Hongera Pinda lakini isiishie kwa wabunge peke yao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera Pinda lakini isiishie kwa wabunge peke yao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Albedo, Jun 17, 2011.

 1. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Jana mimi ( Mwalimu) pamoja na Watanzania wengi ( Wauguzi, Madaktari na hata makondakta) Tulikuwa Mbele ya Runinga zetu tukifuatilia Mjadala wa bunge la bajeti linaloendela hivi sasa. Kilikuwa ni kipindi cha Maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu Mh. Mizengo Kayanza Pinda ( Wengi hupenda kumuita Mtoto wa Mkulima ni kweli yeye ni motto wa Mkulima lakini yeye si MKULIMA). Akiwa ametulia kabisa akiwa na Lengo la kujustify Posho za wabunge mbele za macho ya Watanzania maskini wasio hata na uhakika wa Mlo wa siku waliokuwa wakimsikiliza kwa masikio ya Matumaini, mh Pinda alisema

  Ni Maneno hayo ndiyo yaliyotusukuma sisi Kuja na mapendekezo yafuatayo ambayo kama Yatatekelezwa "Kwa Nia Njema" basi Maisha yatakuwa tambarare

  1. Sisi Madaktari

  Mara nyingi tumekuwa tukitoa Pesa zetu mfukoni kuwasaidia wagonjwa ambao wameshindwa kujinunulia dawa tumekuwa tukifanya hivyo kwa kutumia kamshahara ketu kadogo Ombi kwako Mizengo. Na sisi tunaomba Serikali Ituwekee Posho ya Mdaktari ili Tuweze kuwasaidia wale wagonjwa tunaowaandikia dawa lakini wanakosa Pesa za Kununua dawa hizi. Kwa Kufanya hivyo tutaokoa Nguvu kazi kubwa kwani Mshahara wetu hautoshi kuwasaidia wagonjwa wote. Sisi tunaomba posho ya Madaktari iwe 50,000 tu kwa siku

  2. Sisi walimu

  Sisi tumekuwa tukiwafukuza wanafunzi warudi Nyumbani kwa sababu ya Kukosa Ada na michango mingine, na mara nyingine wanafunzi hawa wameshindwa kufanya mitihani yao ya Mwishi kwa kukosa Ada ya Mtihani. Tunafanya tukiumia lakini hatuna uwezo maana mshahara wetu ni Mdogo. Lakini Tumefarijika na Hotuba yako na tumepata matumaini kwamba Kumbe suala Hilo linawaeza kumalizwa Kwa kuanzishwa Kwa POSHO ya WALIMU. Mheshimiwa Waziri mkuu Ukituwezesha POSHO ya UALIMU ya Shilingi 50,000 tu kwa siku Hautakaa usikie mwanafunzi amefukuzwa kwa kukosa Ada na Michango mingine Kandamizi.

  3. Sisi Wauguzi

  Akina mama wengi wajawazito wamekufa Mikononi mwetu kutokana na Ukosefu wa vifaa salama vya Kujifungulia. Tumekuwa tukitukanwa na kusemwa sana juu ya Vifo vya akina Mama hawa wapendwa wa Tanzania. Mheshimiwa Waziri Mkuu kama tungekuwa na Uwezo tungewasaidia Wajawazito hawa hata kuwanunulia vifaa vya Kujifungulia ( Hakika wamama wengi wanaokufa ni MASKINI, WAKULIMA na WASIOJIWEZA). Nasi tunapenda kukuomba Mheshimiwa Waziri mkuu Atuanzishie POSHO YA WAUGUZI. Mheshimiwa tunakuhakikishia ukituanzishia kaposho ka 30,000 kwa Siku habari ya Wajawazito kufariki kwa kukosa Huduma bora hautaisikia tena  Mheshimiwa waziri Mkuu haya ni Mawazo yetu sisi Madakatari, walimu na wauguzi. Najua muda si mrefu utaanza kupokea maombi kama yetu kutoka Kwa makundi mengine ya Kijamii kama Mahakimu, Polisi na wengine

  Kwa leo ni hayo tu Mheshimiwa Rafiki yangu waziri Mkuu Mizengo Kayanza Peter Pinda
   
 2. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mbombo ngafu fijo
  na sisi tunasema POMBOMBO RWELI!
  unajua mkuu mimi naona bora hata JK kuliko hiii mutu mnayoita mtoto wa mkulima LINAFIKI TUU!
   
