Msigazi Mkulu
JF-Expert Member
- Dec 22, 2013
- 4,110
- 3,269
Nawapongeza sana Baraza la Mitihani Taifa kwa kuanza kudhibiti wizi wa mitihani hasa mitihani ya taifa ya darasa la saba na la nne.
Kwa kuanza mwaka huu naona mmewateua walimu wa shule za sekondari kusimamia mitihani hiyo maana ndo waanga wa wizi wa mitihani kwa kuletewa wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika.
Hivyo basi naendelea kuwashauri kama kweli mmedhamilia kuondoa tatizo hilo muendelee kupandikiza ma informer ili hatuanza haraka zichukuliwe kwa walimu wakuu watakaotaka kurubuni wasimamizi ili kuvujisha mitihani na hatimae wanafunzi kupewa majibu. Hii imeshakuwa desturi kwa shule zote za msingi binafsi na serikali kufanya juu chini mitihani kuvujishwa na bajeti upangwa kabisa ili viongozinwa elimu kupata sifa. Msipofanya hivyo mitihani itaendelea kuvujishwa tu maana hata walimu wa sekondari wana njaa ya pesa pia.
Ushauri kwa walimu wa sekondari walioteuliwa, huu ndo wakati wa kuprove kwamba mpo vizuri kwa kufanya kazi kwa uhaminifu. Ndo wakati wa kuona matokeo halisi sio sinema ambazo tumezoea kila mwaka. Mkiharibu na nyie sasa taifa litaangamia kwa kuzalisha wataalamu wasiokuwa na sifa. Vilevile mtapeleka tabia hii ya kuiba mitihani ngazi ya sekondari ambapo haikuwepo kwa kiasi kikubwa, kwa ngazi ya sekondari wizi umezoeleka katika shule binafsi tofauti na ngazi ya msingi ambapo wizi unafanyika shule binafsi na za serikalini na bila kificho.
Mwisho nashauri baraza la mitihani Taifa kuweka maafisa mitihani kila ngazi ya wilaya ili wawe ndo waratibu wakuu wa shughuli za mitihani sio kuwaachia maafisa elimu na walimu wakuu kusimamia hilo zoezi wakati na wao ndo kipimo chao cha uchapakazi ndo maana wanashiriki kwenye mchakato wa wizi wa mitihani kwa kuwahamasisha na kuwashurutisha walimu wakuu kuhakikisha wanafunzi wote wanafahulu kwa namna yoyote ile. Ikishindikana hilo la kuweka maafisa wa NECTA kuanzia ngazi ya wilaya basi hili zoezi lisimamiwe na ofisi ya udhibiti ubora.