Hongera NECTA kwa kusambaratisha wizi wa mitihani Wilaya ya Kilindi

Hofu-less

JF-Expert Member
May 19, 2014
520
1,031
Hakuna jambo baya kama wizi wa mitihani kwani hupelekea kupata mabosi Vilaza na kutuletea tabu kwenye taifa.

Wilaya ya Kilindi ilikua ni mojawapo ya Ngome za uvujaji wa mitihani , ilifikia hatua mpaka mitihani ya MOCK ilisoviwa, wadau mbali mbali walipigia kelele suala hili Mimi binafsi nilitaja mpaka shule kupitia nyuzi mbali mbali humu.

Pamoja na kutishiwa maisha na vigogo lakini pia sikupewa zawadi yoyote!

Jambo la pekee nilifurahi kuona utopolo huu ukifika mwisho na sasa angalau kuna afadhali japo kuna shule chache ambazo nitazitaja kwenye uzi ujao bado hazijaacha.

Hongera Necta endeleeni kukataza na kukomesha
 
Hivi sasa ivi mtu unaakili zako timamu unaenda kuiba hii mithani ya necta ili iweje? Iyo pesa ya kuibia mwanao mtihani si bora umfungulie mashine ya kusaga maihindi.

Siku hizi ukiona mwanao kafaili mtihani hii ya sasa hata usijisumbue naye kabisa. Uyo ni wa kumtaftia alternative nyingine ya maisha kabla hajakuozea.
 
Hongera necta kuzuia wizi, hapa 96% mmeweza.

Kifuatacho ongezeni posho ya wasimamizi.
 
Hivi sasa ivi mtu unaakili zako timamu unaenda kuiba hii mithani ya necta ili iweje? Iyo pesa ya kuibia mwanao mtihani si bora umfungulie mashine ya kusaga maihindi.

Siku hizi ukiona mwanao kafaili mtihani hii ya sasa hata usijisumbue naye kabisa. Uyo ni wa kumtaftia alternative nyingine ya maisha kabla hajakuozea.
Uko sahihi kuwa siku hizi watoto wanalazimishwa kufaulu ili kujaribu kung'arisha awamu ya 5, ila mitihani hawaibi wazazi na kuwapa watoto wao ispokuwa baadhi ya shule ndio wanachukua mitihani kwa njama na necta ili kuongeza ufaulu kwenye shule zao na kujitangaza kibiashara ili wapate fame na kupata wanafunzi wengi
 
Hamieni Tarime nako wizi wa mitihani unaratibiwa kutokea halimashauri kwa wasimamizi kupangwa na kupewa maagizo maalum
 
Back
Top Bottom