 3. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Unampongeza kwa lipi mbona hueleweki?
  Cdm wanapozikataa posho ili ziingie kwenye gvt fund haziwasaidi wananch?
  usiwe mbumbumbu posho ni zaidi ya tirion moja na hapo ni sawa na raia kupata matibabu bure na hao
  Dr,walimu,wauguzu kulipwa mara tatu mishahara yao ya sasa we vipi?
   
 4. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  You Must be a REAL GREAT THINKER KUELEWA MAANA
   
 5. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #5
  Jun 17, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  pompo kichwa yako hainasi nini kamanda.
  mbona jamaa anaeleweka tu?
   
 6. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #6
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,381
  Likes Received: 3,341
  Trophy Points: 280
  Na sisi wapiga lager huwa kuna watu wanatuomba tuwanunulie bia na unakuta mtu una change kamili ya bia moja. Tunaomba kaposho ka sh 9,000 tu kwa siku. Tutaweza kupiga bia zetu kama nne na kuwanunuia wasiona kitu bia 2. Asante mh. punda kama utatusaidia kwa hilo.
   
 7. e

  ejogo JF-Expert Member

  #7
  Jun 17, 2011
  Joined: Dec 19, 2009
  Messages: 994
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkuu Albedo, unajua atawajibuje hao walimu, wauguzi, nk. atasema hao wote wawakilishi wao ndio wabunge. imenishangaza sana kuona kiranja mkuu anatetea posho kwa point ya kuwa wabunge huwa wanawasaidia wananch nauli. Hivi wakituwekea mazingira mazuri ya kiuchumi kuna mtu atakwenda kuomba nauli!! Kwanini hiyo pesa wanayopewa posho isiende kuboresha mazingira yetu ya kiuchumi ili tuwe tunavua wenyewe samaki badala ya kila siku kwenda kupanga foreni kuomba tupewe samaki!!
   
 8. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #8
  Jun 17, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Nasikia Posho kwa Ajili ya Dereva wa Mbunge ni 450,000 TSh hivi kuna Utaratibu gani wa kibunge kuhakikisha kwamba huyu Dereva anapata hiyo Stahiki yake? Nani anapeleka michango ya NSSF kwa hawa madereva? Hii ni Dhambi kubwa ambayo jana Pinda alikuwa anaipigia makofi
   
 9. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #9
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Kuna rafiki yangu anasoma TIA Arusha yupo Dodoma tangu juzi amemfuata mbunge wake lakini tangu amefika hadi sasa hivi hajafanikiwa kumwona na Mbunge anayo taarifa kuwa yuppo mtu ana siku 2 Dodoma anamtafuta. Naona Machale yashamcheza kuwa jamaa kaenda kuomba wagawane posho ameamua kumiga chenga ya mwili
   
 10. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #10
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  pinda....
  posho na sie watembea kwa miguu, tukipita mitaani tukakutana na ombaomba tuwagawie kidogo....10, 000 kwa siku itatosha.
   
 11. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #11
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  big up Albedo

  Nawaunga mkono wote-waalimu, madaktari na wauguzi. Hii ni kwa mujibu wa dhana mpya ya POSHO aliyotupa PINDA jana kuwa tunakupa posho ili zikusaidie kuwasaidia watu wengine.

  utetezi mwingine unawafanya watu wakudharu- it is too cheap
   
 12. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #12
  Jun 17, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,536
  Trophy Points: 280
  muhemishiwa kiranja mkuu, na sisi makondokta wa daladala na vifodi tunaomba posho ya makondakta; maana wakati mwingine abiria (hususani wanafunzi na vikongwe) wanapanda bila nauli hivyo inabidi tufidie ili kukamilisha hesabu za tajiri!!
   
 13. N

  Ntandalilo Member

  #13
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante mkuu!
   
 14. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #14
  Jun 17, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Wafanyakazi wote na tuandamane kudai posho zetu tunapokuwa tunafanya kazi zetu kama wabunge wanavyolipwa posho kwa kufanya kazi zao.
   
 15. samito

  samito JF-Expert Member

  #15
  Jun 17, 2011
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 621
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa hiyo Pinda ametoa mwongozo kwa wananchi wakiwa na shida ya vijihela wakawaone wabunge wao esp wakiwa kule dodoma! PINDA bwana sijui ni uzee au? lakini naamini wazee ndo wenyebusara zaid sasa sijui jamaa ana nini? anatuona watoto!
   
