Hongera Polisi kitengo cha Trafik Mikoa ya Mbeya na Songwe kwa kuwafanya madereva watii sheria

tramadol

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
5,383
4,317
Hongera sana kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya na Songwe kwa kuwafanya madreva wote kutii na kufuata alama za barabarani aiseeeee.....Huwezi amini kama kweli hapa ni Tanzania kwa jinsi tunavyoona Dar es salaam na mikoa mingine.

Kitu ambacho nakiona ni kitendo cha madreva wote wa magari madogo na makubwa kusimama katika eneo lenye alama ya kivuko cha miguu hata kama hakuna anayevuka kwa wakati huo.Dreva anasimama kama sekunde 2 au 3 then anaendelea na safari yake.

Hakika kwa hilo nawapongeza sana trafic wa hiyo miko miwili kwa kuwafanya madreva kutii sheria bila shuruti.

Mikoa mingine waige mfano huu aisee hakika INAPENDEZA SANA.
 
Ni ushamba na ujinga uliopitiliza, foleni Mbeya imesababishwa na ujinga huu wa trafic. Yaani eti gari ya mbele yako imesimama dakika mbili, ikipita tu zebra na wewe wa nyuma unasimama dakika mbili haijalishi kuna kuna wavukaji au la. Yaani hata kama mlikuwa msafara wa gari kumi , kila gari kwa wakati wake itasimama kwenye zebra. Polisi wanajificha mita mia mbele ya zebra kuangalia nani kapita bila kusimama.
 
siyo dakika mbili ni sekunde 2 au 3
 
Sekunde 2 hadi 3 hapo unaona ni muda mrefu je akienda kule Dar si atasimama Wiki mbili Tazara.
 
Atakuwa katumwa huyu kupima upepo waone response ya uchangiaji
 
Wala Mimi simlaumu maana kuna watu akinunua kitu, wasio nacho wote hawana akili. Huyu Gari imempa dharau kwa watu kiasi kwamba anaamini ana akili kuliko wengine.
 
Hongera sana kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya na Songwe kwa kuwafanya madreva wote kutii na kufuata alama za barabarani aiseeeee.....Huwezi amini kama kweli hapa ni Tanzania kwa jinsi tunavyoona Dar es salaam na mikoa mingine.

Kitu ambacho nakiona ni kitendo cha madreva wote wa magari madogo na makubwa kusimama katika eneo lenye alama ya kivuko cha miguu hata kama hakuna anayevuka kwa wakati huo.Dreva anasimama kama sekunde 2 au 3 then anaendelea na safari yake.

Hakika kwa hilo nawapongeza sana trafic wa hiyo miko miwili kwa kuwafanya madreva kutii sheria bila shuruti.

Mikoa mingine waige mfano huu aisee hakika INAPENDEZA SANA.

siyo dakika mbili ni sekunde 2 au 3

Ni ushamba na ujinga uliopitiliza, foleni Mbeya imesababishwa na ujinga huu wa trafic. Yaani eti gari ya mbele yako imesimama dakika mbili, ikipita tu zebra na wewe wa nyuma unasimama dakika mbili haijalishi kuna kuna wavukaji au la. Yaani hata kama mlikuwa msafara wa gari kumi , kila gari kwa wakati wake itasimama kwenye zebra. Polisi wanajificha mita mia mbele ya zebra kuangalia nani kapita bila kusimama.
 
Ni ushamba na ujinga uliopitiliza, foleni Mbeya imesababishwa na ujinga huu wa trafic. Yaani eti gari ya mbele yako imesimama dakika mbili, ikipita tu zebra na wewe wa nyuma unasimama dakika mbili haijalishi kuna kuna wavukaji au la. Yaani hata kama mlikuwa msafara wa gari kumi , kila gari kwa wakati wake itasimama kwenye zebra. Polisi wanajificha mita mia mbele ya zebra kuangalia nani kapita bila kusimama.
Kwa madereva wenu hao wa kibongo, acha iwe hivyo hivyo tu. Tofauti na hapo ni majanga.
 
Nikuulize wewe. We are living in the modern world where we have no time to waste. Time is a factor of production.
Muda ni rasilimali pekee ambayo ukiipoteza huwezi kuipata tena
Labda tumewahi sana kumiliki na kitumia magari kabla hatuja staarabika. Acha hali iendelee kudhubitiwa hivyo hivyo
 
Hongera sana kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya na Songwe kwa kuwafanya madreva wote kutii na kufuata alama za barabarani aiseeeee.....Huwezi amini kama kweli hapa ni Tanzania kwa jinsi tunavyoona Dar es salaam na mikoa mingine.

Kitu ambacho nakiona ni kitendo cha madreva wote wa magari madogo na makubwa kusimama katika eneo lenye alama ya kivuko cha miguu hata kama hakuna anayevuka kwa wakati huo.Dreva anasimama kama sekunde 2 au 3 then anaendelea na safari yake.

Hakika kwa hilo nawapongeza sana trafic wa hiyo miko miwili kwa kuwafanya madreva kutii sheria bila shuruti.

Mikoa mingine waige mfano huu aisee hakika INAPENDEZA SANA.
Kweli naunga mkono hawa askari wa usalama barabarani wamewanyosha sana madereva nadhani ni mkoa wa Mbeya pekee yake hapa Tanzania ambao alama za barabarani kama zebra zinaheshimiwa hata kama hakuna mtu wa kuvuka kwenye zebra gari lazima lisimame kwa muda halafu ndio liendelee,pia kwenye maeneo ya watu lazima gari liende kwa mwendo unaotakiwa kama vile 50 kmh,Hongereni sana askari wetu wa usalama barabarani mkoani Mbeya
 
Hakika kweli wanastahili pongezi sana hawa jamaa wa Trafic wa Mbeya na Songwe mpaka madreva wa tz na nchi jirani wakitii zebra cross kwa kusimama wenyewe
 
Still ni ushamba Na usumbufu, waweke vivuko vya madaraja
ndivyo sheria ya usalama barabarani inavyomtaka dereva afanye....usijione wewe Dar kutosimama zebra cross basi ndiyo mjanja sana ni basi tu trafic wako hawajaamua kusimamia sheria hiyo ktk vipengele vyote jinsi inavyopaswa
 
ila tuwe na ukweli, waenda kwa miguu ndio wanapaswa heshimu hizo zebra, wasubirie gari zipite na wao wapite
 
kila mtumia barabara anatakiwa kuheshimu alama za barabarani sheria haisemi mtembea kwa miguu ndiyo anatakiwa kuheshimu zebra cross bali mtembea kwa miguu na dreva pia
 
ndivyo sheria ya usalama barabarani inavyomtaka dereva afanye....usijione wewe Dar kutosimama zebra cross basi ndiyo mjanja sana ni basi tu trafic wako hawajaamua kusimamia sheria hiyo ktk vipengele vyote jinsi inavyopaswa
naona sasa madereva wengi wameanza kutii hiyo sheria hata hapa Dar kwasasa naona zebra cross wanasimama tofauti sana na ilivyokuwa zamanai.nakumbuka siku moja pale magomeni usalama nilishuhudia mama na mtoto wake wakigongwa na landruiser eneo la zebra cross ilikuwa ajali mbaya sana na wote waaga dunia on the spot
 
Back
Top Bottom