Hongera mkoa wa Singida kutoka nafasi ya mwisho mpaka nafasi ya 14 matokea darasa la saba 2018

MLAU

JF-Expert Member
Aug 23, 2007
4,726
3,354
Hongera sana kwa idara ya elimu mkoa wa Singida kwa kuwafanikisha watoto wa shule za msingi mkoani hapo kwa kuwafanya wafanye vizuri mitihani yao ya darasa la saba kwa mwaka 2018 kwa kutoka nafasi ya mwisho yaani 26 mwaka 2017 mpaka nafasi ya 14 mwaka 2018

Nakumbuka mwaka 2016 singida ilitoa shule ya mwisho kabisa ktk matokeo
 

Attachments

  • MPANGILIO KATIKA MKOA-PSLE2018.pdf
    325.5 KB · Views: 98
Hongera zimwendee Dr rehema nchimbi kwa kuwashika mkono waalimu wote mkoani kwake, ingekuwa wengine wangeanza kuwalaumu walimu
 
Ndo ubovu wa elimu yetu unapoanzia.
Nani alisema Ukiwa na ranking hiyo hutapata wa kwanza na wa mwisho?
Ni kweli kuwa mtu kuwa na elimu ni lazima tufanye ranking ya hivi?
Je, ikiwa nao waliiba ili waonekane wanafanya kazi kama baadhi ya maeneo walivyofanya, je ndio elimu tuitakayo?
Bado kama Taifa nadhani baadhi ya mifumo ya kumcheka wa mwisho na kumtukuza wa kwanza haijatusaidia.
Kuna watu wagunduzi wengi walitokea kwenye udhaifu wa kuchekwa na kuonekana hawafanyi vizuri darasani lakini leo dunia inawatambua kwa kazi nzuri.
Mifumo hii baadhi ya wenzetu waliondelea na tunaowaiga walishaifuta kwa kuwa haina tija ya mda mrefu.
 
Back
Top Bottom