Hongera Mh Rais; Umeonyesha kuwa unawajali wananchi wako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera Mh Rais; Umeonyesha kuwa unawajali wananchi wako

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by engmtolera, Dec 22, 2011.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Dec 22, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  Rais Jakaya Kikwete akiangalia athari ya mafuriko ya Msimbazi katika eneo la Jangwani, Dar es Salaam leo wakati alipofanya ziara ya kukagua athari za mafuriko yaliyosababishwa na mvua zilizonyesha kwa siku mbili mfululizo jijini humo. Amewataka wahame. (Picha: Ikulu)
   

  Attached Files:

 2. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,158
  Trophy Points: 280
  unawajari = unawajali
   
 3. ikizu

  ikizu JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2011
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hana jipya ameshindwa kuweka utaratibu mzuri juu ya majanga leo hii anaenda kuwasanifu
   
 4. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #4
  Dec 22, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa si amewahaidi wahanga atawatafutia viwanja sehemu nyingine,ebu ngoja tumpe mda awatafutie viwanja wakazi wa mabondeni
   
 5. Criss

  Criss JF-Expert Member

  #5
  Dec 22, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 825
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sina sababu ya kumpongeza.....kwa kua hastahili kupongezwa ...na kwakua wao ni watu wakuchukulia mambo kikawaida kwajina la Mungu nawahakikishia siku moja na yeye tutaenda kumuokolea juu ya mabati huko magogoni.

  Kama Baba unaefahamu wajibu wako na ukajifanya kutokujali mazingira hatarishi inayoishi familia yako siku wakipatwa na madhara uliyoyatarajia eti unakurupuka na kuja kuwaona pengine hata kuwapa pole hahahahaaaa hapo kama sio kuwakashfu ni nini unafanya?

  Hapo ni nini asichokijua hata astahili kupongezwa?
  kama kiongozi mkuu wa inji ni hatua gani zamsingi alizozichukua kukabiliana na tatizo husika?

  Binafsi labda nimpongeze kwa kuwalinda watendaji wenye afya mbovu za mwili na akili walio majasiri wa kuilea Miundo mbinu ya miaka 47 kwa kuishiwa mbinu na mikakati inayoendana na wakati husika .

  Hivi hii inaingia akilini kwa inji inayosherehekea miaka arobani inasumbuliwa na mvua isiyofikia hata Ml_210?
   
 6. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #6
  Dec 22, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  atakuwa Mnyamwezi huyo bi FF... Mwachie tu..
   
 7. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #7
  Dec 23, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Thursday, 22 December 2011 20:29[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  0digg
  [​IMG]
  Rais jakaya Kikwete(katika) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano ya Jamii .Stephen Wasira(kushoto),Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik,Meya wa Ilala jerry Slaa,waziri wa Tamisemi,George Mkuchika na Waziri wa ulinzi(kulia)Hussein Mwinyi wakiwa wameinamisha vichwa kuwakumbuka waliokufa kwenye mafuriko jana.Picha na Fidelis Felix​
  WALIOKUFA WAFIKIA 30,MAELFU WAKOSA MAKAZI
  Waandishi Wetu
  RAIS Jakaya Kikwete ametoa tamko kwa wakazi wanaoishi mabondeni, kwa kuwataka wahamie kwenye maeneo mapya watakayopangiwa ili kuepuka madhara zaidi.Wakati Rais akitoa tamko hilo, takwimu zilizokusanywa na gazeti hili kutoka mamlaka mbalimbali tangu kuanza kwa mvua hizo mnamo Desemba 20, zinaonyesha waliokufa ni 30 lakini, Rais aliambiwa kuwa waliokufa ni watu 20.

  Akizungumza jana katika shule ya msingi ya Mchikichini, Jijini Dar es Salaam alipokwenda kuwapa pole waathirika wa mafuriko yaliyotokana na mvua zilizonyesha kwa siku tatu, Rais Kikwete aliwataka watu kuhama mabondeni.

