Hongera mtangazaji Farhia Middle kwa kumbana Hemed Kivuyo

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
20,690
20,445
Nimemfuatilia mtangazaji wa ITV bi. Farhia Middle mara kadhaa, nimeona pale anapokuwa amemaliza kusoma taarifa za habari za michezo amekuwa akiwabana vilivyo watangazaji wenzake wanazi wa vyura kama akina Kivuyo, ambao wamekuwa wakisoma habari za michezo bila kuzingatia uzito wa habari ya mjini kwa siku husika.

Mfano leo, Kivuyo amekomaa na habari za mashabiki wa Liverpool waishio Dodoma, wakati kuna tukio zito nchini la fainali ya Kombe la FA ambalo mshindi wake ataiwakilisha nchi katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Farhia amembana Kivuyo aizungumzie mechi ya leo, ila Kivuyo aliendelea kukwepakwepa lakini Simba ni kama maji, utayaoga usipoyanywa
 
Mara ooh namungo hana uzoefu...!
Sasa mbona mzoefu hakufika fainali.
 
Ila kuna watu MNA moyo!!!!! Mm local chanels nimeshindwa kuzitazama hasa awamu hii ya tano!!yan ni RFA tena BBC swahili tuuuuu!!!
 
Back
Top Bottom