Hongera Pride FM Mtwara

Dingswayo

JF-Expert Member
May 26, 2009
4,019
2,923
Nimekuwa nikisikiliza Pride FM ya Mtwara kupitia internet, kusema kweli nimefurahishwa na ubora wa vipindi vyao pamoja na umahiri wa watangazaji wao. Nawapa sana hongera na nawaomba wazidi kudumisha ubora huo na wawe mfano wa kuigwa.
 
Declare ur interest kwanza

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hiyo radio nimetokea kuipenda sana tofauti la leo nyingine ..maneno mengi na matangazo kibao,na kuna ile nyingine ya Iringa siyo mbaya sana nayo pia.
 
Declare ur interest kwanza

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Sina interest yoyote Mkuu. Naongea kutoka hisia zangu. Mtwara si kwetu ingawa niliishi mkoa huo zaidi ya miaka 30 iliyopita. Nimefurahishwa tu kuwa kwangu mimi redio hii ya Mtwara imezipita zote zile ambazo ninasikiliza.
 
sina interest yoyote mkuu. Naongea kutoka hisia zangu. Mtwara si kwetu ingawa niliishi mkoa huo zaidi ya miaka 30 iliyopita. Nimefurahishwa tu kuwa kwangu mimi redio hii ya mtwara imezipita zote zile ambazo ninasikiliza.

we unaipata ukiwa maeneo gani ya dunia kwa sasa??
 
PrideFM..na Dk MTuli...mtatuzi wa kero za wanachi wa Mtwara, Moto ushwaka....iko pouwa sana ni 87.8FM inapatikana
 
Sina interest yoyote Mkuu. Naongea kutoka hisia zangu. Mtwara si kwetu ingawa niliishi mkoa huo zaidi ya miaka 30 iliyopita. Nimefurahishwa tu kuwa kwangu mimi redio hii ya Mtwara imezipita zote zile ambazo ninasikiliza.
HII redio ni mfano mzuri sana,kumbe ni radio ya mtwara!big up
 
we unaipata ukiwa maeneo gani ya dunia kwa sasa??
Inapatikana pande zote za dunia ambapo kuna mtandao wa internet. Kama ulisoma vizuri post yangu ni kuwa naisikiliza kupitia internet. Natumaini ukiwa na internet utaipata.
 
NIMESIKIA pride fm leo hii,kwamba marehemu Bob Makani akiwa mwanafunzi Makerere University aliichezea Uganda national team katika fainali ya kombe la gossage dhidi ya tanganyika ambapo yeye akiwa centre half,tanganyika ilifungwa katika hiyo final game.Vilevile mhindi wa kwanza kucheza big time soccer tanzania alitwa Bulji kutokea mtwara.
mchezaji chumi kutokea mtwara aliichezea timu ya taifa continuosly for 13 years-sidhani kama kuna mchezaji mwingine aliyeifikia hii feat
 
Nimekuwa nikisikiliza Pride FM ya Mtwara kupitia internet, kusema kweli nimefurahishwa na ubora wa vipindi vyao pamoja na umahiri wa watangazaji wao. Nawapa sana hongera na nawaomba wazidi kudumisha ubora huo na wawe mfano wa kuigwa.

Kwa kweli hawa jamaa wako fit sana yaani ni mfano wa kuigwa hapa nchini. Sikutegemea kama nitakuja kusikiliza radio bora toka mikoani zaidi ya Dar Es Salaam. Kwa uhakika hawa jamaa wanawashinda Clouds, Radio 1, na nyingi tu za hapa Dar Es Salaam. Mmiliki wao inabidi awaongezee mshahara watangazaji wake la sivyo watachukuliwa na hizi radio za kipuuzi za hapa mjini kiingereza kibovu kiiiingi wakati wakati asilimia kubwa ya wasikilizaji wao ni waswahili, wanakera sana.
 
Back
Top Bottom