  Shule ya Mchikichini ni miongoni mwa vituo vilivyotengwa kwa ajili ya kuwahifadhi waathirika wa mafuriko hayo.
  Rais alisema: “Wakati Watanzania tunaomba usiku na mchana mvua iweze kunyesha ili mazao yaweze kustawi, wapo wenzetu ambao wanaomba jua liwake mwaka mzima.”

  Alisema wanaombea jua liwake mwaka mzima, ili mvua isinyeshe kwa sababu wamejenga nyumba zao mabondeni ambako hawaruhusiwi.“Acheni kuishi kwa mashaka, ukiona wingu jeusi unaanza hofu, kila siku adui yako wewe ni mvua, tafadhali hamieni kwenye maeneo salama yatakayotengwa,”alisema Kikwete.

  Mkuu huyo wa nchi aliongeza kwamba, katika maeneo mengine mafuriko yametokea kwa sababu watu wamejenga kwenye maeneo ya wazi na maeneo ya barabara.

  “Maeneo hayo yakijengwa maji yanatafuta sehemu ya kupita, yakishindwa yanabomoa nyumba na miundombinu mingine,” alisema Kikwete.Alisema yote hayo yanafanyika huku viongozi wakiwemo watendaji wa mitaa na kata, wakiwa wanaangalia.

  “Watu wanajenga na kuziba barabara, wengine wanajenga kwenye viwanja vya wazi kuna madiwani, watendaji wa kata na watendaji wa serikali za mitaa lakini hawachukui hatua zozote,” alisema Kikwete.

  Rais Kikwete alisema hata kwenye maeneo hayo yanapotokea maafa, kazi ya uokoaji inakuwa ngumu kwa sababu maeneo yote yamejengwa nyumba.Alisema serikali itahakikisha waathirika wa mafuriko hayo wanapata huduma zote za kibinadamu zinazohitajika wakiwa katika vituo vua huduma.

  Kabla ya kuzungumza na waathirika hao, Rais Kikwete alikagua maeneo ya jiji la Dar es Salaam yaliyokumbwa na mafuriko hayo kwa kutumia Helkopta.

  RC Sadik

  Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik alimweleza Rais Kikwete kwamba ekari 2,000 za ardhi, zimetengwa katika wilaya ya Kinondoni kwa ajili waathirika wa mafuriko hayo.

  Alisema katika eneo hilo vitapatikana viwanja 2,800, ambavyo vitagawiwa kwa watu hao waliopatwa na maafa.

  “Mheshimiwa Rais wapo baadhi ya watu wanaoishi mabondeni waliowahi kupewa viwanja ili wahame lakini, hawakufanya hivyo na viwanja walivyopewa waliviuza,” alisema Sadik.Alisema katika bonde la Msimbazi kila mwaka yamekuwa yakitokea maafa, ingawa hayakuwahi kutokea maafa makubwa kama ya sasa.

  “Hatuwezi kuwa watu wa kusubiri maafa kila mwaka, ni lazima hatua sasa zichukuliwe ili wakazi wa mabondeni waweze kuhamia katika maeneo salama,” alisema Sadik.

  Alisema kwa kuwa shule za msingi zitafunguliwa katika kipindi cha wiki mbili zijazo, waathirika hao watahamishiwa kwenye eneo maalum litakalojengwa kwa mahema.Sadik akizungumzia misaada ya kibinadamu ambayo imeanza kutolewa, alisema wameanza kugawa vyakula na maji.

  Alisema mablanketi 1,600 yameanza kutolewa na magodolo yataanza kugawiwa katika maeneo mbalimbali hivi karibuni huku huduma za afya zikiwekwa katika kila kambi.Kuhusu miundombinu iliyoharibika, Sadik alisema wahandisi wa mkoa wameanza kufanya tathimini kufahamu uharibufu na hatua kuchukua.

