Hongera mke wangu siku yako ya kuzaliwa 28/01 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera mke wangu siku yako ya kuzaliwa 28/01

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by funzadume, Jan 28, 2011.

 1. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,494
  Likes Received: 2,090
  Trophy Points: 280
  kwako leo najitosa, yamoyoni kuyasema
  nitajitenda makosa, kama nikikaa kimya
  kwangu wazidi kipusa, wa-watoto wangu mama
  Hongera mke wangu, siku yako kuzaliwa

  wazidi nipa hamasa, siku zinavyoyoyoma
  Kwako mi nimenasa, siwezi kujitutuma
  macho nilipepesa, kwako wewe yakakwama
  Hongera mke wangu, siku yako kuzaliwa

  Nakumbuka agosti, mwaka tisaina kenda
  ukipita na mashosti, marafikizo mwaenda
  moyo ulipigwa shoti, na kuzidi kunidunda
  Hongera mke wangu, siku yako kuzaliwa

  nilipojaribu kuita, sauti ilikatika
  nilipatwa na utata, kwa kuona malaika
  tamaa nikakata, ulipoenda hakika
  Hongera mke wangu, siku yako kuzaliwa

  siku zilijipitia, machoni sikukutia
  ila nilijipa nia, la moyoni takwambia
  mpaka napotea njia, nilipo kufukuzia
  Hongera mke wangu, siku yako kuzaliwa

  Andiko lilitimia, siku tulipokutana
  la moyoni nikatoa, bila aibu kuona
  nilitamani kulia, uliposema hapana
  Hongera mke wangu, siku yako kuzaliwa

  kumbe hukumaanisha, ile yako hapana
  ulitaka niondosha, utafakari kwa kina
  baada ya wiki kwisha, ikawa ndio hapana
  Hongera mke wangu, siku yako kuzaliwa

  nawashukuru wazazi, ua kunizalia
  ya leo siku na mwezi, mke wangu kuzaliwa
  kwa uwezo wa mwenyezi, anazidi nikuzia
  Hongera mke wangu, siku yako kuzaliwa

  Ningependa kukuenzi, kwa kukupa hii dunia
  ila hilo siliwezi, uwezo haujatimia
  ila takupa mapenzi, ufarahie malkia
  Hongera mke wangu, siku yako kuzaliwa

  Kaditama namaliza, sina cha kuongeza
  zidi kuniliwaza, mapenzi yakupendeza
  naahidi kukutunza, watoto kuwaongeza
  Hongera mke wangu, siku yako kuzaliwa

  Funzadume mwana wa washawasha

  Shairi ili nimemtungia mke wangu kama zawadi ya siku yake ya kuzaliwa leo hii pamoja na shairi ili nimemnunulia zawadi nzuri sana na kilichoandikwa humu ni cha kweli kutoka moyoni mwangu

  nimehamua kushare nanyi leo shairi ili kufuraia siku ya kuzaliwa mke wangu
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160

  shairi limetulia! Nitakuomba uniandikie nami nataka mtokea mtoto wa Kiarabu
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  Jan 28, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  Hongera sana FD kwa ushairi mzuri mpe salam sana wife na sherehe njema ya bday
   
 4. Lily Flower

  Lily Flower JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2011
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 2,555
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Shairi zuri limesimama haswa

  Hongera nyingi kwa siku ya kuzaliwa mke wako kipenzi.
   
 5. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #5
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,494
  Likes Received: 2,090
  Trophy Points: 280
  poa mtu wako ila waarabu chapa halafu kula kona ndg zake wakikustukia wanakurushia kichomi, hawatakaki waolewe na ngozi nyeusi wale
   
 6. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  Hongera mrs funza.
   
 7. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #7
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,494
  Likes Received: 2,090
  Trophy Points: 280
  asante naona mmepishana siku chache kuzaliwa na wife wangu halafu amezaliwa siku moja na Preta what a coincidence
   
 8. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #8
  Jan 28, 2011
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Nikaribishe pilau
   
 9. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #9
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,494
  Likes Received: 2,090
  Trophy Points: 280
  thanks nitamfikishia salaam
   
 10. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Aiseeeee im proud of you man! mpaka nimehic uchozi fulani hivi! mpe hongera sana wifey
   
 11. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #11
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,494
  Likes Received: 2,090
  Trophy Points: 280
  thanks Husninyo:clap2:
   
 12. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #12
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Happy Birthday Mrs ......
  Mungu akupe maisha marefu yenye baraka tele,mafanikio na amani.
   
 13. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #13
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,494
  Likes Received: 2,090
  Trophy Points: 280
  karibu mtu mzima
   
 14. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #14
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,494
  Likes Received: 2,090
  Trophy Points: 280
  thanks nitamfikishia salaam
   
 15. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #15
  Jan 28, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kumbe mkeo Preta?

  Tumewagundua humu humu.

  Hongera Preta katika siku yako ya kuzaliwa.
   
 16. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #16
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,494
  Likes Received: 2,090
  Trophy Points: 280
  thanks i feel u
   
 17. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #17
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,494
  Likes Received: 2,090
  Trophy Points: 280
  sidhani kama ni Preta maana kuna kipindi nilimpigia akaniambia yuko njiani halafu preta huku anarusha tu msg nikajua sio yeye atakuwa pacha wake
   
 18. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #18
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Hongera kwa kipenzi wife wako na kwa kumjali!!..Feliz Compleanos Mrs.F!!!
   
 19. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #19
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Kudos kwa shairi zuri mkuu FD ; naamini utaniruhusu nami nilitumie siku ikifika! Mfikishie zetu salamu; Tunamwombea Maisha marefu kama Mlima Kilimanjaro!
   
 20. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #20
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,494
  Likes Received: 2,090
  Trophy Points: 280
  ruksa kulitumia ila itabidi ulichakachue baadhi ya mistari maana ili la kwangu linaelezea vitu ambavyo vilitokea siku za nyuma na ni la kweli mwenyewe Mrs kalisoma mpaka machozi alipomaliza nikampa simu ya Samsung Touch Screen alichanganyikiwa zaidi
   
Loading...