Hongera Paul Makonda kujiuzulu uenyekiti tahliso | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera Paul Makonda kujiuzulu uenyekiti tahliso

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by thatha, Oct 1, 2012.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  MIMI PAUL MAKONDA napenda kuwashukuru kwa dhati viongozi wote wa Vyuo Vikuu/Taasisi za elimu ya juu nchini kwa kuniamini na kunichagua kuwa Mwenyekiti wa “TAHLISO” mnamo 27 Septemba, 2011 mpaka hivi leo ambapo natangaza rasmi kukasimisha nafasi yangu ya Mwenyekiti kwa Makamu Mwenyekiti wa “TAHLISO” Taifa Ndugu AHMED ABUBAKARY MOHAMED kukaimu nafasi hiyo kwa kipindi hiki.Nawashukuru viongozi wote
  ,Wizara,Wakurugenzi na Viongozi wote na wadau wa elimu ya juu nchini kwa ushirikiano mkubwa walionipa kipindi chote cha uongozi wangu wa “TAHLISO”

  3.0 DHAMIRA.
  Nimeamua kufanya hivyo ili kutenganisha kofia mbili za uongozi kwa wakati mmoja “TAHLISO na siasa za vyama vya siasa (UVCCM) na kuzuia mgongano wa maslahi ya kisiasa dhidi ya TAHLISO kwani TAHLISO ni Umoja wa Serikali za Wanafunzi Tanzania ulio huru usioingiliwa au jihusisha na chama chochote cha siasa nchini.Hivyo kujenga imani,mshikamano,utulivu na amani kwa wadau wote kama ambavyo tumekuwa tukishirikiana katika kipindi chote.

  HITIMISHO.
  Nawashukuru tena kwa dhati wote mlio hudhuria mkutano huu na kuwaomba tushirikiane kwa pamoja kuijenga nchi na kutanguliza maslahi ya Taifa mbele.

  “MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA.”

  PAUL MAKONDA

  My take;Ni viongozi wachache wanaoweza kuthubutu kuachia madaraka kwa hiari yao.makonda ameonyesha njia.
   
 2. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  sasa tufanye nini hapa?
   
 3. t

  thatha JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Jifunze kuacha tamaa ya kulimbikiza madaraka.ukipata nafasi moja acha nyingine ili watanzania wengine nao waonyeshe uwezo wao.
   
 4. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  UVCCM na TAHLISO ni wapi na wapi?
   
 5. t

  thatha JF-Expert Member

  #5
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Huku ndio kukua na kupanuka kwa demokrasia. utaifa kwanza.
   
 6. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #6
  Oct 1, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Kwa hili, Höngera Ndg Makonda.
   
 7. C

  Curriculum Specialist JF-Expert Member

  #7
  Oct 1, 2012
  Joined: Oct 8, 2007
  Messages: 2,736
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Katiba ya TAHLISO hairuhusu Kiongozi kukaimisha au kukasimisha! Alipaswa ajihudhuru nafasi yake kukaimisha ili akikosa anachotaka arudie madaraka yake kirahisi ni ufusadi mwingine!
   
 8. K

  Kanundu JF-Expert Member

  #8
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 891
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  WAKUU!

  Labda kama kiswahili changu si kibovu. Hivi neno KUKASIMISHA kama linaeleweka vizuri ni kwamba bado nafasi hiyo ni yake hivyo akishindwa huko anakogombea atarudi kuendelea na cheo chaka. Kama ndivyo sioni cha kushangilia hapo.

  Hivi hizi digrii za siku hizi zikoje wakuu?????
   
 9. v

  valid statement JF-Expert Member

  #9
  Oct 1, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Digrii gani hasa,maana zipo nyingi...
   
 10. m

  mkatangara Member

  #10
  Oct 1, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyo Tusiuane ni kuwadi wa huyo Makonda hawezi kusifia kitu ambacho ni uongo,
  Huyo makonda hajajiuzuru TAHILISO na kwamba amekaimisha nafasi hiyo na yeye kwenda kugombea umakamu mwenyekiti uvccm na kwamba akishindwa anarudi kuendelea na nafasi yake.
  Huu ni undumilakuwili na jamaa anajionyesha jinsi alivyo mroho wa madaraka, kwanza hafai kuwa kiongozi Tahiliso hata huko uvccm.
   
 11. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #11
  Oct 1, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mpaka watu wapige nduruuuu ndiyo Uachie madaraka?
   
Loading...