  “ Kuna madaraja kadhaa yamebomoka na barabara kuharibika, wahandisi wetu wanafanya tathimini ili tuweze kuchukua hatua za ujenzi,” alisema Sadik.

  Waliokufa wafikia 30
  Wakati Rais akielezwa waliokufa ni 20 takwimu ambazo Mwananchi imezikusanya kutoka mamlaka tofauti zinaonyesha kuwa mvua hizo, zimesababisha vifo vya watu 30 na majeruhi 50.Takwimu hizo zilipatikana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali ya Amana, Hospitali ya Mwananyamala na Hospitali ya Temeke.

  Hata hivyo, Sadik alimweleza Rais Kikwete kuwa waliokufa katika mafuriko hayo ni watu 20 na walioathirika ni 4,909.Hata hivyo, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema jana kuwa tangu mvua zilipoanza kunyesha, mkoa wake wa kipolisi wa Kinondoni, kuliripotiwa vifo 13, vikiwamo vitatu vya watu wa familia moja ya Abeid Mntangi, mkazi wa Kimara.

  Alisema familia hiyo ilikumbwa na maafa hayo baada ya ukuta wa nyumba yao kuwaangukia, kwa kusukumwa na maji ya mvua.Kenyela alisema katika eneo la Kimara Baruti, ulikutwa mwili wa mtu mmoja mwanaume mwenye umri wa kati ya miaka 55 na 60, ukiwa umekwama kwenye mizizi.

  "Maiti hiyo ilikutwa haina nguo na haijatambuliwa vilevile, eneo la Kawe mtu mmoja mwenye asili ya Kimasai miaka kati ya 40 hadi 45 mwili wake umekutwa mto Kawe nao pia uko Mwananyamala," alisema.Alisema eneo la Tabata Ami, mwili mwingine wa mwanaume mwenye umri kati ya 35 hadi 40 aliyekuwa amevaa fulana nyeupe na jinzi uliokotwa.

  Katika eneo la Kigogo kwa Dua Said, Kamanda Kenyela alisema uliokotwa mwili wa mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 12 ukiwa pembeni ya mto Msimbazi.Kamanda Kenyela alisema mwili wa Khalid Ali (22) ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mgulani, ulikutwa ukielewa kwenye Bonde la Mto Msimbazi.

  Katika eneo la Magomeni Suna, mwili wa mtu aliyetambuliwa kuwa ni Mwinyi Makame (20) ulikutwa pembeni mwa bonde la Msimbazi.Kenyela alisema maiti za watu wanne ambazo bado hazijatambuliwa na miili mingine imehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala.

  Alisema katika eneo hilo la Magomeni Suna, pia ulikutwa mwili wa mtu aliyetambuliwa kwa jina moja la Athuman umri (22) ambaye ni fundi magari na mwili huo pia umepelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

  Hosipitalini Dar
  Kwa upande wake Ofisa Uhusiano Msaidizi wa Hospiali ya Muhimbili, Jeza Waziri alisema katika hospitali hiyo kulipokelewa maiti 15 na majeruhi 11.Waziri alisema kati ya maiti hao, wanawake ni watatu na wanaume 12. Alisema majeruhi saba kati ya hao 11 bado wamelazwa na kuendelea na matibabu hospitalini hapo.

  "Maiti zilizotambuliwa ni saba na ambazo hazikutambuliwa majina ni nane. Majeruhi wote walilazwa na kuruhusiwa,' alisema Waziri.Alitaja maiti waliotambuliwa kuwa ni Hidaya Amri (1) mkazi wa Jangwani, Hamisi Nyao (19) mkazi wa Vingunguti, Nyanda Kiangi (35)Mkazi wa Kigogo na mwingine aliyetambulika kwa jina la Bakari (10).

