Rais Jakaya Kikwete akiangalia athari ya mafuriko ya Msimbazi katika eneo la Jangwani, Dar es Salaam leo wakati alipofanya ziara ya kukagua athari za mafuriko yaliyosababishwa na mvua zilizonyesha kwa siku mbili mfululizo jijini humo. Amewataka wahame. (Picha: Ikulu)
Huku kwetu kumpungia mtu kwa mkono wa kushoto ni madharau.
Mbunge wa Mafia kwa moyo aliouonyesha,,,tunataka safu ya viongozi wa juu wenye moyo kama yeye ...Tafadhali sana afikiliwe kwa Uongozi wa juu! Sio viongozi wanaonekana pale JK anapotembelea Wahanga wa mafuriko basi matumbo mbele ili waonekane kwenye vyombo vya habari..BIG UP MH. Mbunge.
apongezwe? Kwa Faraja ya mikono mitupu? Angefanya la maana kuwalinda kwa dakika hii. Angekuja na misaada kama mahema,chakula, magodoro ambavyo vitawalinda waathirika kwa sasa kisha ndo atoe na hzo ahadi hewa za viwanja. Tanzania, fungukaaaa....!
KWA nini asipongezwe? asingetokea mngesema katokea mnasema duuuu,binadamu haishi kulalama
"Uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam tayari umeandaa eneo la ekari 200
lenye viwanja 2,800 katika wilaya ya Kinondoni"
Kweli kuna watu wana skills za biashara na ni wepesi wa kubaini Business Opportunities, hapa kwenye hii picha naona kuna ambulance ya kampuni binafsi ya ulinzi imekaa tayaru tayari kula kichwa incase Dokta kaanguka.
Sawa basi, pamoja na hayo angalau muwe mnamkumbusha awe anaonyosha masikitiko, ikiwezekana muwe mnamlambisha hata ndimu ili itoe lile tabasamu aweke kahuzuni kidogo, l.o.l!
hana jipya ameshindwa kuweka utaratibu mzuri juu ya majanga leo hii anaenda kuwasanifu