Hongera Prof. Kabudi kwa umahiri wa kusoma kwa kufuata vituo kwa usahihi

Ni kweli, jamaa ni mzuri sana wa kusoma na kutamka na pia kuandika. Alipokuwa UDSM alikuwa ndio MC wa events kubwa kubwa zenye ugeni mzito pale chuo. Pia matangazo ya chuo yalikuwa yanapita kwake kwa uhariri kabla hayajaenda katika public
 
Ni kweli ana sauti ya ki-mamlaka.Uwezo wake wa kuongea ni wa juu sana.ndiyo maana marehemu alipa hiyo wizara.

Ila sina uhakika na utandaji wake wa kazi.sababu kusemasema ni kitu kimoja na utendaji kazi wenye matokeo ni kitu kingine.Nimejifunza kwa Husein Mwinyi wa Zenji.sauti yake ni ya chini sana ila matokeo yake ni makubwa sana.
Mwinyi amefanya nini?
 
Mzee wa mia kenda
Hawezi kuonesha kuwa tukio au mahali anapotoa sauti ni pa kufurahisha au kuhuzunisha. Ni kasoro kubwa . Anafoka au anatamka kimamlaka mahali pote. Sikutarajia kwenye wasifu wa msiba wa mtu wake asioneshe hata tone ya huzuni.
 
[QUOTE="M-mbabe, post: 38448066, member: 19553"hongera japo unapenda sifa
My 5-year kid can do it mbona. Tena in English!
[/QUOTE]
 
Jamani hakuna aliyekamilika ila sifa ya MTU apewe akiwa hai aisikie. Profesa Palamagamba Aidani Kabudi anajua kutamka matamshi ya lugha sana, kusoma kwa kufuata vituo zile nukta, mkato, koma, funga na fungu semi na alama nyingine akipewa paragraph akusomee sio siri utafurahia sana aina ya usomaji wake. Ana sauti ya kimamlaka sana.

Hongera hapa lazima watakumbushia ile ya kutolewa jalalani ila tukumbuke. Hakuna mkamilifu chini ya jua.....

Hatukujua kuwa aliokotwa jalalani; ni yeye mwenyewe ndio aliyetuambia kuwa aliokotwa na marehemu huko iDodoma jalalani!!
 
Kabudi yuko vizuri ukiachana na vidosari vyake viwili vitatu kama kutumbua macho na kujitoa ufahamu ili kumfurahisha marehemu jiwe
 
Mtu aliyekuwa vizuri KAMWE hawezi kusema aliokotwa jalalani. Mtu asiyejithamini lazima ana walakini mkubwa.
Kabudi yuko vizuri ukiachana na vidosari vyake viwili vitatu kama kutumbua macho na kujitoa ufahamu ili kumfurahisha marehemu jiwe
 
Back
Top Bottom