  Wengine ni Nia Abrahamani (24) na Athumani (26) wote wakazi wa Magomeni.“Kuanzia jana (juzi) hadi saa 7.10 mchana leo (jana), tumepokea maiti 15 ikiwamo maiti moja ambayo inakuja sasa hivi ninavyozungumza na wewe,”alisema Waziri.

  Katika hospitali ya Amana ambayo ipo katika Manispaa ya Ilala, kulikuwa na kifo cha mtu mmoja na majeruhi 45.
  Dk Mwaluka Shanny wa hospitali hiyo, alisema kumekuwa na ongezeko la majeruhi kutoka 10 katika siku ya kwanza mpaka 45 jana.

  Dk Shanny alisema wengi wa majeruhi hao wanatoka katika maeneo ya Kigogo na kwamba baadhi yao walipata mshituko na wengine majeraha madogo.

  “Mpaka leo (jana) saa 8:00 kamili mchana, tumepokea majeruhi 45, kati yao yupo mwanamke mmoja (60) ambaye hali yake ni mbaya kutokana na kupata mshituko wa moyo,” alisema Dk Shaany.

  Katika hospitali ya Temeke tangu mvua hizo zianze juzi, kuliripotiwa maiti moja na majeruhi wawili. Taarifa hizo zilitolewa jana na muuguzi wa zamu wa hospitali hiyo, Shamim Londo.

  Kambi za wathirika
  Baadhi wa waathirika katika kambi ya Shule ya Msingi Gilman Rutihinda iliyoko Kigogo, wamelalamika kwamba tangu wafike kambini hapo juzi hawajapewa huduma yoyote, hata chakula.

  Wakati wenzao wa shule ya Mchikichini wakiwa wamenza kupata chakula, wao walisema hawajapata chakula wala maji licha ya viongozi kadhaa kuwatembelea.

  “Viongozi wanakuja kutupa pole lakini sisi hatuhitaji pole ya mdomo tuna watoto wana njaa tangu jana hawakula chochote tunaomba msaada,” alisema Mwasa Samwel.Waathirika wengine walimuunga mkono mwenzao na kuongeza kuwa licha ya kukosa chakula pia hawana mashuka, vyandarua na nguo.

  “Tumekuja kama tulivyo, tunaomba msaada, hatuna chakula hatuna nguo wala fedha vyote vimechukuliwa na mafuriko,” alisema Habiba Juma ambaye ana watoto wanne.

  Wakati huohuo familia 15 zilizohifadhiwa katika Shule ya msingi Msimbazi baada ya nyumba zao kuzolewa na maji zimelalamikia kukosa misaada mbalimbali kikiwamo ya chakula.Fulugensi Kahima (37), mkazi wa Jangwani alisema msaada wa makazi waliopewa haitoshi na kwamba wanahitaji chakula hasa kwa watoto ambao ndio wamedhurika kwa kiasi kikubwa.

  “Tumepewa hifadhi hapa lakini tangu tufike katika kituo hiki tumeishia kupewa juisi na maji lakini mpaka sasa hatujapata msaada wowote wa chakula zaidi ya kwenda kujitafutia wenyewe,” alisema Kahima.

  Mwananchi ilishuhudia sehemu hiyo waliopewa waathirika kwa ajili ya hifadhi ikiwa katika hali mbaya na hakuna vitu muhimu kama magodolo huku mikeka ikiwa ndio inatumika kama sehemu ya malazi.

  Moja ya sehemu ambayo Mwananchi ilishuhudia ni katika chumba kimoja cha darasa, ambacho familia hizo zimehifadhiwa kukiwa na mchanganyiko wa wazazi na watoto.Familia hizo mbazo kwa sehemu kubwa zinatoka katika eneo la Jangwani walikutwa na mwananchi wakiwa katika maandalizi ya kwenda kufitajutia kipato.