 16. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #16
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  kazi unayo, kaka
   
 17. N

  Njaare JF-Expert Member

  #17
  Jun 17, 2011
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hivi wakati anajibu hilo swali Pinda alijua kuwa anaonekana na wananchi kwenye TV? Kama alijua basi hii ndo waswahili wanasema ni kulewa madaraka au jeuri ya kifisadi
   
 18. T

  Tekenya Member

  #18
  Jun 17, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  teh teh teh!!!!! jaman mbavu zangu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!???????????????
  mwanzisha mada hii nimemkubali, inauma sana. Maelezo ya pinda kuitetea posho hayakubaliki hata kidogo. Kama posho wanapewa wabunge kusaidia watu wao sioni sababu wapewe wao, zipelekwe kwa wananchi,
  la sivyo wananchi tujitokeze na sisi tudai posho.

  IKO WAPI POSHO YANGU MIMI MKULIMA NINAEUMIA NA JEMBE LA MKONO KILA SIKU BILA UHAKIKA WA MAVUNO JAMANI? MBONA SIKIA KILIO CHANGU MIM MKULIMA.
   
 19. A

  Ame JF-Expert Member

  #19
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Mkuu Albedo respect my bro! Kwakweli nilimsikiliza waziri mkuu nikasogeza tena sikio langu kwa umakini zaidi I could not figure out alichokuwa anakiongea hasa ukizingatia yeye ndiye mtendaji mkuu wa serikali. Niliogopa sana nakuhisi vibaya mno. How can he say such a thing? Yaani waziri mkuu ana justify utumiaji wa kodi ya wananchi kwa private issues badala ya kusisitiza building of institutions? Inamaana serikali imeona bora iwape wabunge kodi zetu wakagawe kwa wale ambao watabahatika kukutana nao njiani ku solve private problem zao? Yaani serikali ya CCM imefikia this stage ya kuamua kuua institutions na kuamua kwa facilitate individuals ku solve household issues? Kwahiyo badala ya kuwezesha shule, hospitali, barbara, na public goods zingine ni bora wabunge wapewe cash ili wa solve problems za individuals at household level? Ni huzuni sana kusikia kutoka kwa mheshimiwa mtendaji mkuu wa serikali kuwa kodi kazi yake siku hizi siyo kuboresha tena social services bali kuhudumia individuals at household level kwa matatizo yao binafsi. Yaani kuondoa execution ya serikali kutoka kwenye taasis mpaka kwa individuals (wabunge) in terms of cash kama njia ya kuwatuliza wale wasumbufu wachache wasioona aibu ya kuomba na kwaacha wengi wenye soni wakifa na tai shingoni wakati shida hizo huwapata jamii nzima ya watanzania.

  To be frank tafsiri yangu binafsi ni kuwa ufisadi ni one of the institution ya serikali ya CCM na hii imethibitishwa rasmi na serikali yake maana wamekiri wanawapa wabunge posho ili waweze kuwa facilitate waweze kuwapa pipi wapiga kura wao ili wasijekosa kuwapa kura kwakushindwa kutatua matatizo yao kwakuja na mawazo mapya ya jinsi ya kujenga mifumo imara ya kijamii ambayo itasaidia wananchi kujiletea maendeleo yao badala ya kuhongwa kwa pesa ndogo ndogo za kununulia sabuni vibaba vya unga na nauli za kuwafikisha hospitali zisizo na dawa wala madaktari wakutosha. Ni dharau na tusi kubwa kwa baba, kaka, dada, shangazi, wajomba zangu na ndugu zangu wengine watanzania kuambiwa eti kodi zetu zitasaidia watu mmoja moja atakayeenda kumwomba mheshimiwa mbunge (pamoja na kuwa sisi ndiyo maboss wao) msaada kama hivyo ndivyo si waaache kukusanya kodi ili sisi tujiendeshee shughuli zetu bila wao? Kunahaja gani ya sisi kutoa kodi alafu turudi tena kuomba kodi hiyo hiyo kwa shida zetu za kibinafsi badala ya kujenga huduma za kijamii ambazo tunazihitaji ili tusidhalilike kiasi hiki? Nikutudhalilisha kutudharau na kutotambua kuwa sisi tumewaajiri ili watusaidie kujenga mifumo ya kijamii itakayo hudumia jamii kwa ujumla na siyo kuwapa wao cash ili sisi tuwe omba omba na kutegemea huruma yao kututatulia shida zetu za kijamii.
   
 20. T

  Tekenya Member

  #20
  Jun 17, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wala sio hivyo, ni kwamba yeye wala hataomba tena kura kwa wananchi, umesahau alisema ndo mda wake wa mwisho?
   
Loading...