Hongera Nape, suala la kukaimu muda mrefu ni tatizo

Standards Person

JF-Expert Member
Apr 22, 2021
673
859
Katika mchango wake bungeni mh. Nape Nnauye ameshauri itungwe sheria inayoweka ukomo wa kukaimu.
Jambo hili nikweli bora litungiwe sheria ili kuboresha mazingira ya utendaji kazi,uwajibikaji na kuondoa viashiria vya rushwa.
Madhara yake yanaonekana Tanga Jiji kwani wapo watumishi waliopewa nafasi za kukaimu kwa muda mrefu. Kundi hilo baadhi yao wamegeuka genge la kutishia usalama wa watumishi ambao wamekua tofauti kimtazamo na mkurugenzi wa Jiji hususan kwenye suala la wizi wa mali ya umma.

Wapo tayari mtumishi hata apoteze maisha lakini walinde mapungufu ya mkurugenzi ikiwemo rushwa na unyanyasaji. Lengo ni ili wapewe mamlaka kamili. Maonevu ni mengi mno yaliyotokana na watu wanao kaimu na baadhi yao wamekua kama kikundi cha kushuhulikia watu na mara nyingi hawakai ofisini. Ofisi ya RC,RAS,DC wanajua hilo lakini hawana ubavu wa kumwambia mkurugenzi chochote

Habari za mkurugenzi huyo hazikushuhulikiwa nRC na RAS aliyekuepo. Matokeo yake Jiji limekua likiongozwa na mkurugenzi na genge lake la watu wanaokaimu ofisi kwa muda mrefu
 
Sheria na kanuni zake si kila siku huwa wanaziongelea zipo, labda kama waongeze adhabu ya atakayechelewa kuthibitisha afungwe.
 
Back
Top Bottom