  Dk Slaa: Janga liwe funzo
  Kwa upande wa Chadema, kimetoa pole kwa wananchi waliokumbwa na maafa katika jiji la Dar es Salaam, Mbeya na Dodoma na kuishauri serikali kujiandaa kuyakabili majanga makubwa.

  Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema katika taarifa yake kuwa hawaridhishwi na hatua zilizochukuliwa na serikali kuwahudumia waathirika hao.

  Alisema kutokana na wananchi kupoteza maisha, mali na miundombinu mingi kuharibika Chama wanaona kuwa hilo ni janga la kitaifa na kutaka serikali kuhakikisha inawahudumia kwa umakini wananchi wote walioathirika.

  Dk Slaa alisema kutokana na hali hiyo, serikali inatakiwa kutunga sheria mpya ya ujenzi na kuweka viwango vya ujenzi vyenye hadhi ya kimataifa na hasa ujenzi wa kuta na majengo marefu na kuhakikisha ujenzi holela haujitokezi kwenye miji na majiji .

  Alisema serikali inatakiwa kuhakikisha miji mikubwa inakuwa na mtandao wa mabomba ya maji ya dharura inawekwa ili kukabiliana na majanga ya moto na mafuriko yanapotokea.

  Aliongeza kuwa serikali inatakiwa kujiandaa kukabiliana na magonjwa ya milipuko kama vile kuhara, kipindupindu na mengineyo ambayo yanaweza kujitokeza kutokana na janga hilo kuwa kubwa.

  “Kitengo cha maafa kiwe na vifaa wakati wote kwa ajili ya uokozi, maeneo ambayo hali inakuwa tete pamoja na kutoa elimu jinsi kutumia vifaa, ili kuweza kujiokoa na sio kuacha hali iwe kama ilivyojitokeza jijini Dar es Salaam, waathirika waliposhindwa kutumia hata majaketi ya uokozi,“ alisema.

  Alisema kutokana na janga hilo kugusa maisha ya watu wote, serikali kuwekeza nguvu nyingi zaidi kuwasaidia wanachi.

  Dk Slaa alisema taifa limeonyesha dhahiri kuwa halijajiandaa kuyakabili majanga na kwamba hata vyombo vya ulinzi na usalama vimeonekana kutoandaliwa kimfumo na kinyenzo kukabiliana na majanga.

  Alisema serikali inatakiwa kuondoa kudhaifu mkubwa uliooneshwa na Taifa, ili wanachi waendelee kuamini kile kilichopatikana baada ya miaka 50 .

  Alisema kitengo cha maafa kinaonekana hakikuandaliwa vizuri kutokana na kushindwa kukabiliana na majukumu yanavyopaswa kufanywa wakati wa matatizo makubwa ya maafa.

  Dk Slaa alisema iwapo chombo kilichopangwa kushidwa kufanya kazi yake serikali inatakiwa kukiangalia kwa makini ili kuweza kuhakikisha jamii inakuwa na imani pindi tatizo linapotokea.

  Alisema matatizo kama hayo yanatokana mifumo mibovu ya kujulisha umma kuhusiana na majanga makubwa ndio sababu ya kuharibiwa kwa mali za wananchi na kwamba, serikali inatakiwa kuweka kipaumbele kuwajulisha wananchi ili kuweza kupunguza maafa.

  Habari hii imeandaliwa na Raymond Kaminyoge, Keneth Goliama, Aidan Mhando, Pamela Chilongola na Ibrahim Yamola

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 8. Ambakisye Lazar

  Ambakisye Lazar Member

  #8
  Dec 23, 2011
  Joined: Sep 5, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  apongezwe? Kwa Faraja ya mikono mitupu? Angefanya la maana kuwalinda kwa dakika hii. Angekuja na misaada kama mahema,chakula, magodoro ambavyo vitawalinda waathirika kwa sasa kisha ndo atoe na hzo ahadi hewa za viwanja. Tanzania, fungukaaaa....!
   
