Hongera Naibu Waziri wa Maji Mhe. Juma Awesu

pefhana

Senior Member
Mar 26, 2017
158
105
Ndugu zangu hii nchi imejaa mafisadi kila kona. Rais na Waziri Mkuu wanafanya kazi kwa uzalendo mkubwa lakini kuna viongozi mikoani na wilayani wanawaza kupiga hela za miradi mbalimbali. Nimemsikiliza Naibu Waziri wa Maji Mhe. Awesu akiongea kwa uchungu kuhusu hali mbaya ya miundombinu ya maji mkoa wa Ruvuma.

Nimeshtushwa kusikia Ruvuma ilipewa zaidi ya Bilion 15 kwa ajili ya MAJI. Ninaifahamu vizuri Ruvuma na shida kubwa ya maji waliyonayo wananchi licha ya kuwa na vyanzo vingi vya maji vinavyouzunguka na kukatiza mkoa huo.

Kilichonishtua zaidi ni taarifa kuwa wilaya ya Mbinga imepewa zaidi ya Sh Billion 2.1. Kwani ukosefu wa miundombinu inayotoa maji mkoa huo kwa vijinini ni zaidi ya asilimia 85. Hali ni mbaya. Nimetembelea hiyo miradi feki ya kupigia hela wajanja, ule mradi wa Mabuni uliotumia million 239, Litumbandyosi (311 milion) na Kingole (293 milioni). Kwa kweli Naibu Waziri alistahili kutoa machozi.

Huu mkoa hauna viongozi wazalendo. Inaumiza Sana. Kwa mfano mradi wa Kingole haukutakiwa uchimbwe visima kwa kuwa kuna mto mkubwa tena umeanzia milimani na kijiji kipo chini Sana, palitakiwa mradi wa maji ya mtiririko lakini kwa kuwa walijua wangetumia maji ya mtiririko wasingepiga hela ndefu, wakalazimisha wachimbe visima ambavyo vipo mita miambili kutoka mto mkubwa. Inashangaza Sana.

Kwa nini wachimbe visima wakati wangeweza kupeleka pump mpaka mtoni na kupata maji ya mto moja kwa moja? Inaumiza sana. Mafisadi bado yapo na mengine kila uchao yanaomba yateuliwe yagombee ubunge. Kuna haja sasa kama taifa tukubaliane kuyanyonga mafisadi yanayoleta mateso wakati mwingine hadi vifo kwa wanyonge.

Hii nchi imejaa mtandao mkubwa wa mafisadi na majizi. Hivi karibuni kulitokea kikundi cha mafisadi yakapora ardhi ya wananchi wanyonge kwa kuwa Ina Madini NA makaa ya mawe na kujifanya kwamba wao ni maliasili. HAKIKA KAMA MAGUFULI BADO YUPO MADARAKANI UFISADI HUU HAUTAFANIKIWA.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pamoja na pongezi hizo angewasaidia wapiga kura wake wa Pangani kupata barabara ya uhakika kwanza..uzalendo huanzia nyumbani.
 
Back
Top Bottom