Hongera Nchimbi kwa mchango wako mkubwa katika ushindi wa timu yetu huko Sudan

asiyetabirika

Member
Oct 14, 2019
46
55
Nimeicheki mechi ya Sudan dhidi ya Taifa stars iliyoisha kwa 1-2 nimefurahishwa na kipaji cha huyu mchezaji aliyeongezwa kwenye kikosi cha Taifa stars dakika za mwishoni kutokana na uwezo wake aliouonyesha kwa kuifunga YANGA magoli matatu peke yake hali iliyomfanya kocha wa timu ya taifa kumuona huyu kijana na kumuingiza kikosini dakika za mwisho

Leo nimeuona mchango wake kwenye kufanya vizuri Taifa stars huko sudani, magoli yote kwa sehemu kubwa yameanzia kwake, goli la kwanza yeye alifanyiwa faulo iliyopelekea mpira wa adhabu kwenda golini ilipigwa na nyoni na akafunga bao la kwanza, lakini goli la pili ni kafunga yeye mwenye Nchimbi.

Hongera sana Nchimbi, hongera taifa stars kwa kufanya vizuri mchezo wa leo.
 
Jamaa ana akili ya mpira na pia ana nguvu.
Ameonyesha kuwa Kocha hakukosea kumuita.
 
Nimeicheki mechi ya Sudan dhidi ya Taifa stars iliyoisha kwa 1-2 nimefurahishwa na kipaji cha huyu mchezaji aliyeongezwa kwenye kikosi cha Taifa stars dakika za mwishoni kutokana na uwezo wake aliouonyesha kwa kuifunga YANGA magoli matatu peke yake hali iliyomfanya kocha wa timu ya taifa kumuona huyu kijana na kumuingiza kikosini dakika za mwisho

Leo nimeuona mchango wake kwenye kufanya vizuri Taifa stars huko sudani, magoli yote kwa sehemu kubwa yameanzia kwake, goli la kwanza yeye alifanyiwa faulo iliyopelekea mpira wa adhabu kwenda golini ilipigwa na nyoni na akafunga bao la kwanza, lakini goli la pili ni kafunga yeye mwenye Nchimbi.

Hongera sana Nchimbi, hongera taifa stars kwa kufanya vizuri mchezo wa leo.
Hakuna shaka na uwezo wa Nchimbi isipokuwa namna alivyoitwa.Nchimbi kacheza ligi kuu misimu zaidi ya mmoja hakuna aliyewahi kuonesha kuvutiwa na uwezo wake,Nchimbi kacheza timu zaidi ya moja bado hawakumuona wakamuona mechi moja tu ya Yanga,hapo ndipo unajiuliza wachezaji wetu wa timu ya taifa wanapatikana kivipi?Je,ndo maana timu imejaa wachezaji wa Dar wengi?Ni akina Nchimbi wangapi hawajafutwa hadi waje shamba la bibi ama kwa mchina?
 
Pongezi kwa Timu nzima ya Taifa na bench la ufundi.Huyu kijana Nchimbi ana sifa zote za No.9 ana nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye CHAN huko Cameroun na anaweza kuonwa na Mawakala.
 
Hakuna shaka na uwezo wa Nchimbi isipokuwa namna alivyoitwa.Nchimbi kacheza ligi kuu misimu zaidi ya mmoja hakuna aliyewahi kuonesha kuvutiwa na uwezo wake,Nchimbi kacheza timu zaidi ya moja bado hawakumuona wakamuona mechi moja tu ya Yanga,hapo ndipo unajiuliza wachezaji wetu wa timu ya taifa wanapatikana kivipi?Je,ndo maana timu imejaa wachezaji wa Dar wengi?Ni akina Nchimbi wangapi hawajafutwa hadi waje shamba la bibi ama kwa mchina?
Tena kabahatika kwa sababu kpcha mpya anataka kujaribu kila mchezaji.
 
Asijekosea enda Simba au Yanga au Azam atapotea kama kina Salamba
 
Tena kabahatika kwa sababu kpcha mpya anataka kujaribu kila mchezaji.
Ni kweli,inabidi uongozi na benchi la ufundi waanze kufanya scouting za maana kila ligi kuu na ligi daraja la kwanza zinazochezwa.Huko Cameroon ,Pierre Njaka aliibuliwa na kocha wa timu ya taifa huko vijijini kama wangemsubiri Younde sijui kama angepatikana.
 
Binafsi namsifu sana Chilunda goli la pili...hakuwa mchoyo kabisa mwingine angepiga golini afunge yeye kwenye impossible angle
 
Back
Top Bottom