 9. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #9
  Dec 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Pongezi kwa lipi? unachekesha - ff!
   
 10. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #10
  Dec 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Handsome Boy!

  Anashindwa hata "kuigiza" kuhuzunika?
   
 11. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #11
  Dec 23, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,079
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  alafu alikuja mtu na kuachia uzi eti Mh Rais Dr. Jk yupo vacation!.. watu wengine bana..! hongera sana JK !! "ᵀᴴᴱ'ᴼᴿᴵᴳᴵᴻᴬᴸ✯
   
 12. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #12
  Dec 23, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Big up Jk kwa kuwatembelea waathirika na kuzungumza nao. Tunafarijika


   
 13. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #13
  Dec 23, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Kwa kuwa kajitokeza hapo basi haiwezi kuwa alikuwa "vacation"? Au kwako wewe "vacation" ni wapi au nini?
  Hata kama ni kuganga njaa basi muwe mnatumia na akili japo kidogo.
   
 14. l

  luckman JF-Expert Member

  #14
  Dec 23, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  anawajali kwa lipi? wambagara hadi leo vilio, gogola mboto siku moja baada alipanda ndege akaenda ethiopia kusuluhisha eti mgogoro wa ivorycoast, na bado wanaishi kwenye tent, na sio hao tu, hii ni dar mkoani ndo usiseme, kiujumla thread yako kichefuchefu unaosha visivyoosheka!
   
 15. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #15
  Dec 23, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  lakini tukumbuke kuwa si mala ya kwanza watu wa mabondeni DSM kuelezwa wahame,tumekuwa tukilazimisha kukaa mabondeni eti tuwe karibu na Mji hilo ndilo tatizo letu kubwa,ni mpaka tukumbwe na matatizo ndio tutaona ubaya wa kuishi mabondeni

  Hongera Mh Raisi kwa kuwapatia viwanja,wagome tena kuhama
   
 16. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #16
  Dec 23, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,512
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Nimehisi kichefuchefu!
   
 17. J

  J.Mindu Member

  #17
  Dec 23, 2011
  Joined: Dec 22, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli Mh.rais ameonyesha upendo wa dhati kwa wahanga,kikubwa atekeleze ahadi yake ya kuwatafutia viwanja ikiwezekana hata kuwasaidia uwezo kwani walio wengi ni wanainchi wa kipato cha chini ndio mana hata makazi yao yalioathirika ni ya kawaida sana.Hongera rais.
   
 18. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #18
  Dec 23, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  wewe unayelalamika umetoa mchango gani kwa waathirika?umeshiriki vipi? tabia ya kulalamika lalamika ni ya kike.....na kupinga kila kitu ni ushamba mana mshamba huwa hakubali kue;limishwa wala hajui kuwa hajui,ni ubishi na kupinga tuuuuuuuuuuuuuu.
   
 19. s

  sawabho JF-Expert Member

  #19
  Dec 23, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 948
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono hoja. Utaratibu wa watu kuishi mabondeni hususani katika Jiji La Dar es Salaam umekuwa ukipigiwa kelele sana na Wakuu wa mkoa wote waliopita, lakini wanaonekana kama wanaingilia maisha binafsi ya watu hadi kufikia kusemwa vibaya. Huu ni wakati mwafaka sasa kwa watu waishio mabondeni huo Dar kuhama kuliko kusubiri siku ambayo Katrina itatokea, ingawa Katrina inaadhiri hata walio katika maeneo yaliyoinuka, lakini mabondeni ni inakuwa mbaya zaidi.
   
 20. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #20
  Dec 23, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  acha nisimpongeze kikwete kwa kuwa ni wajibu wake kwa alichokifanya lakini simlaum kwa kuwa amewafariji waathirika.hili tukio ni NATURAL CALAMITY,HAKUNA TUWAHIMIZE WANAOISHIN MABONDENI HASA KANDO KANDO ZA MITO WAHAME.
   
Loading...