Regnatus Cletus
JF-Expert Member
- May 26, 2018
- 1,114
- 958
Ndugu wanabodi,
Salaam!
Nimpongeze ndugu Naibu Waziri wa Elimu, Mheshimiwa WILLIAM OLE NASHA kwa kutoa tamko lenye malengo ya kuendelea kufanya shule kuwa sehemu salama kwa wanafunzi, watoto, na wadogo zetu kupata elimu kwa amani na utulivu wa mwili na akili, ambapo kuanzia sasa NI MARUFUKU KWA WALIMU KUTEMBEA NA BAKORA MAENEO YA SHULE.
Nikushukuru ndugu Naibu Waziri kwa kusikiliza makaripio ya wananchi dhidi ya walimu WASIO NA MAADILI hususani baada ya mauaji ya kikatili ya mtoto Sperius Eradius yaliyofanywa na mwalimu wa nidhamu kwa shutuma batili za wizi wa mkoba.
Marufuku hii isitafsiriwe kama amri za kisiasa, isipokuwa ieleweke kama namna ya kusimamia SHERIA YA UTOAJI WA ADHABU YA VIBOKO, YAANI SHERIA YA ELIMU SURA YA 353 MAREJEO YA 2002, NA CORPORAL PUNISHMENT REGULATIONS G. N 294 2002 ; ZINAZOTAKA ADHABU YA VIBOKO VISIVYOZIDI VINNE ITOLEWE NA MWALIMU MKUU TU, AU MWALIMU MWINGINE KWA RUHUSA YA MWALIMU MKUU, NA SI VINGINEVYO.
Sheria na kanuni za utoaji wa adhabu za viboko zina malengo ya kuwaadabisha wanafunzi kwa kiwango sahihi bila kuongozwa na mihemko na hisia.
Nikiwa kama mdau wa sheria, hasa mtu anayependa kujitoa kupigania haki za watoto, SIPENDEZWI KABISA NA ADHABU YA VIBOKO.
Yangekuwa ni mamlaka yangu ningesisitiza KUFUTWA kwa adhabu za kinyama na kitumwa za viboko, na badala yake, wanafunzi watovu wa nidhamu wapewe adhabu kali za mikono, wasimamishwe masomo, au wafukuzwe shule.
Adhabu ya viboko ni kielelezo cha jamii inayoamini na kuhusudu katika ukatili kama nyenzo ya kuadabishana.
UKATILI DHIDI YA WATOTO NA WANAFUNZI HAUKUBALIKI.
PUMZIKA KWA AMANI MTOTO MWEMA SPERIUS ERADIUS.
Sent using Jamii Forums mobile app