Hongera Mtoi Jiko kujipatia

chama

JF-Expert Member
Aug 6, 2010
8,001
2,418
HONGERA KAKA Mtoi KUPATA JIKO

Nakupa zangu hongera, mapenzi wayakubali
Mtoi nakupa sera, Rehema katoka mbali
Chadema wamejikera; maneno mali kauli
Karibu kwetu Mlalo, harusi wetu kisura

Maneno wayatupia, Rehema kayakubali
Washenga wasafiria , Arusha kuyakabili
Wajitwalia rupia, mahari ya kijabali
Karibu kwetu Mlalo, harusi wetu kisura

Rehema kajipendeza, mithili ya mbega jike
Mtoi katekeleza, kajipa karama zake
Lema kaseleleza, Rehema kampa zake
Karibu kwetu Mlalo, harusi wetu kisura

Rizi ajisemea, harusi yapangiliwa
Mtoi ajiolea, kufuli lapigiliwa
Lema ajikomea, hodi hodi zakataliwa
Karibu kwetu Mlalo, harusi wetu kisura

Chama nafurahia , Mtoi kujitwalia
Lema ajililia, kwa Slaa akimbilia
Rehema kajitulia, mahasidi wala kadhia
Karibu kwetu Mlalo, harusi wetu kisura

Chama
Gongo la mboto DSM

CC Mtoi
 
Nimeipata habari tena ya kusisimua,
Mwanangu kila la heri, jiko umelichukua,
Mola aepushe shari, maisha yawe mulua.
Hongera mwangu moody, kwa jiko kujipatia.

Nakuombea matunda, watoto na wajukuu,
Ndoa nguzo kupenda, mwanangu ninadhukuu
Wako uliyempenda, kila siku sikukuu,
Hongera mwanangu Moody Ndoa kujifungia.

Babako nina furaha, nashindwa kuelezea,
Moyoni naona raha, nazidi sherehekea,
Naomba nyota ya jaha, ndoa yenu naombea,
Hongera mwanangu Moody, Ndoa kujifungia.

Umeuacha uhuni, umeianza safari,
Siingei jaribuni, kaa na utafakari,
Ndoa yako ihami, lewa upendo chakari,
Hongera mwanangu Moody, Ndoa kijufungia.

Natamani ningewini, harusi kuhudhuria,
Nijimwange ukumbini, utenzi kuwaimbia,
Acha nitoe idhini, shairi nakughania,
Hongera mwanangu Moody Ndoa kujifungia.

Kaditamati natua, mbele sitaendelea,
Kalamu nainyatua, nenda kusherehekea,
Nakuombea Mulua, Inshalla yatatimia,
Hongera mwanangu Moody, kuuacha ukapera.
 
Ni kaka mohammed mtoi? Mie namsubiria nje hapo manake kipindi cha kiswahili nilikuwa naenda kuogelea mtoni.
 
Ni kaka mohammed mtoi? Mie namsubiria nje hapo manake kipindi cha kiswahili nilikuwa naenda kuogelea mtoni.

Ndiye yeye hasa kamanda wangu mohamed Mtoi

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom