ngeleja na malima hawakulifanya...kwasababu ya tamaa zao.....
   
 18. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #18
  May 21, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  tatizo la serikali yetu haijali wasomi
  tunaambiwa kila siku tusome lakini ukipata admission ya chuo cha nje
  unaambiwa hakuna hela huku wao kwa wao
  wakipeana allowances na vikao uchwara.
  ukishapata elimu yako kama phd au masters wanaanza kukunyanyaapa
  mm ni mhanga wa hili. serikali yetu inaajali wataalamu wa nje na kutuacha sisi wazalendo
  sijui ni majungu au ni kuwakumbatia kwa vile wana ngozi nyeupe au english. kwa huyu waziri profesa nampa hongera, wengine waige.
   
Loading...